- Mkuu ninakusikia sana, ila I am looking forward kuona mijadala yenye masilahi kwa wananchi wa jimbo la Kyela, ninasubiri kusikia vision ya George, maana ya DK ninaifahamu tayari katika miaka kumi ya ubunge wake toka EAC, mpaka huko Kyela hasa zaidi taifa. Ninaiheshimu sana kazi yake kwa taifa letu, lakini lazima niwe mkweli sijui chochote kuhusu kazi yake jimboni, zaidi ya kuwaisikiliza sana hao maluteni wake, wawili.
Hapa tuko pamoja
- George, itafika wakati itabidi aseme kujibu maswali muhimu kwamba ni kwa nini anataka ubunge wa Kyela na sio jimbo lingine?, kwa nini anataka kumtoa mbunge shujaa wa taifa kama DK? kwa nini anafikiri anaweza kuwapelekea Kyela mazuri kuliko mbunge wao wa sasa? Je mbunge wa sasa amefanya mangapi mazuri na mangapi mabaya? Kama mbunge shujaa kama DK ameshindwa yeye atawezaje? Na maswali mengine mengi muhimu kwa taifa pia, ni majibu ya maswali kama haya ndio yatawasadiai wananchi Kyela na sisi wengine, kuliko hizi lows ninaziona humu.
Nadhani hii kazi alishaianza hapa kwa muda sasa kwa kutumia ID zake za JF (ambazo inaonekana kama ni nyingi) au kutumia wasemaji wake.
- Kampeni hazijaanza, lakini hii tunaita part gazeti au trailer imeshaanza, na heshima kwa George kwa kuli-freeze taifa na JF for almost a week sasa, saafi sana na ataingia kwenye vitabu vya historia ya taifa kwa ujasiri wa kusimama na kusimamia principles. Ndio maana huko nyuma nilisema kwamba huu uchaguzi utakua wa Century na watakaofaidika ni wananchi wa Kyela hivi vichwa viwili vikitwangana.
Hapa tuko pamoja ... huu ni uchaguzi wa karne. Upande mmoja kuna mafisadi woote kuanzia Lowasa na Mwakipesile, upande mwingine kuna Mwakyembe, na wakimaliza kupata mgombea wao, watakutana na mtu ambaye upinzani watamsimamisha huko Kyela.
- La George kuwa fisadi, bado ninalikataa sijaona sababu ya msingi, kama ni kukutana alianza kukutana na the right hand man wa DK, tena aliyemfuata London, silioni hili likipigiwa kelele hapa, Mwakipesile hamjui George, lakini yes ni adui namba moja wa DK, sheria haimzuii kumshabikia George na hata kumfanyia kampeni on his own ili kushindana na adui wake hilo linaeleweka, kwamba eti George anahusika directly na Mwakipesile au Lowassa, nimewauliza sana wale watu wa DK, ambao binafsi ninawaaminia sana inapokuja masuala ya kampeni za DK na George huko Kyela, infact mmojawao alinihakikishia kuwa George akimshinda mtu wake DK, basi yeye atahamia Malawi na kuomba uraia huko, now that is deep royalty kwa kiongozi, as opposed na hizi blah blah humu,
Haya ni maoni yako binafsi na sina sababu yoyote ya kuyachukulia kama facts.
- Alisema alisikia kuwa George anajenga bara bara ya lami Kyela kwa kusaidiwa na mafisadi, hasa Lowassa lakini alikwenda haraka sana huko na kuhakikisha kwamba sio kweli, na nimamumini sana huyu aliyeniambia haya, sasa hawa wawili wakiniambia kwamba George ameanza kuwa fisadi basi wala sina sababu ya kumuuliza George kama ni kweli au uongo, hawa ni watu tunaheshimiana sana, so far wamesema mengi mazuri na mabaya ya George as a candidate wa jimbo lao, lakini la kushirikiana na mafisadi hawajalisema na ninawaamini sana hasa inapokuja interest ya uongozi wa
DK huko jimboni.
Ha ha ha hah,
hii ya barabara ya lami imenivunja mbavu kabisaaa.
- Ushauri wangu kwa George, ni do not panic maana sasa umeingia siasa za taifa na hasa kwa kumgusa shujaaa wa taifa, haya ya JF ni madogo sana kulinganisha na ya mbele zaidi, hizi za JF ni za kawaida ingawa kuna mengine ni mazuri sana kwake kuyakariri, hasa ule ushauri wa Dilunga kwamba ifike time George ndiye awe the owner wa message yake na awe muangalifu sana na vibaka. Huna sababu yoyote ya kuhangaika kujibu hizi shutuma zisizo na kichwa wala miguu, be yourself watu ni watu tu maana ukiingalia vizuri sana hii thread utajionea mwenyewe some of the so called you "friends" wakivua ngozi zao rasmi, ndio maana hata viongozi wetu huteseka sana na siasa zetu Tanzania maana this is how we are, lakini yasikusumbue yachukulie kama changamoto.
Naona ushauri wako umefuatwa kabisaaaa.
Miwsho I am looking forward kuiona na binafsi kushiriki mijadala serious kwa ajili ya wananchi wa Kyela, pindi tu hizi blah blah zikiisha, zitaisha tu karibuni si unajua sisi wabongo na kipya kinyemi, soon tuta get down to serious business, otherwise ninamtakia safari njema kurudi "nyumbani" na pia ninamuombea sana kwa Mungu DK, amsalimishe na majaribu ya waovu wasiomtakia mema na ninawaombea sana wananchi wa Kyela kuwa waangalifu katika kutafakari hii situation, ambayo kama hawako makini itawaletea kimbembe sana, maana this thing is for real.
Mjadala mwema wananchi wenzangu wa JF, ila hapa ninaweka kalamu chini na huu mjadala. Na JF idumu where we dare! nafikiri hata George atajionea mwenyewe humu nyani alivyopigwa giladi, tena bila kumuangalia usoni ikiwa mchana kweupeee! I love JF!
Respect.
FMEs!
Respect kwako pia. George kama ameingia kwenye siasa ategemee kupata maswali na scrutiny ambayo wanasiasa wote bongo wanapewa. Na kwa vile anaingia CCM (chama ambacho mi nakihesabu kama cha mafisadi) basi George ameingia kwenye kundi la mafisadi kwa hiyo ategemee the same standard against mafisadi toka kwa wana JF.
Respect again na unakaribishwa muda wowote kwani mimi nitakuwa hapa hadi kieleweke.