Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Karibu sana Mwakalinga! Hivi SUA ulimaliza ama hukupata maksi za kutosheleza kuwa warded BSc Agr Eng na kukimbilia Poland? You can not fool us all da time mazee

Masanilo,

Unaweza kuandika utakacho kuhusu Mwakalinga lakini ambacho huwezi kufuta ni mafanikio yake katika shule na kazi.

Hakuna hata sehemu moja ambapo Mwakalinga amesema alimaliza SUA wala kuondoka kwake SUA hakukuwa kwasababu ya kufeli shule.

Mwakalinga ana degree tatu katika level ya masters, moja ambayo aliipata Poland na mbili akiwa amesoma UK. Pia amekuwa kwenye Telecoms tokea alipoajiriwa mwaka 1997 mpaka leo bila kukosa kazi hata siku moja, tena kwenye field ambayo ilikuwa na matatizo makubwa na wafanyakazi wengi kupoteza ajira kati ya 2000 na 2004. Alikuwa Lucent Technologies wakati ilipopunguza wafanyakazi wake kutoka 150,000 mpaka kufikia 20,000.

Andika utakacho lakini huwezi kukashifu mafanikio ya Mwakalinga kwenye shule na kazi.

Labda utusaidie wewe ndugu yetu umefanya nini kwenye taaluma yako hata udiriki kukshifu elimu za wengine?
 
Wakuu,

Mimi ndio nimerejea leo kwenye makazi yangu baada ya kuwa kwenye safari nikiongozana na ndugu George Mwakalinga ambaye alienda kujitambulisha kule Kyela na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge mwakani.

Asante George Mwakalinga, nenda kagombee, tunataka ushindani wa kweli, na tusingependa mtu yeyote ahodhi jimbo bali tunataka mtu apate ubunge kwa njia ya ushindani, sababu ni moja tu; people perform better when they are competing.

Mwakyembe naye ajitahidi, asafishe makosa yake, na akiona hawezi basi apishe; ingawa bado namuaminia sana kwani yuko hapa na mara nyingi watu wakitoka nje wanachukua muda ku-settle na kuelewa kalcha ya watu hasa wa "nyumbani"

La mwisho Bwana Mwakalinga aka Mtanzania, ni kwamba tunaomba mungu aje na mgombea mwingine nyutro asiyeleta mgawanyiko huko Kyela na wewe na Mwakyembe wote mpigwe chini, tutampokea mwakyembe kawe awe mbunge wetu kwasababau tunajua umuhimu wake

MTM
 

Suleiman,

Nafikiri ukisoma humu ndani tangu jana tu, utaona jinsi watu wanavyoandika Pumba. Wengine ni Washabiki wa Mwakyembe na wengine wapinzani wake. Sidhani kama Mwakalinga tayari anawashabiki kiasi hicho wakati ndiyo kwanza katangaza NIA ya kugombea.
Kama nilivyoandika mwanzo, ntaomba unizoee hivyo hivyo. Ni kama ujumbe wa FATAKI. Huo anaweza kuwa hata kaandika Mwakyembe mwenyewe. Umejaa vijisifasifa vya kutafuta na vijembe kibao. Sijui nani kauweka hapa na sipo hapa kusema Mwakyembe ni FATAKI. Ila aliyeuandika na ule wa Kalengamab (anayejiita kuwa alikuwa na Mwakalinga from day kama mwandishi wa habari wa kambi yake) hizo zote zimeandikwa na kambi ya Mwakyembe. Hiyo upende usipende ndiyo ukweli.

Ukizisoma zote ni sawa kabisa na ile makala kwenye MAJIRA ambayo Mwakalinga alilalamika kuwa wameanza kuchafua hata hajafika Tanzania. Zote zimeandikwa kwa KUMSIFU Mwakalinga huku zikionyesha ujuzi wa hali ya chini sana ya uandishi kukosa kabisa elimu. Na hapohapo ndipo anapokuja FATAKI na ushauri wake. Hii yote ni well planed attack. Wenye macho tunaona. Hawa jamaa wanamuogopa sana Mwakalinga kiasi kwamba usiku watakuwa wanamuota.

Ila nataka tu niwakumbushe Maneno ya mzee Malecela juzujuzi kwa Mbowe "Vita haishindwi angani, ila inashindwa ardhini". Na nyie kambi ya Mwakyembe, kama mwataka kumshinda Mwakalinga basi hiyo vita msipigane kwenye magazeti na Internet maana huko Kyela, sijui kama hizi habari zenu zinafika. Na hata kama zinafika, basi wanaona wapi mnasema ukweli na wapi mnadanganya.
 
Masanilo,

Labda utusaidie wewe ndugu yetu umefanya nini kwenye taaluma yako hata udiriki kukshifu elimu za wengine?

Du,

Haya kaka Masanilo. Wamekugeukia sasa.

Lete hapa shule yako na mafanikio yako kazini kwako tuyaone......
 
