Kwenye hili wakristo mna la kujifunza

Kwenye hili wakristo mna la kujifunza

Twende mahakamani leo hii nani wanaongoza kwa kudai talaka? Tena zenu mnojiita wasomi ndo hazidumu kabisaaa mna elimu mnaiacha kwenye vyeti tu sio matendo
Sasa nyie si mnaachana kwa talaka tatu tu hata mahakamani hamuendi so ndoa za kiislamu ni chache mahakamani kwa sababu hamfuati utaratibu mnamalizana kwa kadhi. Si unakumbuka ishunya dokta mwaka kesi ilikua kwa sheikh wa Dar.

Wasomi tunafuata process na tunajua kuna kugawana mali ukishangaa unaweza geuka masikini dakika sifuri....

Kusoma raha sheikh.... hata wale waislamu waliopiga shule wanafuata sheria na wana mke mmoja....

Si unaona matajiri wa kiislam kina Mo na wengine.
 
uzito wa ndoa kwenye Christianity ni tofauti kabisa na islam, ndoa ya islamic pia inavunjika mara moja wakati wowote ule, kama unaelewa Christianity kuna ubatizo, komunio na ndoa hizo ni hatua muhimu katika maisha ya Christian na ndiyo maana zote zina sherehe ubatizo una sherehe, komunio ina sherea na vilevile baba lao ndoa pia, hivyo ni tofauti kabisa, muslims hawana kitu kama hicho na ndoa kwa muslims haina maana yoyote ile na ndiyo maana inaweza kuvunjwa muda wowote ule na pia inaweza kufungwa hata na wanawake 4 siyo kitu special kwani kinaweza kurudiwa mara nyingi kwa muslims vs Christians ndoa ni hatua muhimu sana ktk maisha ya Christians, hivyo ndiyo maana Christians wanasherehekea na ndiyo maana ya maisha, watu wanaishi wakiwa na kumbukumbu ya ndoa yao ilivyokuwa wana album na picha nzuri za sherehe wanazitunza kama kumbu kumbu na hii yote ndiyo maana ya maisha, inaleta faraja.

fikiria ulishawahi labda kuangalia picha za graduation yako sekondari au hata chuo miaka iliyopita hauoni kama inaleta kumbu kumbu na furaha fulani kwamba ni ukurasa ktk maisha yako ambayo hauwezi kurudi tena ni tofauti kama hauna, hivyo hiyo ndiyo moja kati ya sabubu pia ya Christians kufanya ndoa kuwa siku muhimu kabisa ktk maisha yao kwani haitakuja kutokea tena, kwa hiyo ni sawa kusherehekea ...
Hata kwenye ukristo mnaweza mkafungishwa ndoa na kiongozi wa dini chapu chapu tu. Kufanya sherehe ni mbwembwe tu sio hitaji la lazima kwenye dini
 
Kwa wakristu ndoa inaishia kanisani, Haichukui hata masaa ma3, Hakuna wali wala pilau ni wapendanao wa2, Ndugu, Mchungaji na pete, Shughuri imeisha.

Baada ya hapo, ni sherehe ambapo hizo ni mbwembwe zako, ila ukiamua kutoka kanisani kwenda gheto hakuna shida maana cheti unakua nacho kabisa.
 
Sisi wakristo tunaoa kwa gharama lakini mahakamani zimejaa kesi zetu za kudaiana talaka
 
Kumekuwa na ndoa zinazofungwa kiislam ila sherehe yake inafanyika ukumbini huku bi arusi akivalia shela kama mkristo na bwana naye akivalia suti ila huko walikofungiwa ndoa na sheikh walivalia mavazi ya kiislam, ukumbini wakavalia kikristo. Huko ukumbini inafanyika sherehe ya gharama kubwa, watu wanakaa meza moja watano, vinywaji vya kila aina kabla ya msosi. Bufee ni ndefu, misosi ya kila aina mpaka inabidi tu uchague vya kula. Ni ufahari mtupu, mbwembwe ni nyingi. Cha ajabu huoni uislam ukumbini watu wamevalia kimagharibi wote
Suti sio vazi la kikristo, na kanzu sio vazi la kiislamu
 
Hata kwenye ukristo mnaweza mkafungishwa ndoa na kiongozi wa dini chapu chapu tu. Kufanya sherehe ni mbwembwe tu sio hitaji la lazima kwenye dini

mbwembwe maana yake nini? kusherehekea baada ya kufunga ndoa ni utamaduni wa Christians, ni sehemu ya maisha isitoshe kwa nini ikusumbue wengine wakisherehekea? wewe nenda kwa shehe fanya ya mkeka basi maliza nendeni nyumbani kesho ongeza mwingine kama manara hivyo hiyo, kwa nini iwe ishu kwako wengine wakipenda kusherehekea tukio muhimu kabisa ktk maisha yao? ...
 
