Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Katika majukwa ya kimataifa kuna masuala mengi huwa hayapaswi kuzungumzwa au kauli tata kutolewa hadharani.
Majukwaa ya kimataifa ni pamoja na majadiliano na waandishi wa habari wa kimataifa, vikao vya wazi na viongozi na taasisi mbalimbali, makongamano pamoja na mikutano mikubwa na midogo, iso rasmi na ilo rasmi.
Hivi karibuni Raisi Joe Biden alitoa kauli kwamba raisi Putin ni mhalifu wa kimataifa na utawala wake wapaswa kuondolewa, kauli ambayo mara moja ilirekebishwa na kupigwa msasa na maofisa wa Ikulu ya Marekani pamoja na waziri wa masuala ya kigeni bwana Blinken.
Huo ni mfano mmojawapo wa kauli tata kurekebishwa moja kwa moja na kuonekana au kueleweka kwa namna ingine ingawa kauli hiyohiyo itolewapo kwa nchi kama Libya, Syria au kataifa kadogo, hugeuka kuwa ni kweli na hatua za kuishambulia nchi hiyo huchukuliwa.
Viongozi wengi duniani hutumia muda mwingi kujiandaa kutoa hotuba, kauli au hata dondoo kupitia vyanzo mbalimbali na mitandao ya kijamii kama twitter.
Hapo ndipo umuhimu wa wasaidizi wa karibu kwenye masuala ya diplomasia, uchumi, ujasusi na mengine unapotambulika.
Kitendo cha raisi Samia kubeba masuala yanohusu siri za nchi (kutokuelewana na hayati Magufuli kwenye suala la covid-19) na kuzieleza hadharani nchini Marekani, chahitaji kuangaliwa.
Kwa wataalam wa lugha la siha (body language) waweza kusema pasi na shaka kwamba raisi Samia anatumia jina la hayati Magufuli kujimaarisha kisiasa, na kidiplomasia.
Lakini kufanya hivyo kuendane na umakini wa kutumia akili na welevu bila kujiathiri mwenyewe maana itaonekana wafanya vibaya na makusudi na umedhamiria.
Raisi Samia kwa kujadiliana na wasaidizi wake bado wana nafasi ya kuhakikisha siku zijazo wanafanya uhakiki wa yale ya kuyazungumza majukwaani na yale ya kuzungumzwa kwenye faragha yaani "off air" or "in private or between four walls or on/off record".
Kwa mfano, katika mahojiano na mwandishi wa New York Times, Raisi Samia angetumia lugha ya kidiplomasia zaidi kwa kuonyesha kutotaka kuongelea suala la mgogoro au kutokuelewana na mtangulizi wake.
Mwandishi wa New York Times ni mwerevu na angeelewa lakini kutokana na uzito wa ajenda yake ya kuonyesha utofauti wa raisi Samia na hayati Magufuli ndo maana alipiga suali hilo, ingawa bado kulikuwa na nafasi ya kulikwepa.
Wakati wa utawala wake aliekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete aliwahi kuhojiwa na mwandishi wa CNN Christiane Amanpour juu ya suala la kuruhusu au kuhalalisha ushoga nchini Tanzania.
Mzee Jakaya Kikwete akiwa ni mwanadiplomasia mbobezi hakutaka kujibu swali hilo moja kwa moja ila akajibu kwamba " our country at the moment is not ready, when is ready we will think about it" na hilo suali likaishia hewani.
Raisi Samia bado ana nafasi ya kujiweka sawa anapokuwa katika majukwaa ya kimataifa ambayo yana watu wenye uelevu na akili nyingi na jambo dogo huweza kulikuuza na kulifanya jambo kubwa.
Isitoshe Raisi Samia ana mengi ya kujifunza kidiplomasia kwa kuwatumia wanadiplomasia wazoefu ambao naamini wapo.