Kwenye siasa, ukisaliti lazima utasalitiwa

CDM imeshakuwa taasisi miaka mingi sana ndio maana pamoja na viongozi wake;
kufunguliwa kesi za kughushi bado chama kipo imara!
 
Vyama vya upinzani vinafanyiwa fitna viwe dhaifu na mwishowe visambaratike. CCM hawataki upinzani, hata Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka CCM.

..waanzilishi wa vyama karibu vyote vya upinzani waliwahi kuwa wanachama wa Ccm.

..Kwa maana hiyo utabiri wa Mwalimu Nyerere ulishatimia. Kilichobaki ni kuviimarisha vyama vya upinzani.
 
Dah!

baada ya kusoma kichwa cha mada, nikakuelewa vingine, tofauti na niliposoma yaliyomo kwenye mada.
"Kwenye Siasa Ukisaliti Lazima Utasalitiwa"..., moja kwa moja ilinipeleka kwenye yanayotokea sasa hivi ndani ya CCM.

Au huko, mkuu'Quinine' unaona kuko vizuri kabisa wakati huu?

Au labda tuseme, bahati yao ni kuwa wao wanayo na wanamiriki asali ya kulambishana ndiyo sababu hatuoni tunayoyaona huko kwingine?
 
..waanzilishi wa vyama karibu vyote vya upinzani waliwahi kuwa wanachama wa Ccm.

..Kwa maana hiyo utabiri wa Mwalimu Nyerere ulishatimia. Kilichobaki ni kuviimarisha vyama vya upinzani.
Kinachokosekana ni kutomiliki chungu cha asali tu basi? Hiyo ndiyo tofauti pekee iliyopo kati ya CCM na vyama vya upinzani.

Leo hii CCM wakipokonywa hicho chungu, huataona tofauti kubwa kati yao na hao wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…