Nchi hii ilianza kuingia kwenye utaratibu wa midahalo tena kwa lugha ya kiswahili hasa wakati wa uchaguzi, na nyakati nyingine huko nyuma. Tulipoaanza kuingiza wagombea wasio na uwezo, hapo tukaona udhaifu ukifichwa wa viongozi hao kwa kusemwa eti wao kazi zao zinaonekana, na hawana muda wa midahalo. Ilifika mahali mpaka Bunge live halitakiwi maana kuna watu hawana uwezo wa kujieleza, hivyo ikawa inaonekana wenye uwezo wa kujieleza watafaidika na hali hiyo!
Sasa kama watu wanakwepa midahalo kwa lugha ya kiswahili wanayoiweza, tena kwa wasimamizi wa hiyo midahalo wanaohofia madaraka yao, inakuwaje wanapokutana na waandishi wanaotumia kiingereza wasichokimudu vyema, na wasio na hofu ya madaraka yao? Matokeo yake ni lazima mtu aongee ukweli,maana ni ngumu kudanganya kwa lugha usiyoimudu vyema, hasa ikizingatiwa huna uwezo wa kumudu midahalo. Katika vitu vilivyomfanya Magufuli aogope kwenda nje, kikubwa ilikuwa ni uwezo wake mdogo wa lugha ya kiingereza, na uwezo wake mdogo wa kujieleza hata kwa hicho kiswahili. Na vile alijua atakutana na watu wasioogopa madaraka yake, aliona bora lawama ya kutokwenda, kuliko fedheha ambayo angeipata kwa kwenda nje.