Kwenye mkataba nimemwandika kama mrithi Ila yeye kamwandika baba yake

Simple. Mwambie kwa lugha nzuri tu na wewe waenda kuhuisha tena taarifa hixo na kumuondoa yeye kama mrithi na kumweka baba yako na watoto.
Muache tu aandike atakavyo, lakini sheria ya mirathi itaamua mgawanyo wa mali. Na iwapo mume amekufa, atapata 1/3 ya malz zake na iliyobaki inaenda kwa watoto , hii ni kama mtatumia sheria ya kiserikali. Yeye akifariki mume atarithi pamoja na watoto. Kama ni muislam safi inaweza kugawanywa kwa kutumia sheria za kiislam, au kama mnafuata mila sana zitagawanywa kutokana na mila husika. Hayo makaratasi ya kazini wala usihangaike nayo sana.
 
Wazazi wa mke huwa wana uchungu sana na watoto wa binti yao kuliko wazazi wa mme kwa watoto wa kijana wao. Ndo maana ni vyema mme amuandike mkewe na watoto.
 
Asilimia kubwa wanawake hawaandiki wanaume kama warithi wao! Nilifanikiwa kufanya hii kazi ya kupeleka taarifa za next of kin pale ofisini kwangu nikaliona hilo! Ila haina shida hata asipokuandika kama mrithi wake pale kunapotokea kifo mume au MKE ndo anapewa kipaumbele kama mna ndoa halali!
 
Ni kweli mkuu vijana wa sasa tunatakiwa tuache tamaduni za wazee wetu ya kuwategemea watoto, tunatakiwa sisi ndiyo tuwape watoto urithi wa Elimu na pesa ili wasije kujiingiza kwenye tamaa, tunavyo wategeme watoto ndiyo tunazidi kuwa fanya washindwe kutimiza marengo yao.
 
Bro nimekabidhi hadi kitambulisho cha nida.... mtu anaekufanya ukunje sura kwa utamu sio wa kumchukulia poa, tatizo tunaangaliaga mabaya tu wakati mazuri ni mengi mno
Nimemuandika mume baada ya kujua zile form hazina impact kihivo, kwanza mtu ukifa huo muda wa kupekua mafile kutafuta form hawana unless unaishi mbali na ndugu zako.
 
Wewe umeonyesha uhalisia wako na maono ya familia yako, na yeye ameonyesha mwelekeo wake. Endelea kuishi.
 
Sasa mkiwa hai tu mume yeye anatapanya rasilimali za familia Kwa kuhonga michepuko na hapo mke yupo hai sembuse mke akiwa hayupo si ndio itakuwa kuzidi tena ?!

Mke ni mtunza na mkusanyaji wa rasilimali za familia lakini mume yeye ni mtapanyaji wa rasilimali za familia.

Akiwahiwa na michepuko tu basi hela za mirathi zote zitaishia kula bata na malaya kama wenye mafao ya kustaafu.

Wastaafu watatajiwa huwa wanaliwa mingo mbaya sana na malaya wa mjini!

Ni mojawapo ya target kubwa sana.

Mwanaume iwapo unakaribia kustaafu niangalie unawindwa!

Halafu zikiisha tu kwaheri [emoji112]

Hakuna wa kukukumbusha muda wa kula was kunywa dawa zako!
 
Pole sana, vya mwanaume ni vya gombania goli, ila vya mwanamke ni vyake mwenyewe...
 
Jamani, Kwenye hii mada naona woooote mmepuyanga kwamba Kazini/Waajiri wanaandika Majina ya Warithi, Hiki kitu Hakipo! Kazini wanaandikishwa NEXT OF KIN kwa maaana ya Mtu wako wa Karibu mwenye Umri wa Miaka 18+ anayeweza kutoa taarifa muhimu kuhusu wewe endapo kuna dharura.
Taarifa hizi hazihusiani na Urithi hata nukta moja bali ni watumishi wanadanganyana kwamba ni Urithi, jibu ni HAPANA.
Masuala ya Urithi ni ya Kisheria na Kifamilia zaidi, Mwajiri hausiki nayo kabisa. So ukiona Mkeo/Mmeo hajakuweka kwenye fomu hiyo ni sawa kwani wewe humjui vzuri kwakuwa wakati mwingine Mkeo anamatatizo ya kiafya ambayo wewe hupaswi kujua au Mkeo ana watoto nje ya ndoa hupaswi kujua, Mkeo anauwekezaji nje ya Ndoa na hataji ujue so Tusilazimishe wake zetu kutuweka kama watoa taarifa wao.
Note: mara nyingi watu hawa wasiwe wale wenye maradhi ya Moyo!
 
Umeambiwa uishi nae kwa akili cha kushangaza yeye ndo anaishi na wewe kwa akili😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…