Hilo song tam sana hasa video yakeNiko hapa natazama " YOU ROCK MY WORLD "
Acha masihara basiii 😄Amemzidi GOAT Jay Z?
Niko serious mkuu 😂😂Acha masihara basiii 😄
Mbona kama Jay Z tuKatika peak ya umaarufu wake miaka ya 1980 na 1990, watu wengi walimwelezea Michael Jackson kama binadamu maarufu zaidi duniani. Jina lake na sura yake vilitambulika karibu kila nchi, hata maeneo ambayo watu hawakuzungumza Kiingereza au walikuwa na exposure ndogo sana kwa Western media.
Watu hawaelewi Michael Jackson alikuwa maarufu kiasi gani. Hakuna mtu aliyewahi hata kumkaribia. Alijulikana katika kila nchi ya dunia ya tatu pamoja na nchi za Magharibi. Hakuweza kufanya public appearances kwenye nightclubs au restaurants kama celebrities wengine. Hakukuwa na kukaa courtside kwenye mechi za NBA au ringside kwenye boxing events. Kwa nini? Kwa sababu mashabiki wangesababisha chaos tu na sehemu nzima ingefungwa. Watu hawaelewi level hiyo ya fame.
Dunia nzima ilitune in kutazama premiere ya Thriller, kabla hata ya social media, YouTube na vitu kama hivyo. Aliweza kuimba, kucheza, kutengeneza choreography zake mwenyewe, na mara chache sana alikuwa akifanya interviews. Aura yake ilikuwa kwenye level nyingine kabisa. Viongozi wa dunia walikuwa wanaomba kukutana naye. Barabara zilikuwa zinafungwa alipokuwa anakaa hotelini, na mambo kama hayo.
Hakuna aliyekuja kabla yake wala baada yake ambaye anaweza kulinganishwa naye.
Watu walikuwa wanazimia walipomwona ana kwa ana. Ilikuwa kitu cha ajabu sana na ambacho hakikuwahi kushuhudiwa hapo awali. Kutakuwa na Michael Jackson mmoja tu, na hatutawahi tena kushuhudia mchanganyiko wa talent na aura kama yake. Never.
Jay Z wangapi wanamfahamu duniani?Mbona kama Jay Z tu
M.JMichael Jackson hakuwa tu msanii mkubwa; alikuwa jambo la kipekee lililotikisa dunia nzima.
Jay Z wangapi wanamfahamu duniani?
Jigga anatembea mtaani watu hawashtuki?
MJ alikuja Tz na Jay Z alikuja pia
MJ alipokelewa na Rais Mwinyi na Waziri wa Foreign, Diria wakati Jay Z alipokelewa na Joseph Kusaga na Ruge FM!
Acheni hizo lame comparisons!
King of Pop hakuhitaji Kiingereza ili kutawala ulimwengu. Watoto katika vijiji vya India, familia nchini Brazil, watu wa China, vijana wa Japan, Mexico na Nigeria, pamoja na wengi ambao hawakukua wakizungumza Kiingereza, walikuwa wakisikiliza Thriller, Billie Jean na Smooth Criminal mara kwa mara. Wengi wao walijua kila hatua ya moonwalk, kila “hee-hee,” na kila mpigo wa muziki wake kabla hata hawajajifunza Kiingereza cha msingi.
Muziki wake ulikuwa na mvuto wa kipekee. Ulivuka mipaka yote ya lugha kana kwamba haikuwepo kabisa.
Hivyo ndivyo Michael Jackson alivyokuwa mkubwa. Mamilioni ya watu duniani kote walimfahamu Michael Jackson muda mrefu kabla hawajajua English. Sauti yake ilikuwa “lugha” ya kwanza waliyoipenda.
Hakuna mwingine aliyewahi kufanya jambo kama hilo.
Mpaka sasa anaongoza streaming kwenye Spotify na Biopic yake “Michael” iliyotoka April inaongoza kwa mauzo duniani kote na hii ni miaka karibu 20 tangu amefariki 2009
Hao wa sasa kina Chris Brown, Usher Raymond, Bruno Mars, Justine Timberlake, Beyonce, Taylor Swift na wengineo wanakwambia MJ was influential kwenye career zao
Legend forever. 👑