Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Watu wa kanda ya ziwa sijui huwa wana shid gani. Yani black mamba amepewa story za kutungwa za kichawi kiasi kwamba anaogopeka sana.

Ni nyoka hatari ndio lakini sio kwa hizo mbwembwe anazopewa. Simon Keys anacheza nao kila siku.
Nadhani hii ni kwa mjibu wa mawazo yako. kanda ya ziwa ungesemea uchawi na ukamhusisha fisi;Bundi;mamba kwa wakala ukerewe ungeeleweka.

koboko hausishwi na uchawi kama unavyodai wewe. na kwa sababu wewe unamchukulia poa kuliko watu wa kanda ya ziwa naomba uje umuuwe basi nauli juu yangu na zawadi ya mabeberu3 ya mbuzi.
 
Anaitwa koboko, usisikie maneno ya watu usijitusu usiingie kichwa kichwa uyo mdudu ni noma uyo mdudu acheki na kima unapo ingilia maslai yake aliangushaa mbuzi wa mzee 6 kwa mpigo. Mungu mkubwa tulipona.
sisi ng'ombe saba na watoto2 kwa muda mfupi tu
 
Kwakesi yoyote ile kubwa nandogo mcheki huyo mchawi mkielewa vizuri anakuja kuwakata namkono kisha mtawauwa wenyewe nakuwazika.
Screenshot_20240327-192608.jpg
 
Jf salaam🙏

Ni muda sasa tangu aanze kuonekana huyu nyoka hatari koboko na inasemekana wapo wawili.

Taarifa zilianza kunifikia kutoka Kwa wazee wangu maana huo msitu ukweli sio wangu ni wa mzee ila kaniruhusu kufanya shughuli zozote za kujiingizia kipato.

Mara kadhaa amekuwa akionekana na muda wa usiku kupiga kelele flani Hivi.

Nakumbuka baada ya kupata mapumziko mafupi nilienda kijijni kwa wazee wetu. Nikafika na nikaenda mlimani(msituni) lengo nikufanya research kwa kina Ili niwekeze ufugaji wa nyuki (asali).

Nilimchukua dogo mmoja ambae Huwa anachunga mbuzi wangu tukaenda naye huku akinifotoa picha za kila aina na Kila Rangi.

Mwisho tukafika kwenye mti mzuri wenye kijani kibichi wenye matawi mazuri akanipigia picha za kutosha pale.

Baada ya hapo tukakaa chini ya mti huo kwenye jiwe huku nikipitia picha nilizopigwa na kufuta zile sikuzipenda

Tukiwa hapo tunapiga story ghafla tukasikia kelele za ndenge flani juu ya mti Mimi kelele zile nazijua huwa ni Alert ya hatari fulani wameiona wale ndege.

Kuinua macho juu sikuamini nilichokiona ni yeye koboko mtesa ametulia tulii Wala hatikisikii kama amekufa.

Dogo(muha) kumuona akapanic akaanza mbio nikamwambia simama hapohapo akasimama huku nami nikitoka eneo la tukio hadi kwa dogo.


Nyoka ni mkubwa na anaogopesha na kwa mazingira yale huwezi mshambulia kwa kutumia njia zetu hizi za asili(fimbo)

Maana ni mstuni vinginevyo anakuua ndani ya muda mfupi tu hakuna sehemu ya ku escape asikudhuru.

KUMBUKUMBU ZANGU

Miaka ya nyuma tukiwa wadogo nilishuhudia maiti za Watoto wenzetu watu na ng'ombe 7 zikiwa zimelala Chali (kufa).

Ni baada ya Hawa Watoto kuona huyo nyoka aina ya koboko na kumshambulia ndipo alipowageuka na kuwauma wote wawili na ng'ombe zao zote Saba na zilikufa hapohapo!

Nakumbuka kipindi hicho hicho nikiwa primary mtoto mwingine darasa letu Moja akiwa anaenda kuokota maembe kwenye mti wa mwembe akamuona koboko Kasimama wima naye pasina kujua alianza kumshambulia.

Hapo hapo alimgonga na kufa mama yake alisikia kelele za mwanae akilia Kwa uchungu Kwa sababu ilikuwa mbali na mwembe na mara zote walikuwa wanaenda Watoto kadhaa kuokota maembe pale. ile anatoka akamsaidie alimkuta tiyari kashafariki na nyoka amepanda juu ya mtu flani mfupi.

Ndipo alipo piga yowe kuomba msaada na walifanikiwa kumuua.

Inavyosemekana na Mimi naweza kuwa shahidi wa hili ni kwamba....

Nyoka aina ya black mamba ni wapole kupita kiasi pale anapokuwa katika Hali yake ya kawaida.

Pia anasikia kuliko kawaida anaupeo mkubwa wa kuhisi hatari na hata harufu na hivyo kujiweka tiyari Kwa ajiri ya mapambano.

Akiona mazingira aliyopo sio salama kwakwe kufanya shambulio hujiondokea kabla hujamfikia Wala kumuona.

Lakini pale ukimuona wewe jua kakusubiri na amejiandaa Kwa muda mrefu sana amegojea tu ulianzishe upate unachostahili.

Kwa matukio hayo mawili ambayo siyo ya kusimuliwa na hili langu Mimi mwenyew Tena mwezi 2 tu mwka huu nakubaliana na hili kuwa Hawa nyoka ni wapole na ni hatari.

