DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU),
Kyara, amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais, atahakikisha anarejesha heshima ya wanaume ambayo imeonekana kupotea, kutokana na ukweli kwamba wengi wao siku hizi wanakwepa majukumu na kutegemea wanawake au kujikomba kwa watu ili kupata fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Njedengwa jijini Dodoma, mara baada ya kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea urais kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Kyara amesema suala hilo ni miongoni mwa vipaumbele vyake. Majalio, ambaye aliambatana na mgombea mwenza wake Satia Bebwa, amesema: “Hakuna Taifa bila mwanaume. Tunapoangalia kwenye usawa, ni muhimu kuhakikisha kundi hili haliachwi nyuma. Sasa hivi majukumu mengi yanabebwa na akina mama, hali imekuwa mbaya, vijana wengi wameingia kwenye ‘uchawa’ badala ya kupambana kufanya kazi.”