Kalaga Baho Nongwa
JF-Expert Member
- Sep 27, 2020
- 9,953
- 23,150
Nimuonee wivu nani Sasa?Ukizidisha wivu unakuwa mchawi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimuonee wivu nani Sasa?Ukizidisha wivu unakuwa mchawi
Bongo nyoso Yani wewe kuwa seremala ushatoboa maishaNaumia sana nikifikiria wazazi walivyojinyima kutulipia ada, kuna kipindi walikopa kabisa, naumia sana kuona mategemeo ya wazazi kwa ada walizolipa hayajafikiwa,,, Inauma sana !!
Ukiachana na maumivu ya wazazi na mimi napitia maumivu mazito, kaka na mdogo wangu walisoma kwa juhudi sana, sioni kama ipo fair kwa wanachopitia, walistahili zaidi sana sana sana. mtu alie kwenye unafuu wangu akijisifu ana ahueni basi ni wazi ni mjinga.
Binafsi niliishia form 4 mwaka 2012 shule ilinipita kushoto, mzee aliniambia nijiandae kurudi kijijini, ilibidi nikajiongeza nianze kujifunza chochote nikaingia kwenye useremala kwa msaada wa mjomba wa rafiki (mjini connection), nikawa saidia fundi kidogo nikaweza kuhama hata nyumbani na kumiliki pikipiki, nikajichanga changa na mimi nikawa na ofisi yangu inayonipa kipato si haba kwakweli hata kagari kapo, haikuwa rahisi hata kidogo hasa mwanzoni, kuna kipindi kidume chozi lilinitoka kwa ugeni wa kazi lakini nilikomaa.
Sasa hapo home kuna bro na mdogo wangu wa kike wamemaliza vyuo ngazi ya degree lakini mambo si mambo kiuchumi, bro alihangaika hizi kazi za kujitolea, akaingia kitaa akapata kazi kampuni binafsi kazi kibao malipo kiduchu, alisota miaka minne kampuni ikafungwa na kazi ikaisha,,, ikabidi home pale tujichange tumpe mtaji, ikabidi ajifunze kunyoa nae akafungua ofisi yake, kiuchumi pana nafuu lakini hadi kafika hapo kapitia misoto kwa ukosefu wa ajira za ofisini.
Kwa mdogo wangu nae tangu 2020 alipomaliza chuo hali bado sio poa, ilibidi tujichange change nae apige mwendo, biashara ya keki mara ya kwanza ilibuma kwake akawa yupo home, tukajikusanya kusanya kwa sasa angalau ana kamgahawa kidogo pana unafuu.
Nilichokuwa najiuliza ni kwamba, hizi elimu zinaandaa wengi wawe maofisini wanasukuma kalamu na kukaa kwenye viti wakisubiri mishahara lakini hizi ajira zimekuwa adimu, nimeona kwamba yafaa zaidi kungekuwa kuna veta kabla ya kwenda chuo.
Umeeleza vema sana, hongera. Lakini ni ukwel usiopingika, ili kufikia katika level hiyo ya kuuza katika masoko ya nje, ni lazma uhitaji na uhusikaji wa huduma toka profession nyingine zitatumika. Kuna issue za kodi na ushuru kwa mfano, mambo ya manunuzi na accounting, kuna finance na ubora. Ni mlolongo mpana na kutekelezeka kunahitaji mabadiliko ya kimfumo.Sio tatizo, hata watanzania wote tungekuwa tunazalisha bidhaa, bado soko lingekuwepo na ni soko kubwa tu. Kwakuwa uzalishaji huo ungefanywa na watu mahiri katika fani zao, basi wangekuwa wanaproduce efficiently, na hivyo kuweza kuuza hata masoko ya nchi nyingine, kwakuwa tunaproduce at absolute advantage.
Kipindi nipo Arusha moja ya kitu nilichowakubali kule madogo hata akiwa na elimu hizi za course work mara nyingi anakuwa na kifani kingine...atakosa labda hela ya kujenga lakini hizi zingine za bia mbili tatu na kuvaa hazimzingui..Ni vizur sana,pia hata akienda chuo tuwe tunawaandalia kamtaji kakuja kuzugia pale anapotoka chuo
Wazo la mleta mada ni zuri sana. Ukisoma vizuri uzi wake, hasemi watu wasisome, bali wawe na "back up". Sio vibaya mtu akiwa hata na professions mbili, zote zitakuwa na msaada kwake.Umeeleza vema sana, hongera. Lakini ni ukwel usiopingika, ili kufikia katika level hiyo ya kuuza katika masoko ya nje, ni lazma uhitaji na uhusikaji wa huduma toka profession nyingine zitatumika. Kuna issue za kodi na ushuru kwa mfano, mambo ya manunuzi na accounting, kuna finance na ubora. Ni mlolongo mpana na kutekelezeka kunahitaji mabadiliko ya kimfumo.
Kinachozungumzwa na wengi, na nafikiri hata hoja ya mleta mada imelala katika mfumo wa uzalishaji kwa namna ya "sole proprietorship", hii haiwezi leta tija.
Mtaala wa Veta unafundisha fani moja? Kwanini unahisi bidhaa zinaweza kukosa soko?Niko na mtazamo tofauti kidogo. Kufungwa kwa makampuni/ kampuni kunaweza sababishwa na hali isiyoridhisha kiuchumi. Logic ya kawaida kabisa, ili kampuni iweze tengeneza faida, lazima kuwe na soko la uhakika kwa bidhaa au huduma zake.
Sioni hii mantiki ya kuona kupeleka vijana VETA kama suluhu la kile vijana wengi wanakabiliana nacho, tatizo la ajira, logic ni kwamba, hao wataofanikiwa kuhitim mafunzo Veta, wataangukia katika hilo kundi la wazalishaji (Producers). Ili waweze pata kipato na kujikim lazima bidhaa zao ziwe na soko la uhakika kwa walaji wa mwisho, fikiri tu, kila kijana awe mzalishaji na hakuna soko la uhakika kwa hizo bidhaa, tutakua tumetatua hilo tatizo?
Suluhu la hili, ni lazima kuwe na balance, walioajiriwa na hawa ndio ndio soko la uhakika kwa bidhaa/huduma zitazozalishwa na hao waliojiari kama mnavosisitiza hapo.
Uzalishaji pasipo na soko la uhakika, ni kazi bure.
sina muda huo..Sasa badala ya kukosoa mawazo ya wanaume,weka ya kwako tuone ulivyoelewa!!sio lazima tuelewe sawa,we umeelewa vipi?