Kwetu mimi pekee sijaelimika ila useremala unanibeba, kaka na mdogo wangu walioelimika wanasota, nashauri VETA kabla ya chuo

Kwetu mimi pekee sijaelimika ila useremala unanibeba, kaka na mdogo wangu walioelimika wanasota, nashauri VETA kabla ya chuo

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Sisemi kwamba watu wasisome, La Haha! bali wawe na "back up a.k.a Plan B, Sio vibaya mtu mwenye degree awe na ujuzi wa kushona, ujenzi, useremala, upishi, n.k. huu ujuzi una uhakika zaidi wa kumlisha kuzidi nafasi za kazi ambazo wachache huajiriwa, anapomaliza chuo awe na uhakika wa kuanza kujitegemea mapema huku akiendelea kujaribu bahati yake kwenye ajira.

Kuwa na degree ni sawa na kujua kufua nguo Kwa mashine, kuwa na ujuzi wa ziada ni sawa na kujua kufua nguo wa mikono, Ni baraka kujua vyote ila ni muhimu zaidi kujua kujifulia kwa mikono. Vivyo hivyo na sisi kuwa na mbadala ni jambo jema zaidi.

Naumia sana nikifikiria wazazi walivyojinyima kutulipia ada, kuna kipindi walikopa kabisa, naumia sana kuona mategemeo ya wazazi kwa ada walizolipa hayajafikiwa,,, Inauma sana !!

Ukiachana na maumivu ya wazazi na mimi napitia maumivu mazito, kaka na mdogo wangu walisoma kwa juhudi sana, sioni kama ipo fair kwa wanachopitia, walistahili zaidi sana sana sana. mtu alie kwenye unafuu wangu akijisifu ana ahueni basi ni wazi ni mjinga.

Binafsi niliishia form 4 mwaka 2012 shule ilinipita kushoto, Nilifaulu tu English kwa B kwengine F na D mzee aliniambia nijiandae kurudi kijijini, ilibidi nikajiongeza nianze kujifunza chochote nikaingia kwenye useremala kwa msaada wa mjomba wa rafiki (mjini connection), nikawa saidia fundi kidogo nikaweza kuhama hata nyumbani na kumiliki pikipiki, nikajichanga changa na mimi nikawa na ofisi yangu inayonipa kipato si haba kwakweli hata kagari kapo, haikuwa rahisi hata kidogo hasa mwanzoni, kuna kipindi kidume chozi lilinitoka kwa ugeni wa kazi lakini nilikomaa.

Sasa hapo home kuna bro na mdogo wangu wa kike wamemaliza vyuo ngazi ya degree lakini mambo si mambo kiuchumi, bro alihangaika hizi kazi za kujitolea, akaingia kitaa akapata kazi kampuni binafsi kazi kibao malipo kiduchu, alisota miaka minne kampuni ikafungwa na kazi ikaisha,,, ikabidi home pale tujichange tumpe mtaji, ikabidi ajifunze kunyoa nae akafungua ofisi yake, kiuchumi pana nafuu lakini hadi kafika hapo kapitia misoto kwa ukosefu wa ajira za ofisini.

Kwa mdogo wangu nae tangu 2020 alipomaliza chuo hali bado sio poa, ilibidi tujichange change nae apige mwendo, biashara ya keki mara ya kwanza ilibuma kwake akawa yupo home, tukajikusanya kusanya kwa sasa angalau ana kamgahawa kidogo pana unafuu.

Nilichokuwa najiuliza ni kwamba, hizi elimu zinaandaa wengi wawe maofisini wanasukuma kalamu na kukaa kwenye viti wakisubiri mishahara lakini hizi ajira zimekuwa adimu, nimeona kwamba yafaa zaidi kungekuwa kuna veta kabla ya kwenda chuo.
 
huwa nasikitika sana napoona kaka na mdogo wangu wameelimika mpaka degree lakini shughuli wanazofanya ni kinyume kabisa na elimu zao na kiuchumi zipo chini.

