Kwenye utatuzi wa kero na changamoto za wananchi serikali itumie hili wazo linaweza kuwasaidia

Kwenye utatuzi wa kero na changamoto za wananchi serikali itumie hili wazo linaweza kuwasaidia

ndo vile

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2023
Posts
443
Reaction score
296
Serikali inaweza kutumia wazo hili katika kuwafikia wananchi kirahisi na kutatua kero na changamoto zinazowakabili Watanzania

MAMA ANAKUITA" call Center PROJECT PROPOSAL (Njoo Tuseme kwa mama, Piga no …… utete na Bi. Mkubwa)​

“Mama anakuita call Center” ni namba mahususi ya simu itakayotumiwa na wananchi kueleza kero zao na kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa kero hizo.

Namba hiyo itakuwa ni bure,kwa maana ya kutokuwa na gharama yoyote pindi mwananchi atakapopiga namba hiyo.

Call center hii itakuwa inahudumia wananchi kwa kanda ili iweze kuwa na ufanisi na ilete uhalisia zaidi kwa sababu ya shughuli za kijamii na kiuchumi katika kanda huwa zinafanana!!i.e mwananchi wa kanda ya kati anaweza asiwe na kero ya zana za uvuvi kama ilivyo kwa mwananchi wa kanda ya ziwa.

Namba hii ni kwaajili ya kuwasilisha kero ambazo zimeshindikana kutatuliwa katika ngazi ambazo wananchi wanaishi.

Pindi mwananchi atakapopiga simu kwa ajili ya kuwasilisha kero yake,simu yake itapokelewa na vijana mahiri wenye ujuzi na taarifa za kutosha kuhusiana na utatuzi wa kero yake.

Endapo kero ya mwananchi itakuwa nje ya uwezo wa vijana hawa,mwananchi ataunganishwa na ngazi za juu zaidi zenye uwezo wa kutatua kero yake.

Ili mwananchi aweze kutatuliwa kero yake kiurahisi kutakuwa na maelekezo rahisi ambayo mwananchi atapaswa kuyafuata i.e kuongea na muhudumu wetu kwa kero zinazohusisha maswala ya ardhi bonyeza 1,au kuongea na muhudumu wetu kwa kero inayohusu upatikanaji wa pembejeo bonyeza 6,au kuongea na muhudumu wetu kwa maswala mengineyo bonyeza 9.

Kwenye kila kero kutakuwa na jopo la wataalamu waliotayari kusikiliza,kushauri na kuwaunganisha wananchi kwenye sehemu husika kwa ajili ya utatuzi wa kero.

Wapokea simu watakuwa na mawasiliano ya taasisi zote za kiserikali kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa kero mbalimbali za wananchi.

Mwananchi mwenye kero atapaswa kutoa taarifa zake kama majina na sehemu anayotoka ili kurahisisha ufuatiliaji wa utatuzi wa kero zake.

Kutakuwa na utaratibu wa kuwapigia wananchi waliowasilisha kero zao kwa ajili ya ufatiliaji wa mwenendo wa utatuzi wa kero zao.

Kutakuwa na database inayoonyesha kero zilizoletwa,sekta ya kero,sehemu zilizotoka pia taarifa ya kero zilizotatuliwa na kero ambazo hazijatatuliwa.

MALENGO
  1. Kuongeza wigo wa wananchi kuwasilisha kero zao ili ziweze kutatuliwa.
  2. Kuwapunguzia gharama za usafiri wananchi wanaosafiri kwa ajili ya kuwasilisha kero zao.
  3. Kuongeza faragha kwa wananchi pindi wanapowasilisha kero,wananchi kueleza kero zao kwa kujiamini zaidi.
  4. Kutoa fursa kwa wananchi wanaokaa maeneo ya pembezoni kuwasilisha kero zao.
  5. Kuwapa fursa wananchi kutumia muda mwingi zaidi katika shughuli za kiuchumi na kimaendeleo.
  6. Kupunguza hatari ya wananchi kuambukizwa magonjwa yanayotokana na misongamano.
  7. Kupunguza gharama za serikali na chama zinazotokana na ziara za kusikiliza kero

Successful story​

Nchi ya India ni moja ya mfano mzuri wa matumizi ya call center katika kuwasiliana na wananchi. Programu ya "Janani Sewa" iliyozinduliwa na serikali ya India imeweza kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi. Kwa kutumia huduma hii mwananchi anaweza kupiga simu bure na kupata msaada wa kiafya wa haraka kutoka kwa wataalamu wa afya. Janani Sewa ni mfano halisi uliofanikiwa ya namna ambavyo serikali inaweza kutumia call center katika kuwasiliana na wananchi na kutatua kero na changamoto zao.

MAELEZO YA KAULI YA” MAMA ANAKUITA” njoo tuseme kwa mama.
Mama anakuita ni wito kutoka kwa mama yetu Mh.Rais Samia Suluhu Hasani,wito huu umejaa upendo,huruma,unyenyekevu,na ni wito wenye dhamira ya dhati yenye kiu ya kumsikiliza na kumuhudumia mtanzania mwenye kero. Kauli hii ya wito inafanana kabisa na kauli nyingi za upendo kutoka kwa mama zetu wa kitanzania ambao mara nyingi wito wao huwa ni wito wa baraka,wenye kutia moyo,wenye upendo,mafundisho na wenye kuongeza ujasiri wa kupambana zaidi.

