GE2025 Kwenye siasa hakuna uadui au urafiki wa kudumu. Lakini kwa Luhaga Mpina hapana.Hajatumwa na CCm

GE2025 Kwenye siasa hakuna uadui au urafiki wa kudumu. Lakini kwa Luhaga Mpina hapana.Hajatumwa na CCm

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa CCM kwa zaidi ya miaka 20, Luhaga Mpina sasa kaondoka kwenye Chama hicho na kujinga na ACT Wazalendo, huko amefika tu na kupewa nafasi ya kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu ujao

Kwa kipindi chote akiwa CCM, Mpina alikuwa mpinzani wa ubadhirifu wa mali ya umma, wizi, rushwa, kifupi alijali sana maslahi ya Taifa na hakika alionyesha moyo wa ushujaa, ujasiri na uzalendo kwa Taifa na watu wake.

Mara nyingi Mpina aliingia kwenye ugomvi na wakubwa na pia Wabunge wengine ndani ya CCM kutokana na kuwa kinyume nao kwenye suala zima linalohusu maslahi ya Taifa.

Kusimama.peke yako na kukosoa Serikali wazi wazi tena ukiwa Mbunge ndani ya chama tawala ni jambo linalohitaji ujasiri na uzalendo usiopimika.

Ikumbukwe pia kwamba, hivi karibuni Mpina aliingia kwenye mzozo na Rais Samia alipofanya ziara Mkoa wa Simiyu. Katika ziara hiyo, Rais Samia alimkataa Mpina hadharani. Kweli jina lake lilikatwa na ndipo akaamua kwenda ACT Wazalendo.

Kutokana na misimamo yake kwa muda wote huo na kwa kauli za wakubwa ndani ya CCM dhidi yake nakosa nguvu na Imani kwamba, Luhaga Mpina kaenda ACT kama danganya toto. Ili CCM ipate ka mseleleko kwenye Uchaguzi huo Mkuu. Kwamba ni mpango wa CCM kuhadaa umma na Dunia kuwa Uchaguzi ni fair and Democratic.

Haiwezekani watu ambao wamekuwa wakiparuana na kuzodoana.kwa.miaka yote hiyo, Leo ndani ya muda mfupi wakae meza moja na kupeana kazi za aina hii yaani kuwatapeli watanzania.

Mi naona tuache kumhukumu na kutoa conclusion ya moja kwa moja kuwa Mpina ni pandikizi la akina Jakaya na CCM yake.

Kwa vile, CHADEMA imejikuta hapo ilipo, basi tuunganishe nguvu kwa pamoja na tumuunge mkono Luhaga Mpina na ACT.

Wale wengine wanaoruka na chopa kwenye Uchaguzi Mkuu na agenda zao za ubwabwa hao tunajua wazi kuwa wanamtumikia fulani.

Pamoja na kwamba Kwenye siasa hakuna urafiki au uadui wa kudumu , lakini kwa Mpina hapana, huyu hajatumwa..
Ukiwa mjinga utamuamini mpina kuwa ni mpinzani wa serikali lakini ukiwa na akili utajua mpina naye ni project kama zilivyo kuwa project za hapo awali
 
Kanda ya Ziwa na Mpina tu

Ukiwa mjinga utamuamini mpina kuwa ni mpinzani wa serikali lakini ukiwa na akili utajua mpina naye ni project kama zilivyo kuwa project za hapo awali
Mpaka aje Malaika kutoka Mbinguni ndio tutamwamini. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK, Magufuli, Samia, Lissu, Gwajima, Polepole. Wote hao wanakosolewa na kutukanwa na wengine wanaomba hata wafe.

Sasa kwa Luhaga Mpina kuna ajabu gani? Ndivyo wabongo tulivyo. Ujuaji mwingi na ujinga ujinga mwingi hata usio na maana.

Tuendelee kufunga na kuomba ili Mungu ashushe Malaika kutoka Mbinguni aje agombee Urais. Lakini kwa umbulukaka wa aina hii lazima naye atakataliwa tu ataambiwa wewe ni pandikizi, ni project ya Shetani.
 
Back
Top Bottom