Tukio la wale watoto wawili na ng'ombe wao. Sisi ndo tulikuwa wa kwanza kumuona yule nyoka na ilikuwa Hivi.....

Siku Moja tunaenda machungani katikati ya njia kulikuwa na mti flan Hivi kama kichaka (ipo miti Ina randa na kutengeneza kichaka kizito)

Tulipitisha mifugo yetu yote salama na sisi wenyewe tukapita salama mtu wa4 ndo akatumbia oneni yule nyoka tukarudi kumtazama asee alikuwa mrefu sana na ametulia kama hajui kinachoendelea...

Tulichokifanya ni kwenda kuwambia wakubwa wetu karibu na eneo lenyewe. Na walipokuja wakamuona na kumtambua walitumbia ondoeni ng'ombe na mifugo yenu hapa tukafanya hivo.

Nao walipoona tumeondoka waliondoka pia bila kumfanya chochote.

Bahati mbaya sana Kwa wenzetu siku chache mbele wao walipo muona tu ujasiri uliwaingia na kuanza kumshambulia huo ndo ulikuwa mwisho wao na ng'ombe wao pia.

Yowe lilipigwa nyoka huyo akauliwa.

Nimekuja kuomba ama kufundishwa njia/mtego Ili nimuue bila kuathiri watu wa maeneo hayo.

Msitu huu nimepanga kufugia nyuki Kwa wingi lakni kinacho niogopesha ni uwepo wa black mamba kwenye eneo hili.

Eneo ni zuri sana Kwa nyuki kwani maji yapo si zaidi ya mita250 na nyuki ni wengi sana hasa kwenye mapango ya miti,mawe na wengine hujitengenezea asali juu ya mti tu.

Najua humu Kuna watu wa maliasili na wataalamu wa maswala haya naombeni namna ya kumuondoa huyu mdudu na nimeambiwa wapo wawili.

Wapo walio waona Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti na usiku hupiga kelele zao Kwa kupokezana wasi wasi wangu zaidi watazaliana na kuongezeka zaidi.

Ahsanteen sana.

View attachment 2945391
Tafuta nguchiro walioshiba na uwafuge kwenye huo msitu🤣
 
ndo natafuta mbinu sasa ya kummaliza
Andaa Upinde na Mshale halafu jikunje hadi kibyongo kikutoke halafu kabla ya kuufyatua mshale fanya maombi yote kumbuka kuacha Wosia kuwa "ukifa Mkeo asiolewe" jifute jasho halafu uachie mshale uende halafu njoo humu JF tupe mrejesho tukiona kimya tutajua mshindi ni nani.
 
Kwakesi yoyote ile kubwa nandogo mcheki huyo mchawi mkielewa vizuri anakuja kuwakamata namkono kisha mtawauwa wenyewe nakuwazika.
Screenshot_20240327-192608.jpg
 
Andaa Upinde na Mshale halafu jikunje hadi kibyongo kikutoke halafu kabla ya kuufyatua mshale fanya maombi yote kumbuka kuacha Wosia kuwa "ukifa Mkeo asiolewe" jifute jasho halafu uachie mshale uende halafu njoo humu JF tupe mrejesho tukiona kimya tutajua mshindi ni nani.
😂 😂 😂 Wosia tyr ushaandikwa kuhusu mke wangu mkuu atakayekaidi atanifata
 
Ukimua wewe mwenyewe huyo nyoka utafungwa kwa kosa la kuhujumu uchumi.Huyo ni nyoka adimu sana,so anaingiza fedha za kigeni nyingi sana ktk utalii.Mali asili watamchukua, huyo ni nyoka wa serikali.
maliasili tangu nitoe bandiko humu hajajitokeza hata mmoja na atajua vipi kuwa kauawa? halafu wasiingilie shughuli za watu tukiwaita kama hivi hawaonekani ikitokea la kutokea kama ulivyosema akauawa na wakajua utawaona haoo na sare zao
 
Kwakesi yoyote ile kubwa nandogo mcheki huyo mchawi mkielewa vizuri anakuja kuwakamata namkono kisha mtawauwa wenyewe nakuwazika.View attachment 2946171
Ingia hapo utapeliwe halafu ufe.Itakuwa hivi.,Atakwambia mlipe kwanza hela kwa ajili ya mizimu, ukishamlipa atafanya kama amemfanyia dawa,halafu atakwambia kamkamate huyo nyoka kwa mikono sehemu ya mkia ukiwa umefumba macho kwamba tayari ameshavurugwa na mizimu.Halafu watu watakuja kukuokota ukiwa unatoka mapovu.
 
Chomeni mipira ya tairi za magari chomeni mfululizo siku 7 hawatakaa tena huo msitu watahama kabisa..
Tena mkidondosha na oil chafu ndio kabisa

Tahadhari ukiwasha moto wa tairi muondoke kabisa eneo hilo maana mmeanzisha vita vya 3 vya dunia na hao nyoka..
Atasema huyu kenge gani kajipa mamlaka ya kuharibu hali ya hewa😀😃jamaa angetafuta mishe nyingine,hofu isije akachukua nguvu kazi za watu akawatanguliza kwenye balaa tu😄😄😅
 
Back
Top Bottom