Kwenye suala la Tozo, Rais Samia ataibukia hapa kuonesha ni msikivu

Kwenye suala la Tozo, Rais Samia ataibukia hapa kuonesha ni msikivu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Mbinu ni zile zile hakuna jipya katika Serikali zetu za Kiafrika. Kutengeneza tatizo halafu unalitatua.

Tumeona jinsi ambavyo sasa wana CCM wameambiwa wajifanye kumwomba Rais Samia aangalie suala la tozo mpya ya miamala ili baadaye Rais aseme amesikia kilio cha wananchi na kuondoa.

Inabidi watumike CCM na si wapinzani ili isije onekana amewaogopa wapinzani. Tutasikia Jumuiya, Wabunge na viongozi kadhaa wa chama wakisema wameongea na Rais naye atatoa tamko.

MAMA ANAUPIGA MWINGI INGAWA NI NJE YA UWANJA.
 
Itakuwa kwa kujifaragua maana Alisha assent
Screenshot_20210719-082429_1.jpg
 
Mlango wa kutokea una andaliwa muwe wapole.......
IMG-20210719-WA0037.jpg
 
Kuna tamko linaandaliwa la Mh Rais kuzungumzia Tozo
 
Mbinu ni zile zile hakuna jipya katika Serikali zetu za Kiafrika. Kutengeneza tatizo halafu unalitatua.

Tumeona jinsi ambavyo sasa wana CCM wameambiwa wajifanye kumwomba Rais Samia aangalie suala la tozo mpya ya miamala ili baadaye Rais aseme amesikia kilio cha wananchi na kuondoa.

Inabidi watumike CCM na si wapinzani ili isije onekana amewaogopa wapinzani. Tutasikia jumuiya, wabunge na viongozi kadhaa wa chama wakisema wameongea na Rais naye atatoa tamko.

MAMA ANAUPIGA MWINGI INGAWA NI NJE YA UWANJA.
Old Stone Age tricks.
 
Hii Wizara haimtoshi kabisa Mwigulu! Na huu ndiyo ukweli mchungu.
 
Kipimo cha Samia sio kimoja, bado kuna demokrasia (kuruhusu mikutano ya siasa) kwa vyama pinzani, kumaliza la tozo ni sehemu ndogo tu ya tatizo lililopo.
 
Hii mbinu huwa wakati flani Marais wanaitumia kuongeza popularity. Wana create a problem then wana provide a solution
[emoji1787]...... Yaani hawa wanasiasa wametuona mazuzu sana sisi... Hadi sasa ndivyo ilivyo.....
 
Hii Wizara haimtoshi kabisa Mwigulu! Na huu ndiyo ukweli mchungu.
Huyu PhD Kapwaya Sana Ndiyo Maana Alipokuwa Boss Wa Ma~Police Alitimuliwa Kazi. Hawa Wana Vyeti Vya Kuonyesha Ila Utendaji Ni Kama Galasa La ♧ Tu😃😂😁😀
 
Serikali ya kukosa msimamo sio serikali ni utopolo
1. Serikali imekurupuka na kupitisha tozo lenye ongezeko kubwa sana bila utafiti wa kutosha.Hili ni kosa.Lisirudiwe.

2. Watu wamepinga sana ongezeko katika tozo, hususan kwa minajili ya kupinga kiasi cha ongezeko, si kupinga tozo lenyewe.Ingawa kuna wachache wamepinga kulipishwa tozo/kodi mara mbili.

3. Rais na serikali wakibadilisha maamuizi, ama kwenye kiwango cha tozo ama kwenye kuondoa tozo, nitawaona kama watu ambao walikosea hapo mwanzo, halafu wakajisahihisha kulingana na mrejesho wa wananchi. Hiki si kitu cha kubeza, ni kitu cha kupongeza.Watu wenye maarifa hubadilisha mawazo kulingana na taarifa mpya, wajinga tu ndio hawabadilishi mawazo hata wanapopata habari mpya zinazoonesha wanastahili kubadilisha mawazo
 
Hakuna cha tozo kubwa hiyo ni tozo ya kawaida tena inafidia Ukwepaji kodi kunakofanywa na wananchi kutodai na kutoa risiti.. yaani kwenye 130,000 kwa mfano unakatwa 6180 ndio pesa nyingi hiyo?

Hapo kuna faida ya kampuni 3650 na tozo ya serikali 2530 sasa tozo kubwa iko wapi? VAT inalipwa na kampuni
 
Hili ni suala relative, kama una kipato kikubwa na hela yako rahisi kutoka huwezi kuona hili kama jambo kubwa.

Jambo la muhimu ni kujua "the point of diminishing returns" kwa nfumo mzima.

Si kila mtu ana kipato kama chako.

Kwa kuangalia miamala ilivyodorora siku chache zikizopita, inaonekana watu wengi hawakubaliani nawe.

Kitu kingine, kuna msemo "Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno".

Hizi kodi na tozo zinatumika kwa ufanisi kivipi?

Kuna nchi nyingi kama kwa mfano za Scandinavia zinatoa kodi kubwa, lakini wananchi wanaona kodi zinafanya kazi gani, shule bure mpaka chuo kikuu, matibabu bure, huduma bora mpqka magerezani etc. Hapo hata mwananchi haoni tqmabu kulipa kodi kubwa.

Sasa huku kwetu kila kukicha unasikia scandal watu wameiba hela, hapa EPA, hapa Deep Green, you name it. Sasa hapo unategemea wananchi wawe na imani na mfumo?

Rais kapendekeza lijengwe daraja jipya Selander, mawqziri wamemwambia daraja halina tija hapo, lingewekwa sehemu nyingine, rais kasema hapa daraja litapendeza, watu watapiga picha. Akala,imisha daraja lijengwe ili watu wapige picha. Kwa gharama sana. Halafu watu wakamuliwe mpaka mavi kulipia gharama.

Hapo watu wakiona tozo hizi ni ujinga utawakatalia?
 
Back
Top Bottom