KENZY jamaa yetu demu wake alikua anamtesa sana mpk jamaa akakonda. kila mda ni kugombana na demu ndio mgovi. kila siku akawa anatuomba ushauri. mwanzo tukamwambia wew kaza. lakin mwsho wa siku tukaona jamaa yetu anateseka sana. anapoteza mda wake, hela zake, anazid kukonda uku demu ananawir, nk. utelezi wenyewe anabaniwa😆. bas bhana siku hiyo tukakaa nae ka masaa matatu tukiongea (usiku hiyo) tukamshauri bhana huyo demu amuache maana tonaona kila siku migogoro. hakuna chochote anachopata. bas jamaa akasema wanangu mim nimewaelewa na huyu demu mim kiukwel namwacha kesho kesho.
Ikafika kesho, kweli jamaa akamwambia demu mimi na wew naomba tuachane. akampa na sababu. (na yule demu alikua na dharau mpk sio poa) basi demu akasema amna shida ka nd umeamua iwe hivyo.
Cha ajabu jamaa mwenyewe nd alimwacha demu, lakini yeye mwenyewe alianza kulia karibu siku nzima. ata msosi hakula.
zimepita siku mbili tunaona kijana wapo pamoja. kumbe jamaa yetu alikuja kuomba tena msamaha. (lilikua zuzu sana) 😕 bas bhana wakarudiana. lakin wakawa wanaishi kama mwanzo tu. jamaa yetu badala ya kufrah ni huzun tu anapata ndani ya hlo penzi.
Anzia pale niliapa sitokuja kushauri chochote kuhusiana na wawili wapendanao. acha akufilie uko au atoke mwenyewe kama akibahatika lakini😅