Kwenye mapenzi hivi vitu viwili havifundishiki

Kwenye mapenzi hivi vitu viwili havifundishiki

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Naona kuna tabia imezuka Sana humu mtu akiumizwa huko akaleta uzi humu watu wanakimbilia kuandika "ACHANA NAYE!!".
Mnafikiri kuacha ni kitu chepesi tu?

Msichokijua KUPENDA na KUACHA hivi ni viti visivyofundishika bali ni maamuzi na utashi wa mtu, itakapofikia mtu kupenda huridhia kwa nafsi na upeo wake wa akili vilevile itakapofikia mtu kuacha ataacha kwa uwezo wake mwenyewe.

Muacheni mtu akinai mwenyewe maana hata kupenda alipenda mwenyewe!. Kumfundisha mtu kuacha au kupenda ni sawa na kumpa majibu ambayo kwake hayaoni.

Upendo ni njia isererekayo ambayo ni wawili tu ndio huamua kuserereka nayo,ukiingia kati mwisho wasiku watakuchota wakutupe kando wenyewe waserereke zaidi!.

Kama unaona Kuna mtu anateswa na mapenzi mpe ushauri yule ambae ni tatizo sio yule ambae hana tatizo!,Kama wote ni tatizo wape wote ushauri ila epuka kuwaambia "ACHANENI" hichi kitu hakifundishiki bali mtu huridhia kumuacha mwenzie na kupendana kwao hukuwafundisha wewe.

Yangu ni hayo.
 
Back
Top Bottom