Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Watu wa kanda ya ziwa sijui huwa wana shid gani. Yani black mamba amepewa story za kutungwa za kichawi kiasi kwamba anaogopeka sana.

Ni nyoka hatari ndio lakini sio kwa hizo mbwembwe anazopewa. Simon Keys anacheza nao kila siku.
Nadhani hii ni kwa mjibu wa mawazo yako. kanda ya ziwa ungesemea uchawi na ukamhusisha fisi;Bundi;mamba kwa wakala ukerewe ungeeleweka.

koboko hausishwi na uchawi kama unavyodai wewe. na kwa sababu wewe unamchukulia poa kuliko watu wa kanda ya ziwa naomba uje umuuwe basi nauli juu yangu na zawadi ya mabeberu3 ya mbuzi.
 
Anaitwa koboko, usisikie maneno ya watu usijitusu usiingie kichwa kichwa uyo mdudu ni noma uyo mdudu acheki na kima unapo ingilia maslai yake aliangushaa mbuzi wa mzee 6 kwa mpigo. Mungu mkubwa tulipona.
sisi ng'ombe saba na watoto2 kwa muda mfupi tu
 
Tafuta nguchiro walioshiba na uwafuge kwenye huo msitu🀣
 
ndo natafuta mbinu sasa ya kummaliza
Andaa Upinde na Mshale halafu jikunje hadi kibyongo kikutoke halafu kabla ya kuufyatua mshale fanya maombi yote kumbuka kuacha Wosia kuwa "ukifa Mkeo asiolewe" jifute jasho halafu uachie mshale uende halafu njoo humu JF tupe mrejesho tukiona kimya tutajua mshindi ni nani.
 
Kwakesi yoyote ile kubwa nandogo mcheki huyo mchawi mkielewa vizuri anakuja kuwakamata namkono kisha mtawauwa wenyewe nakuwazika.
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Wosia tyr ushaandikwa kuhusu mke wangu mkuu atakayekaidi atanifata
 
Ukimua wewe mwenyewe huyo nyoka utafungwa kwa kosa la kuhujumu uchumi.Huyo ni nyoka adimu sana,so anaingiza fedha za kigeni nyingi sana ktk utalii.Mali asili watamchukua, huyo ni nyoka wa serikali.
maliasili tangu nitoe bandiko humu hajajitokeza hata mmoja na atajua vipi kuwa kauawa? halafu wasiingilie shughuli za watu tukiwaita kama hivi hawaonekani ikitokea la kutokea kama ulivyosema akauawa na wakajua utawaona haoo na sare zao
 
Kwakesi yoyote ile kubwa nandogo mcheki huyo mchawi mkielewa vizuri anakuja kuwakamata namkono kisha mtawauwa wenyewe nakuwazika.View attachment 2946171
Ingia hapo utapeliwe halafu ufe.Itakuwa hivi.,Atakwambia mlipe kwanza hela kwa ajili ya mizimu, ukishamlipa atafanya kama amemfanyia dawa,halafu atakwambia kamkamate huyo nyoka kwa mikono sehemu ya mkia ukiwa umefumba macho kwamba tayari ameshavurugwa na mizimu.Halafu watu watakuja kukuokota ukiwa unatoka mapovu.
 
Atasema huyu kenge gani kajipa mamlaka ya kuharibu hali ya hewaπŸ˜€πŸ˜ƒjamaa angetafuta mishe nyingine,hofu isije akachukua nguvu kazi za watu akawatanguliza kwenye balaa tuπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…