Binafsi niliishia form 4 mwaka 2012 shule ilinipita kushoto, mzee aliniambia nijiandae kurudi kijijini, ilibidi nikajiongeza nianze
Kwaiyo unajiona ushatoboa Maisha Mkuu?

Mtaacha lini dharau wabongo !!
 
Nakuunga mkono sana kwenye hili Mkuu, tena kama kwa sasa hali ya kiuchumi hairuhusu basi badala ya JKT ni afadhali iwe kwenda VETA.

Hata kama sio wote watapata nafasi, hao hao wachache kwa utaratibu utakaoonekana unafaa waende wakajifunze ufundi.

Kuna watu watatetea JKT lakini kiuhalisia ni kupotezeana muda na kutesana bila sababu.
 
Ni kweli kabisa, kwenye maamuzi inabidi tupime mzani sehemu yenye uhitaji zaidi.

Kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la ajira, kwenda veta ni muhimu zaidi kumuandaa kijana awe na ujuzi wa kuanza kujitegemea akikosa ajira ama anavyoendelea kuomba ajira.

Kwenda JKT sikatai Kuna umuhimu wake lakini kujifunza kujilisha Kuna umuhimu zaidi, Mtu alimaliza chuo na hana ajira kitu muhimu zaidi ni yeye kuwa na ujuzi aanze kujitegemea kuliko kuwa na ukakamavu wa JKT.
 
Naumia sana nikifikiria wazazi walivyojinyima kutulipia ada, kuna kipindi walikopa kabisa, naumia sana kuona mategemeo ya wazazi kwa ada walizolipa hayajafikiwa,,, Inauma sana !!
Upeo wako wa mambo ni mdogo,ukitaka kujua uhodari wa samaki shindsna nae akiwa kwenye maji,samaki hawezi kuwa mwamba akiwa nchi kavu!!

Hao ndugu zako wangapata fulsa ya kile walichosomea,wangekuwa mbali kwa maendeleo.Kufundisha,ukalimani wa lugha,matumuzi ya IT ofisini,wewe na VETA ysko unaziweza hizi kazi?!!

Kibaya kuhusu Elimu ya juu ni kukosa Skills,waalimu wa VETA ni kutoka kwenye kada ya Elimu ya juu,kama ulikuwa hujuhi,usiwacheke ndugu zako,instegemea wamesomea nini!kama wamesoma Civil engineering,harafu hawawezi kazi ya uselemara,hapo Sawa,maana useremala ni kipengere kwenye kozi yao,lakini kama mtu kasoma,"degree ya heritage preservation,political science,au udakitari,hizi taaluma lazima upewe fulsa ya kuajiliwa kwanza,bila hivyo ni ngumu,hata wao wakienda veta kusoma skills,kwenye ujuzi mbalimbali,watatoboa vzr
 
Hata hujelewa mantiki ya mtoa mada aisee. Hili Taifa hili aisee
 
Siwez Kuamini kama mpaka leo inahitaji ka elimu juu ya UMUHIMU WA ELIMU. MTOA MADA HUONI HATA FIKIRIA YAKO YA TABU ALAF UNAONA UMEMELIZA TAYARI?
Inaweza kuwa kafanikiwa kwa level yake, na fikra zake zimeishia hapo ila angepata elimu na anchofanya, angekuwa mbali mara 10 ya sasa..

Ndio umuhimu wa elimu, unapokuja..uwezo wa kung'amua mambo kwa upana na weledi..

Angekua ashafungua kampuni yake, anatafuta tenders private na Government, na hata biashara ya kimataifa..

Na angeweza,diversify shughuli zake kiurahisi, ila kupondea elimu ndio ameona ni vizuri zaidi.
 
Waliofeli wanafeli Kwa kutumia kufeli Kwa watu wengine kama kipimo cha wao kufaulu. Haoni sabab y kuangalia waliofanikiwa zaidi Kwa sabab Kuna watu wamefeli zaidi yake. We unadhan huyu mtu yuko barab-bara?. Ndo hawa wanaoroga ndug wasifanikiwe ili wawasaidie walahi
 
Back
Top Bottom