Mtanzania,

Pole sana safari na karibu sana JF. Naona ujiandae sana kusoma maana habari za Mwakalinga zilikuwa zinaongezeka page hadi page kama wakimbiaji wa mita 100. Sasa una page kibao za kusoma. Kaa mkao wa kula.

Anyway, weekend tuwasiliane. Salimia Capital City na wanae.
 
Wakuu,

Mwaka 2005, Mwakalinga alimuunga mkono Dr. Mwakyembe. Kule anakotoka Mwakalinga (kata ya Katumba Songwe) ndio ilikuwa ngome kuu ya Mwakyembe. Wadogo zake Mwakalinga walikuwa katika wapambe zake Mwakyembe.

Hii ya uhusiano wa Mwakalinga na Mwakipesile linatoka wapi? Kuweni makini kutambua
strategy waliyoiandaa ili kumchafua huyu kijana. Moja wanataka kumhusisha yeye na Mwakipesile; pili kumhusisha yeye na mafisadi.

Uzuri tuna mawasiliano yote ya emails katika ya Mwakalinga Na Dr. Mwakyembe mpaka mwaka 2006. Mawasiliano ambayo yanaonyesha walikuwa wana ushirikiano na waliungana pamoja kumng'oa Mwakipesile.

Kinachowashinda ni kwamba huwezi kukuta au kuona mahali popote ambapo Mwakalinga amefanya kitu chochote ambacho ni kinyume na maadili. Amejenga biashara zake Kyela zinazokaribia bilioni kwa sasa na nenda hata leo, huwezi kukuta hata mtu mmoja anayesema aliwahi kudhulumiwa au kunyang'anywa kitu na Mwakalinga.

Kuweni makini sana mnaposoma hizo articles zao? Mtu kugombea ubunge sio dhambi; hivyo hii ya kuamua kumvaa Mwakalinga kwa kila njia, wanajidanganya bure.

Mwandishi Felix Mwakyembe ambaye ni mdogo wake Mbunge Mwakyembe aliandika makala ndefu kwenye gazeti la RAI akichambua siasa za Mbeya. Bahati mbaya wakaipa habari yake ukurasa wa mbele. Huyu jamaa ambaye anamjua Mwakalinga vizuri, kwenye hiyo habari akaandika ni kijana aliyeko masomoni Uingereza. Lengo lilikuwa kumshushia aonekani ni kijana na tena mwanafunzi tu. Hiyo ni dalili ya watu walio na wasiwasi mkubwa na sasa wanahangaika kwenye magazeti na JF kupika kila aina ya uongo.

Nitaendelee kujibu baadhi ya hoja kidogo kidogo kabla ya kuelezea safari zetu.
 

Mkuu Sikonge,

Asante sana mkuu; wewe na mimi na Mwakalinga tumetoka mbali sana na naona umeamua kupambana kwa nguvu zote kutetea washikaji wasipakwe matope.

Naona kuna kurasa nyingi sana, nitakuwa najibu hoja moja moja ili wana JF wengine wafahamu na hizo sumu wanazolishwa zisiweze kuwadhuru.

Nitakupigia simu weekend nikupe michapo ya Kyela.
 
Du,

Haya kaka Masanilo. Wamekugeukia sasa.

Lete hapa shule yako na mafanikio yako kazini kwako tuyaone......


Teh teh teh teh am not that cheap mpwa wangu! sijaanzisha JF wala kuwa mweka hazina wa Tanzanet, sina supermarket, One star hotel kifupi sina mafanikio na siwezi gawa laputopu hahahahahah mwaka 2010 balaa
 
Wakuu,

Naomba kwa wale ambao mna mtetea au ni wapambe wa Mwakalinga, muache hasira na andikeni hoja. Jino kwa jino wote tutageuka kuwa na ngeu.

Hilo ndilo ombi la Mwakalinga mwenyewe. Kwa mfano kuna sehemu nimeona mtu kaandika Mwakalinga atamwaga laptop kila shule. Jamani, Mwakalinga hajasema hivyo na naamini hata siku moja hawezi kusema hivyo maana huwa haahidi mambo asiyoweza kuyafanya.

Tubaki kwenye hoja.

Kule Kyela watu wameelemika na kufarijika, tusiwachanganye na kuwaangusha kwa habari ambazo sio kweli. Mtu anaweza akaja hapa JF akasoma na akafikiri ni kweli mwakalinga ameahidi hivyo; baadaye akiona hakuna laptop akaanza kusema jamaa alidanganya.
 
Karibu mkuu Mwakalinga. Nakukaribisha huku tukiamini kwamba hujatumwa na mafisadi (akina RA) kugombea Kyela. Kama unadhani una ubavu wa kupambana na mpiganaji Mwakyembe, karibu kwenye kilinge.
 

Bwana George Mwakalinga aka Mtanzania. Karibu tena ndugu. Ila ningependa kukupa onyo mapema. Kwa vile umetangaza azma yako ya kugombea ubunge huko Kyela kupitia tiketi ya CCM, kaa ukijua kuwa hatutakuwa na simile pale utakapoanza kubweteka na kuwa fisadi (endapo utashinda). Tutakufanyizia kama tunavyowafanyizia mafisadi wengine.
 

