Hili ni suala relative, kama una kipato kikubwa na hela yako rahisi kutoka huwezi kuona hili kama jambo kubwa.
Jambo la muhimu ni kujua "the point of diminishing returns" kwa nfumo mzima.
Si kila mtu ana kipato kama chako.
Kwa kuangalia miamala ilivyodorora siku chache zikizopita, inaonekana watu wengi hawakubaliani nawe.
Kitu kingine, kuna msemo "Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno".
Hizi kodi na tozo zinatumika kwa ufanisi kivipi?
Kuna nchi nyingi kama kwa mfano za Scandinavia zinatoa kodi kubwa, lakini wananchi wanaona kodi zinafanya kazi gani, shule bure mpaka chuo kikuu, matibabu bure, huduma bora mpqka magerezani etc. Hapo hata mwananchi haoni tqmabu kulipa kodi kubwa.
Sasa huku kwetu kila kukicha unasikia scandal watu wameiba hela, hapa EPA, hapa Deep Green, you name it. Sasa hapo unategemea wananchi wawe na imani na mfumo?
Rais kapendekeza lijengwe daraja jipya Selander, mawqziri wamemwambia daraja halina tija hapo, lingewekwa sehemu nyingine, rais kasema hapa daraja litapendeza, watu watapiga picha. Akala,imisha daraja lijengwe ili watu wapige picha. Kwa gharama sana. Halafu watu wakamuliwe mpaka mavi kulipia gharama.
Hapo watu wakiona tozo hizi ni ujinga utawakatalia?