Njoo tuseme kwa mama, Piga no ……utete na b.mkubwa, inaonyesha heshima na utayari wa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasani kupokea ,kusikiliza,kushauri,na kutatua kero za watanzania ambazo zimeshindwa kutatuliwa katika maeneo yao.

Piga no ………utete na b.mkubwa ni maelekezo ya namba ya kupiga kwa mwananchi mwenye kero ili aweze kusikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa kero yake.

WALENGWA
Wananchi wote wenye kero na changamoto mbalimbali ambazo zimeshindwa kupata utatuzi kwenye maeneo wanayoishi.

OPPORTUNITIES ZA “MAMA ANAKUITA call Center”
  1. Uwepo wa watanzania wengi wanaotumia simu za mkononi i.e kuwepo kwa line zaidi ya milioni 72 zilizosajiliwa.
  2. Dunia ya sasa kupiga hatua kubwa katika teknolojia na mawasiliano i.e dunia ya sasa kumiliki simu siyo anasa ni swala muhimu na la msingi.
  3. Dhamira ya dhati ya viongozi wa juu za kutatua kero za wananchi.
  4. Kuongezeka kwa mtandao wa upatikanaji wa mitandao ya simu hadi sehemu za vijijini na maeneo ya pembezoni.
  5. Asilimia kubwa ya watanzania kuweza kusikia na kuongea kiswahili.
  6. Muundo mzuri wa utawala wa nchi kuanzia katika ngazi ya shina hadi ngazi ya taifa.
  7. Uwepo wa kero nyingi ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi .
  8. Uwepo kwa uzembe wa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kushughulika na kero za wananchi.
  9. Gharama kubwa inayoingia serikali kugharamia ziara za viongozi kwenda kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

WEAKNESSES ZA “MAMA ANAKUITA call Center”
  1. Kutokuwepo kwa mtandao wa simu kwa baadhi ya maeneo haswa ya pembezoni.
  2. Uwezekano wa wananchi wengi kutumia zaidi “MAMA ANAKUITA call center katika kutafuta suluhu ya changamoto zao na kuacha kutumia majukwaa mengine kama kuonana na viongozi wa maeneo yao.
  3. Mtoa kero kutopatikana kwa ajili ya ufautaliaji.
  4. Muda mrefu wa mwananchi mwenye kero kusubiria kabla ya kuunganishwa kwa ajili ya kusikilizwa.
  5. Uwepo wa gharama za ziada za kuajiri vijana kwa ajili ya kusikiliza kero.
  6. Uwezekano wa baadhi ya wananchi kutoa kero zisizo za ukweli kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
  7. Uwezekano ya wananchi kupiga simu za kero ambazo kiuhalisia siyo kero za msingi na kusababisha foleni kwenye call center.
  8. Ugumu wa “MAMA ANAKUITA call center” kuhudumia wananchi kwa masaa 24.

MATARAJI0​

  1. Kuibuliwa na kutatuliwa kwa kero nyingi kwa kutumia muda mfupi na gharama nafuu.
  2. Itatoa picha kamili ya hali halisi ya mambo yanayoendelea field na kusaidia kwenye maamuzi ya serikali.
  3. Itasaidia kutoa picha kamili ya hali halisi ya mambo yanayoendelea field na kuisaidia serikali kubadilisha namna ya utendaji wa serikali.
  4. Kuongezeka kwa uwajibikaji wa viongozi kuanzia ngazi za chini hadi ngazi za juu.
  5. Serikali kuweza kubaini viongozi wazembe kwa urahisi.
  6. Serikali kuweza kupata tathmini ya sekta zinazofanya vizuri na sekta ambazo hazifanyi vizuri.
  7. Kuimarika kwa mahusiano na mawasiliano kati ya serikali na wananchi.
  8. Serikali kupata taarifa za aina za kero zinazowasumbua watanzania wengi
  9. Kuzalisha ajira kwa vijana wa kitanzania.
  10. Kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali na chama kwa kupunguza gharama za ziara za viongozi kwenye kufatilia kero.
  11. Wananchi wanaokaa pembezoni kupata fursa ya kuelezea kero zao.
MATARAJIO YA KISIASA
  1. Watanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasani pamoja na chama cha mapinduzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa October 2025.
  2. Serikali kuweza kuchukua hatua za haraka juu ya kero zinazosumbua idadi kubwa ya wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2025.
  3. Serikali ya chama cha mapinduzi kupata tathmini halisi ya utelekezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
  4. Wananchi kuwa mashuhuda wa uwajibikaji wa serikali katika kutatua kero na changamoto,imani ya wananchi kwa serikali kuongezeka maradufu.
  5. Imani ya kundi la vijana kwa serikali kuongezeka kupitia vijana kunufaika na ajira.
Kazi iendeleee……Mama🖐 tena.

Collins the boy 2024

audaxc@yahoo.com
 

Attachments

Back
Top Bottom