Mtanzania;

Ninahisi ninakufahamu, lakini siamini kuwa wewe ni Mwakalinga. Hilo inatokana na style ya uandishi wako kuwa tofauti na Mwakalinga..

Anyway nitakupigia simu baadaye. Unajua saa nyingine inakuwa ngumu mtu kumchafua mtu bila sababu na ukakaa kimya.

Yap! jino kwa jino sio stahili nzuri.

Karibu tena
 


Sikonge,

yote haya yanaweza kuwa ya kweli lakini hayatoi kinga kwa wewe (katika hali ya kawaida na heshima ya hii forum) kutoa maneno ya kudhalilisha gender au watu wasiohusika na hii forum.

Ukiwa kama mmoja wa wale wanaodai kuitakia hii forum mafanikio (hata kuwa na thread inayoomba watu wachangie hii forum), inakuwa kinyume na tija kwa wewe kutoa maneno yanayodhalilisha watu, au kutumia matusi na lugha moja au nyingine ambayo inadhalilisha forum hii ambayo unadai kuipenda na kuijali sana.

otherwise, ninaendelea kusoma mambo na vijimambo (kashfa na matusi) hoja na viroja huku nikiendelea kushuhudia huu mpambano wa karne.
 
Naona kuna kurasa nyingi sana, nitakuwa najibu hoja moja moja ili wana JF wengine wafahamu na hizo sumu wanazolishwa zisiweze kuwadhuru.
Hapa tupo pamoja Mwakalinga, nakupongeza kusimamia kidete unachokiamini, kwa kweli njoo na maziwa wa kutosha wapambe wako wamekudhalilisha hapa......

Tutajua kutoka kwako, kwanini huamniki ulitamka mbele ya mmoja ya waasisi wa JF uko vacation, hujaja kutangaza kuogombea kitu ambacho ni haki yako kikatiba, mara vuru vuru vuru mimi msomi wa IT kutoka Poland nakuja waletea maendeleo Kyela.Ooooh my GOD..baada ya kutokea Monduli na kupewa mikakati, mmoja wapo kumleta mtoto wa JK ambaye naye anajiona ni Rais wa jamhuri kama baba yake, mipango hiyo ulianguakia pua...

Tunaomba ujibu moja moja mahusiano yako na Mwakipesile RA na EL

Tupo pamoja Engineer wa Kilimo na IT na Telecoms
 


The original..... yupo wapi yule ponjoro aliyekuwa kule BCS? LOL

Unanikumbusha mbali sana kaka.
 
Karibu mkuu Mwakalinga. Tunakukaribisha huku tukiamini kwamba hujatumwa na mafisadi (akina RA) kugombea Kyela. Kama unadhani una ubavu wa kupambana na mpiganaji Mwakyembe, karibu kwenye kilinge.
 

Ndugu mtanzania,

mimi naamini kuwa wewe una kila haki ya kugombea ubunge wa sehemu yoyote ile na kwa mwaka au wakati wowote ule unaopenda. Kitu kimoja tu ambacho kimenifurahisha ila pia kunishangaza (kwa kweli sikuwahi kujua hili kabla ya kusoma hii thread), ni kiwango cha utajiri (wealth) na investment zako.

Kwa kweli, inaonekana kijana umebarikiwa sana kimaisha na katika hili naomba sana nikupongeze. Endeleza kazi zako na biashara zako na kila unachofanya kwa maisha yako binafsi na hata ya kisiasa kama ukiamua kuingia rasmi.

Hata hivyo ukweli utabaki pale pale kuwa, mwanasiasa yeyote lazima awe tayari kukumbana na upinzani na ushindani ili kupima au kujenga uwezo wake wa kikazi na kisiasa. Kwa hili, usikasirike au kuchukia unapopingwa. Hayo ni mambo ya kawaida kwenye siasa.

Asante na hongera sana kwa mafanikio yako yote.
 
The original..... yupo wapi yule ponjoro aliyekuwa kule BCS? LOL

Unanikumbusha mbali sana kaka.

Ponjoro yupo...anajiita The Truth....siku hizi hamna anayempa attention so naona ameamua kusepa.

BCSTimes...daaah tumetoka mbali sana. Nakumbuka mpambano wako na Mwanakijiji wakati bado unatumia jina la Fikiraduni....Lol
 
Mkuu Mtanzania,

Karibu sana tena kwenye jukwaa ingawa limejaa mambo mengi tu mengine ni ajabujabu tu.

Lakini wewe unajua mwenyewe nini unafanya na sisi wote wapenda maendeleo tupo pamoja nawe kuona kwamba maendeleo Tanzania yanaanzia Kyela na la muhimu ni watu kuwa na "critical thinking".

Ila wengi humu ama wametaka kuchafua hali ya hewa au wanaleta utaniutani tu.
 
Hehehehe...very funny. Naona Mtanzania anajaribu kukana kuwa yeye sio George Mwakalinga lakini hakuna mtu anaye buy hiyo BS....Lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…