Kwenye Shamba la Wanyama kinachohitajika Sio Kumfukuza Binadamu, bali kuondoa Mentality kwamba baadhi ni Bora kuliko Wengine

Kwenye Shamba la Wanyama kinachohitajika Sio Kumfukuza Binadamu, bali kuondoa Mentality kwamba baadhi ni Bora kuliko Wengine

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,416
Bila kufanya hivyo tutakuwa tunabadilisha wanyonyaji na sisi wabadilishaji kuendelea kunyonywa..., hivyo basi kuliko kusubiri siku tukishawabadilisha labda tutaacha kunyonywa, tuanze kuwasihi wa leo wasitunyonye na wao waache kunyonya (wajifunze kula na vipofu).

Kinachoendelea sasa katika mnyororo wa kunyonya kila mtu anaridhika so long as anapata hata kidogo hivyo kushindwa kumkemea wa juu yake akiogopa akifanya hivyo atakuwa kama wa chini yake. Ingawa hawa wanyonyaji wasichojua ni kwamba kundi la wasiopata mgao huu linazidi kuongezeka hivyo kuleta hatari kwa wote hapo kesho.... Wanachuma Janga ambalo litakuja kuliwa na hata SISI ambao sio Wahusika

1756023034521.png
 
Back
Top Bottom