Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Huu ndio hasa ushauri wangu kwa kaka yangu mkuu wa mkoa wa Arusha. Inaonesha wazi nyota yake ya mafanikio ni kali sana na inaandamwa na kila mwenye nia njema na nia mbaya.
Kwa wasomaji wa biblia wataungana nami kwa kurejea matukio mbalimbali ya kuandamwa kwa watu wenye nyota za mafanikio. Wengine walitakiwa kuuawa ili kuzima mafanikio yao. Mfano Yusufu, Daudi nk. Hawa ni mfano tu wa waliobeba maono.
Hivyo basi ikiwa kuna mtu yeyote anadhani kwamba amebeba maono, na pengine nyota yake imekuwa iking'aa na kuandamwa; basi mtu huyo anapaswa kulinda sana hisia zake na kujiepusha na mihemko. Kwani adui zake huweza kutumia udhaifu huo wa kushindwa kuhimili mihemkonna hatmaye kumtengenezea zengwe.
Huo ni ushauri wangu kwa wote wenye nyota za mafanikio. Najua wakati mwingine si rahisi sana kudhibiti hisia, muhimu ni kujitahidi kwa kila hali kwani kufikia kilele cha mafanikio ni kama kuwa vitani.