Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Achana na mambo ya mkaa endelea na shughuli zako, kugongwa na nyoka ni bahati mbaya mkuu na kwake nyoka hapendi kugonga mtu (ni matumizi mabaya ya sumu ambayo anatumia kuwinda)

Mkianza shughuli atahama au atakuwa anapita usiku mchana anapotea. Kelele na mishe za raia zitamdogeza mbali

N.B. Tunakuhakikishia akikugonga na ukafariki MKE WAKO HAOLEWI kama jina lake (jokes)
 
Huyo nyoka ni hatari kama wengine tu ila story zake za wasukuma ndio zinafanya aonekane ameshindikana
Watu wakienda huko unyamwezini na usukumani kutembea, hurudi na story hizi wanazopigiwa na wenyeji wao wa huko. Alaf na wao hukimbilia kuzileta hapa JF bila kuzifanyia uchunguzi wa kutosha.
 

Attachments

  • Screenshot_20240327-121449.jpg
    298.5 KB · Views: 7
Naona unataka kuleta ubishi usiokuwa na maana. Lakini pia haujajua ni kwanini huyu alipewa jina la King Cobra.
Huku Afrika hatuna King cobra ndugu, wapo Asia. Hapa Afrika tuna Mozambican spitting cobra (anatema mate na kusimamisha shingo) na forest cobra (hatemi mate ila anasimamisha shingo), ambao ni wadogo kiumbo kwa king cobra.
 
Nadhani wapo aina tofauti lakini kuhusu magamba huwa tunayaona mara nyingi na hata kuwua

hawa nao wazungumzia mimi ni weusi tii na wakati mwingine hadi hung'aa kwa weusi wakena anatema mate. hawa kwetu wala sio tishio kitu nilikuwa sijui kwamba anaweza kumla black mamba hapo sikuwahi sikia wala kuona. kupitia bandiko hili nimejifunza mengi. Ahsante sana
 
Ni kweli King cobra anamla koboko ila ukiambiwa kati ya cobra na koboko, Nani ufungiwe nae chumba kimoja, chagua cobra
 
Mozambique spitting Cobra common sana hao!
King Cobra hawarushi mate wanapatikana Asia tu,hakuna NYoka Africa anaweza kumuwinda black mamba kirahisi!
Yuko kwenye top of the food chain ya nyoka
 
Shukran mkuu, ila hao unaosema wewe kuwa umeona magamba yao ni cobra wa kawaida ambao wanapatikana sehem mbali mbali nchini.

King Cobra ni habari nyingine aisee. Kwanza mkorofi, mtemi na haogopi.

Tatizo hapatikani Africa... Kule juu nilikuwa nakutania tu lakini najua kiuhalisia hauwezi kumpata 🙏
 
PAMOJA MKUU. Ndo faida ya kuwa jf
 
Na wilaya ya Urambo kama ana fahamiana na mtu amuulizie kuna vichwa hadi hao jamaa wa maliasili wanavitumia kuwadaka hao wapuuzi.
 
Mkuu nawewe umezidi sasa
 
Muue kabla yeye hajakuwahi; ni ama zake au zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…