Kwetu mimi pekee sijaelimika ila useremala unanibeba, kaka na mdogo wangu walioelimika wanasota, nashauri VETA kabla ya chuo

Kuelimika maana yake nini? Au mpaka ufike chuo kikuu.. Africa bado tuna safari ndefu sana.. (Useremala ilikuwa fani moja wapo ya Yesu ujue)
 
Hana muda wa kuangalia waliofanikiwa zaidi yake, wakat ana benchmarking ya familia inamtosha kupiga kelele..
 
Bila shaka waliocomment wengi ni wenye degree na wapo kwa mashemeji zao,nashangaa wanamuwakia mtoa post,wakati mtoa post alikuwa anatoa ushauri.

Hili nimeshajiandaa niandae mazingira ambayo mtoto akiwa likizo aweze kupata muda wa kujifunza utaalamu mwingine nje ya masomo yake ili hata akimaliza chuo aweze kufanya mambo mengine nje ya alichokisomea
 
Hizo gharama za chuo bora nitamshauri aende VETA akimaliza nimpige na kama M2 hivi ya mtaji...Ila kama akilalamika sana unamuacha tu aende chuo
 
Wewe ndo uwezo wako mdogo sana tena sana.Huyo jamaa kaongelea changamoto ambazo familia nyingi zinapitia na yeye katumia familia yake kama mfano mzuri.

Na wala hajasema anajisifia...Na pia kama kweli kafanikiwa hivyo nampa pongezi.Na suala sio hizo ajira tu..ni malipo au mishahara baada ya kuajiriwa na uhalisia wa gharama za maisha.

Lazima tuweze kutumia elimu zetu tuweze kusurvive na kuishi..na ndo maana tunafundishwa vitu vingi sana ukiachilia professional tunazotumia.

Waendelee kuwasupport kwa biashara ndogo ndogo hao ndugu zake...na pia wao wanaweza kutumia elimu zao na exposure zao kuangalia hiyo biashara ya useremala wanaweza msaidia vipi etc...Elimu zao zitumike nyumbani, na watafanikiwa.Na hata huko baadae wakipata ajira waendelee kuendeleza hizo biashara zao na zaidi wakimtumia huyo huyo ndugu yao ambaye tayari anaexperience ya ujasiriamali
 

Mkuu, kwa hoja hizi, una elimu kubwa sana. Endelea kupambana, utaajiri wengi.
 
Hamna lolote umejitungia uwongo ujifurahishe na ukashifu elimu ambayo ulishindwa kuipata. watu kama wewe tunawafahamu wako wengi ni kama wachawi wako kuwakatisha tamaa watu wengine wasisome. We umeshindwa kusoma wacha upambane na hali yako siyo kuja kusemea elimu vibaya humu. Elimu kuitafuta ni agizo la Mungu watu wataenedelea kusoma mlioshindwa pambaneni na mambo yenu mengine.
 
Nakuunga mkono.
Kwa sababu lengo la kupeleka vijana JKT ilikuwa kuwafanya wawe wazalendo,kuwaondoa uwoga na kuwa shupavu/shujaa.
Lakini nikiwacheki bado ni waoga na panya road wanasumbua mitaani.
 
Na ndiyo maana wadau wa elimu tunaendelea kupiga kelele ili serikali ibadilishe hii mitaala yao ya sasa.

Kuna umuhimu mkubwa wa kuwekeza kwenye elimu ya kumjengea mhitimu maarifa na ujuzi zaidi, kuliko hii elimu ya sasa ambayo imejikita zaidi kuwandaa wahitimu kufaulu mitihani ya kukaririshwa, na baadaye kuajiwa.

Elimu ya ufundi, ubunifu, ujasiriamali, usimamizi katika biashara, michezo, muziki, tehama, nk ipewe kipaumbele kwenye mitaala mipya.
 
Kwenye ukoo wetu kuna wasomi kibao lkn yupo Mwamba mmoja wa darasa la 7 na biashara yake ya mkaa anakimbiza wote. Wanamuogopa
Ndiyo matokeo ya ujinga, angalia ulicho-comment. Watu hawasomi watajirike, elimu ni kwa ajili ya kutoa huduma ndugu. Utibiwe na daktari, nesi, upimwe na mtaalam wa maabara, uandikiwe dawa na mfamasia. Ujengewe na injinia, mifugo yako itibiwe na bwana mifugo. Uhudumiwe benki na mtalam wa mambo ya benki. Kesi yako isimamiwe na mwanasheria. Mkipataga matatizo ndio mnajua umuhimu wa wasomi sahivi umekula mihogo yako huna tatizo unaweza kuandika chochote. Hakuna mbadala wa elimu ukishindwa kaa pembeni. Ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba. Nenda shule umri ni namba tu uone raha ya kusoma, ukitaka kujua utamu wa ngoma uingie ucheze.
 
Mstari wa mwisho kuwe na Veta kabla ya chuo ndo umebeba dhima yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…