Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

watamalizwa na wakulima huwa wanakula karanga wale
Hapana nguchiro (mangoose) Hali karanga ni carnivore!
Ziko species ambazo ni omnivores zinachanganya Milo kama banded mangoose lakini hazili karanga nzima nzima kama rodents hao labda uwape peanut butter
Ila slender mangoose ni pure meat feeder anawinda NYoka,mijusi,panzi,kuku nk
 
Ndio mkuu wanapenda jua sana nahisi hivyo maana wanapenda juu kabisa
Wanaopenda juu ya miti ni green mamba ambao huwinda ndege sana black mamba hupendelea zaidi chini!

Na akiteleza huteleza haswa anapenda sana wanyama wadogo wadogo mfano wa panya na mijusi aina zote
Ukimkuta mtini ujue amekusa mlo chini kaamua kutafuta viota vya ndege!!
 
Mkuu wewe unaelewa sana na wajuu kuhusu Hawa viumbe
 
Nimesoma Wikipedia hapa ni vile vile ulivyosema wewe. Miaka ya nyuma walikuwa wengi sana lakn Cha ajabu walikuwa wanashambiliwa sana na wanakijiji na walikuwa wanishi kwenye mashimo ya vichuguu basi wakikurupushwa kutoka mashambani mwenye shamba atawazimba Kwa kutumia miba nao hufa Kwa njaa Kwa sababu hawezi kutoka akitaka kutoka anachomwa na miba Hadi kufa.

Nimejaribu kuangalia kumbe hata vicheche ni jamii Moja na nguchiro mkuu nilkuwa sijui na nilijua kuwa kicheche yeye anakula nyama na wadudu tu. Ahsantee sana

Hawa ndo kwetu walikuwapo Kwa wingi sasahivi wameshatoweka kabisa
 

Attachments

  • Screenshot_20240327-204106.jpg
    359.9 KB · Views: 5
Sahihi!
Wanakijiji waliwaua kwa sababu wanashambulia kuku na vifaranga!
Na hata kwenye hivyo vichuguu ambavyo huishi humo ni vichuguu vilivyokufa either kwa kuvamiwa na siafu au wanyama wanaokula mchwa kama vile muhanga na nunguri!
Hawana uwezo wa kuchimba kama mole rats ndio maana walivyowekewa miba wakashindwa ku plan B kutoka nje
 
Uhakika
 
Mi ushauri ninaokupa ondoa hofu NYoka wako Kila mahali na bila uwepo wao ikolojia itakufa NYoka hawana shida na binadamu ila binadamu ndio muharibifu
Hapo kwenye pori lako endeleza mradi wako,NYoka wanakuona na kukuhisi kabla haujatokeza ukianza pilikapilika hapo watasepa kutafuta sehemu tulivu!
Hapa ninapokaa Kuna brown house snakes zaidi ya ishirini na huwa ikifika jioni nawaona wakitoka chini ya mawe kuwinda Mende,panya nk na Mimi na wao hatuna ugomvi isipokua niwakute ndani kwangu ndio nitaua
 
Sawa mkuu naishi na ushauri wako
 
Kwani mkuu ukimuona let's say kwenye mti na ukazungushia petroli ukawasha eneo Hilo, huwezi mpata tena. Au unaweza chukua chumvi ukamwaga maeneo yake, maana chumvi huwa inamkata kata, au unaweza nunua oil chafu ukamwaga maeneo alipo, maana hawezi kuslide lazima tu akiona hyo Hali hakai ataondoka tu. Wapo wanaochukua uji wa Moto na sufuria juu then wanaenda alipo hasa kwa watu wa musoma na kisha wanaenda eneo na kuanza kumchokoza,akitoka juu ya mti huwa ni moja kwa moja kwenye sufuria la uji,hapo lazima afe
 
ushauri wako ni mgumu kuutekeleza mkuu. Daaah ni mgumu asee
 
Ushauri wa uji wa moto kubeba kichwani ni story kama za sungura na fisi! Koboko anagonga popote na vimeno vyake vidogo vya mbele(front fixed fang) anaweza rukia p*mbu,kidole,sikio,tumbo nk

Striking yake ni ya kudonoa kama kuku tofauti na boomslang au vine snakes(back fanged) ambao hung'ata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…