Kwenye phonebook yako kuna marehemu wangapi?

Kwenye phonebook yako kuna marehemu wangapi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Kuna watu ni wavivu kufutaga contact za marehemu mpaka sasa wako nazo wengine tunasave majina kwenye Gmail ukiingiza kwenye simu mpya yana jirestore.Mimi nina marehemu Watano majina yao nimeamua tu niyaache. Imma, yuni, mamkubwa, elia na fundi Tandika.
 
Mungu aendelee kuwarehemu marehemu na mahayati wote nilionao kwenye phonebook yangu

Kimsingi mimi sifuti number zao deliberately, naona kama kufuta number zao ni kujitenga nao mazima. Kwangu kukaa na number zao ni kuwaheshimisha
 
Siku hizi namba ikikaa muda fulani haijatumika inauzwa kwa mwingine. Ukikaa unashangaa unapata notifications marehemu amejiunga telegram
 
Mungu aendelee kuwarehemu marehemu na mahayati wote nilionao kwenye phonebook yangu

Kimsingi mimi sifuti number zao deliberately, naona kama kufuta number zao ni kujitenga nao mazima. Kwangu kukaa na number zao ni kuwaheshimisha
kuna ule ujumbe mtu anaandika "hakuna jambo gumu kama kufuta namba ya mzazi wako aliyefariki"sasa huwa najiuliza,kama unafuta namba yake si ufute na picha zake!!!
 
Hakika hilo nalijua ila kuna sababu gani mtu kupewa namba ya mtumba(namba iliyotumika)?

Kampuni za simu ziliangalie hili
Fikiria watu wanaofariki ni wangap halafu hizo namba ziachwe tu?
Hujafikkria kwann wanazirudisha? Uhisi gharama za kutengeneza hizo namba ?
Watu wnakufa kibao halafu hizo namba ziwe zinaachwa tu zisifanye kazi tena?
 
Back
Top Bottom