Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
Kuna mtu ananielewa?
Ni kawaida kwa asili ya binadamu kutaka kuwa na hulka ya utimilifu na kutamani mazuri pekee.
Ndiyo maana katika maongezi yetu mara nyingi ni ligi na ushindani, hatuongei ili kusuluhisha bali tunajitetea kwa kuhakikisha tupo sahihi.
Matokeo yake ni vigumu mno kumaliza mijadala iliyo mingi kwa amani. Kila mmoja anataka kuwa sahihi, hata kama anasema uongo kwa kujua ama kutojua.
Hii haina afya, huwezi kushinda kila ligi. Hata ukishinda ikiwa ni kwa Hila huwezi kuwa na amani, tujifunze.
Tunapozungumza kitu iwe ni kwa uhakika, kwa lengo la kutatua na si kushindana.
Wasalaam!