Harusi za bomani nazo ni simple kuliko za kiislam. Bomani mnaenda wanne tu tena kwa miguu, bwana na bi arusi na mashahidi wawili. Kisha mnarudi nyumbani bila shangwe na mbwembwe, msosi unaoliwa ni wa kawaida tu ulioko kwenye ratiba ya mlo wa siku. Ila kuna watu wanafungia bomani, sherehe ya kifahari inaenda kufanyika ukumbini, wanavaa kama wa makanisani. Sherehe za harusi za kikristo zinaigwa na waislam na wa bomani na wale wa kimila
Mimi siku ya kuoa nilienda ukweni na msafara wa wapambe wangu. Nikatoa mahari, tukapiga msosi, zikafuata story mbiki tatu, nikaondoka na jiko. Ilikua shughuki ya familia mbili tu hata majirani wanaweza wasijue. Hapakua na mbwembwe za sherehe, kuvalishana pete wala kusainishana mikataba
 
Kuna jamaa mslamu kaoa ndoa moja simple sana yani, no mc, no mbwembwe!

Wakati wa sa1 kasoro ile kufuturu jamaa kaoa hapohapo, watu wametulia kwenye mkeka na vikombe vya uji wanajitafunia zao maandazi, shehe aliefungisha ndoa kapigwa buku5 tuu ya maji.

Yani ndoa mpaka inakamilika haijazidi hata elfu50.

Hawa jamaa kwa upande huu nawakubali sana.

Wakristo sasa utakuta ndoa inagharimu mamilioni.
Point of correction! Kwa wakristo kinachowagharimu sio ndoa ila ni sherehe za harusi ambazo sio sehemu ya ndoa hata kidogo.
 
Kazi ya pesa ni kutumika, ya nini kutafuta pesa kwa shida halafu mfurahie maisha kwa kikombe cha uji na andazi, that's madness!!
Wengine huwa wanakopa au wanaanza kusumbua kutaka michango. Mfukoni ana milioni 4, bajeti ya harusi milioni 20. Mtu hauna ili wala lile unajikuta tu umeungwa kwenye kundi la michango ya harusi.
 
Ndoa ya uji hiyo kuchepuka kunaruhusiwa kwa mwanamke sasa kazi kwako.
Kupanga ni kuchagua..!!
 
mbwembwe maana yake nini? kusherehekea baada ya kufunga ndoa ni utamaduni wa Christians, ni sehemu ya maisha isitoshe kwa nini ikusumbue wengine wakisherehekea? wewe nenda kwa shehe fanya ya mkeka basi maliza nendeni nyumbani kesho ongeza mwingine kama manara hivyo hiyo, kwa nini iwe ishu kwako wengine wakipenda kusherehekea tukio muhimu kabisa ktk maisha yao? ...
Umepaniki? Sherehe ni mbwembwe tu. Ndoa inaishia pale kanisani. Kiongozi wa dini, wasimamizi, pete na mkataba basi.
 
Kwa wakristu ndoa inaishia kanisani, Haichukui hata masaa ma3, Hakuna wali wala pilau ni wapendanao wa2, Ndugu, Mchungaji na pete, Shughuri imeisha.

Baada ya hapo, ni sherehe ambapo hizo ni mbwembwe zako, ila ukiamua kutoka kanisani kwenda gheto hakuna shida maana cheti unakua nacho kabisa.
Hawajui kuna watu wanafunga ndoa na kurudi nyumbani.
Na wengine, kuna sherehe zinaandaliwa na kanisa.
Ndoa hata nne zote zinafanyiwa sherehe moja

Kuna options nyingi tu ila inategemeana na uwezo wako. Ukitaka kufurahisha macho ya watu, RUKSA na ukitaka ndoa ya uwezo wako. RUKHSA PIA
 
Back
Top Bottom