Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM


Hapa tuko pamoja


Nadhani hii kazi alishaianza hapa kwa muda sasa kwa kutumia ID zake za JF (ambazo inaonekana kama ni nyingi) au kutumia wasemaji wake.


Hapa tuko pamoja ... huu ni uchaguzi wa karne. Upande mmoja kuna mafisadi woote kuanzia Lowasa na Mwakipesile, upande mwingine kuna Mwakyembe, na wakimaliza kupata mgombea wao, watakutana na mtu ambaye upinzani watamsimamisha huko Kyela.


Haya ni maoni yako binafsi na sina sababu yoyote ya kuyachukulia kama facts.


Ha ha ha hah,

hii ya barabara ya lami imenivunja mbavu kabisaaa.


Naona ushauri wako umefuatwa kabisaaaa.


Respect kwako pia. George kama ameingia kwenye siasa ategemee kupata maswali na scrutiny ambayo wanasiasa wote bongo wanapewa. Na kwa vile anaingia CCM (chama ambacho mi nakihesabu kama cha mafisadi) basi George ameingia kwenye kundi la mafisadi kwa hiyo ategemee the same standard against mafisadi toka kwa wana JF.

Respect again na unakaribishwa muda wowote kwani mimi nitakuwa hapa hadi kieleweke.
 

George kweli ni smart kuweza kucheza na pande zote mbili za Mwakyembe na Mwakipesile kwa muda wote huu. Ninachojiuliza sasa hivi, ni kwa George ameamua kuchukua upande wa mafisadi wa kina Mwakipesile?
 
Fataki yupo wapi?, ningependa aje apambane na Mtanzania ana kwa ana.

Najua upo bize mkuu na mastrategy ila usikimbie sana, Siku hizi hata kwenye simu unaweza kuingia kwenye net. Ndo maana tunataka viongozi wa kisasa wanaoenda na wakati.

Pole FATAKI dakika zina tick tick tick tick..
 

wewe nawe mkuu kama kipindi tukiwa elementary school halafu baadhi ya vijana wanawachochea wenzao kupigana.

ha ha hahaha
 
Mponjoli,

Kwi kwi kwi, sasa si nilikuwa na Mwakalinga kijijini na baadaye nikarudi mjini?

Dah...Mkuu Mtz,

Inaonekana ulimbana sana Mwakalinga.....kwa mtindo huu, tukiambiwa Mwakalinga alipofika AR alienda mara moja pale Mawingu Club kakamata TOTOs la Meru....mkuu unaweza elezea yote yaliyojiri kwa bed pamoja na kuielezea nini ya shori yule... (joke)...hahahah!
 

Kwa hiyo na wewe unavyompigia debe Kikwete kuwa apewe uongozi mwaka 2010 bila kujali kuwa Kikwete amekuwa serikalini na kwenye siasa kwa miaka zaidi ya 20 unatumia mawazo mgando?
 
Kwa hiyo na wewe unavyompigia debe Kikwete kuwa apewe uongozi mwaka 2010 bila kujali kuwa Kikwete amekuwa serikalini na kwenye siasa kwa miaka zaidi ya 20 unatumia mawazo mgando?


Mwafrika;

Swali zuri. Unapomaliza shule(yoyote) unaanza kazi ya chini, other things remain constant unapanda ngazi kwa ngazi, mpaka ufikie kuwa president wa kampuni inaweza kuchukua hata miaka 20. Hapo sina tatizo na wewe. Ndo issue kama ya Kikwete.

Dr miaka kumi inatosha, kwakweli tuweni na tamaduni ya kuachiana madaraka, hii ya akina Mugabe sio sahihi.

Mi nimeangalia kwa upana sio kwa issue hii ya Mwakyembe vs Mwakalinga
 


Pumba!
 

Naona sasa zimeanza kurushwa namba za kuonesha uwezo wa kifedha wa Mwakalinga. Kama Mwakalinga ana pesa hizi zote na miradi yote hii, je ni kwa nini anataka kuwa mbunge wa Kyela?

Kwa nini asisaidie tu kama kina Bill Gates wanavyofanya bila kuingia kwenye siasa?

Mtanzania una jibu? Nafasi yako hapa ya kuelezea sera na sababu ya kutaka kuwa mbunge wa Kyela. Nimekurushia bonge ya soft question la ki-charlie Rose.
 

Bado hujaweka tofauti yoyote kati ya Kikwete (ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10) ambaye amekuwa kiongozi wa ngazi ya juu kwa muda wowote kuruhusiwa kubaki madarakani lakini wazee wenzake (kina Mwakyembe?) wanaambiwa watoke.

Nataka kusoma sababu na/au tofauti ya hivyo viwili.
 


Sawa mzee. Kikwete miaka kumi Uwaziri wa mambo ya nje. Enough.

Miaka kumi urais. Enough.

Nilichosema kama unapanda ngazi au unashikilia vyeo tofauti ni sawa, sio kuwa kwenye cheo kimoja your entire life.

Umenielewa mkuu?
 

Katika waraka(mwongozo) wa Mwakipesile kwa wanakyela, unaotumika kumnadi Mwakalinga kuna mambo ishirini yanayotajwa(waraka ambao umewekwa hapa JF na mdau mmoja) kwa ajili ya kuwaongoza wanakyela kumchagua bw.Mwakalinga.

Kusaidia kupeleka walimu wa sekondari kyela wakati akiwa anasoma chuo kikuu wakati Mwakyembe akiwa mhadhiri hakutoa msaada wowote.
Waraka aka mwongozo unasema Mwakyembe amewekeza dar, kajenga nyumba kubwa kuzidi hata mafisadi, na wewe hapa tena unarudia maneno yale yale ya mwongozo wa mwakipesile.

Katika hali kama hii utawezaje kutuaminisha kwamba bw.Mwakalinga hayuko kambi moja na mwakipesile?
unajua hata kama mwaka 2005 mwakalinga na mwakyembe walikuwa kambi moja sio suala la ajabu mwaka 2010 mwakalinga na mwakipesile kuwa kambi moja kwakuwa tayari mwakalinga hayuko pamoja na mwakyembe.
kwangu mimi hiyo siyo hoja ya msingi ya kuwafanya mwakipesile na mwakalinga wasishirikiane.
 
Masanilo;

Wanachama humu wataamua nani ana hoja au vihoja.
 
Sawa mzee. Kikwete miaka kumi Uwaziri wa mambo ya nje. Enough.

Miaka kumi urais. Enough.

Nilichosema kama unapanda ngazi au unashikilia vyeo tofauti ni sawa, sio kuwa kwenye cheo kimoja your entire life.

Umenielewa mkuu?

kwa logic hii, kwa nini isiwe kwamba Mwakyembe naye apewe miaka 10 Kyela? Kwa nini unatumia different standard?
 

Safi kabisa Mwita,

Kwa kuongezea tu, kwa nini Mwakalinga na wapambe zake watumie msaada alioutoa kwa wana Kyela (kama kweli aliutoa bila strings attached) kuwa ni chambo cha kuwataka watu wa Kyela kumpa kula (kura)?

Hii ni blackmail au nini?
 
kwa logic hii, kwa nini isiwe kwamba Mwakyembe naye apewe miaka 10 Kyela? Kwa nini unatumia different standard?

East Africa + Bunge la Muungano ni miaka mingapi?

Au utasema ni vyeo tofauti? OK.

Naomba niulize wakati nakubaliana na wewe kuwa ni vyeo tofauti.

Mwakyembe ametangaza kugombea tena Kyela?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…