Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Eti cheupe dawa wako ulimlipia ngomba 35...acha urongo bana

Mtoto guu guu, paja paja, hata kovu hana.

Siyo kama wako, makovu kibao. Hasa lile na mguuni alimwagikiwa UJI W MOTO.

Kama umechukizwa na mie kuwa na mke "Cheupe dawa", nenda Dampo. Walau na wewe utagundua kuna wengine umewapita.
 
..binafsi nataka kujua kwanini Mwakalinga anafikiri atafaa kuwa Mbunge na mwakilishi wa wana Kyela.

..tunajua kwamba Mwakalinga ni msomi, but so is Dr.Mwakyembe.

..tunajua kwamba Mwakalinga inaipenda Kyela ame-invest huko etc etc, lakini sidhani kama kuna mtu anaweza kudai Dr haipendi Kyela.

..hatuna taarifa kwamba Mwakalinga ni fisadi. Dr naye vilevile anasifika taifa zima kwa kuupinga ufisadi.

..mtizamo wa Mwakalinga kuhusu Kyela ni upi?

..kwanini anafikiri wana Kyela wanapaswa kubadilisha uongozi ktk nafasi ya Mbunge?

..ni kitu gani ambacho anadhani anaweza ku-offer, tofauti na Dr.Mwakyembe,katika nafasi ya ubunge, ili kusukuma mbele zaidi maendeleo ya Kyela?
 
Mtoto guu guu, paja paja, hata kovu hana.

Siyo kama wako, makovu kibao. Hasa lile na mguuni alimwagikiwa UJI W MOTO.

Kama umechukizwa na mie kuwa na mke "Cheupe dawa", nenda Dampo. Walau na wewe utagundua kuna wengine umewapita.


Achana nao hawana hoja, zimeisha.
 
Nimekusoma na kukuelewa mkuu...Pa1
 
Hivi mnajua kanda2 ni nani?
Hivi mnajua Mwafrika ni nani?
Hivi Mwanakijiji mbona hachangii thread hii?

JF wanafiki wakubwa, mnakuja kumchafua mwana JF mwenzenu eti laptop kumbe mmepanga?

Kama mnatofauti na Mwakalinga kwa nini msitoe hoja kwa usernames zenu za kawaida?

Mnatengeneza strategy ya kuandika absurd things ili Mwakalinga aonekane hafai?

Futeni hii post lakini ukweli tumeugundua, Mwanakijiji kua kaka! Hata Mwakalinga naamini anajua ukweli huu.
 
Dah,mkuu mbona hivi????,yaani umeamua kutuwakia na kutuita wana Jf wanafiki wakubwa kisa Mwakalinga...Kama ulitaka kumfikishia ujumbe Mwanakijiji ungemPM tu badala ya kuwahusisha wanaJF wote na kuwaita wanafiki.....Tutake Radhi mkuu
 
As long as yuko hapa hapa jamvini na aje na majibu basi. Hatutaki wapambe kumjibia.
 
Mwakalinga is a weak character ndo maana hata wapambe wake wanaanza matusi.....wanakuja na hoja zisizouzika hapa JF.....Mwakyembe yuko imara na taifa zima tunamtegemea kwa kile ambacho hata milima inakiona alichokifanyia taifa letu. Huyu pandikizi la ufisadi hatakuwa na kipya zaidi ya kujilimbikizia mali kwa hadithi za alinacha....akagombee Zimbabwe patamfaa sana

Masa
 


Kiroja hiki.....nasema Mwakalinga hafai hafai kabisa na wapiga debe wake wamefulia msome alichoondika huyu Engineer wa Dar Tech.... tuombe msamaha mkuu uonyeshe ustaarabu basi kama sisi wanafiki wewe na Mwakalinga ni akina nani?
 

We Engineer.. mbona unaniingiza katika mambo haya. Nimeamua kutochangia kwa sababu si lazima nichangie. Marafiki wa wawili wako kwenye mchakato wa kugombea nafasi moja hivyo hekima inanilazimisha kukaa pembeni na kuwaacha wagongane wenyewe huko huko. Lakini zaidi sana sijui mambo mengi kuhusu Kyela au siasa za Kyela hivyo nikianza kuchangia nitajifanya mjuaji wa vitu nisivyojua na hivyo naweza kuingia biases zangu na hivyo kutosaidia mjadala.

Niwie radhi kama ungependa nichangie. Tafadhali usinihusishe na mjadala huu. Mimi simo. Wakati ukifika wa kutoa maoni nitafanya hivyo bila kuomba kibali kwa mtu yeyote au baraka zake.
 

Ndio maana wapata wivu kwa mwenzao ambaye kaishi huko bila kubeba maboksi na kuamua kurudi nyumbani kulisaidia taifa lake.Lazima tukubali tu kuwa dunia haiko fair kihivyo... kuna wengine wana courage ambazo wengi wamekosa.Kwangu mimi kwa Mwakalinga kushinda au kushindwa kwenye uchaguzi 2010 sio issue kubwa,Kwangu ishu ni kuwa ameweza kuwa na guts za kujaribu yale ambayo wengi wetu wameogopa kufanya.
 
Hakuna na kushangaza sana kwa huyo Mwakalinga kukaa ulaya sio kuchukua Ubunge.Je anaubavu wa kuleta mageuzi ya kweli?Leadership is not a tilte is but action
 

KG

Elias Mwanjala alikuwa jamaa yake Mwakyembe na sasa hawana ujamaa kwa sababu ya Elias kuamua kumsaliti mwakyembe mchana kweupe na kwenda kujiunga na kambi ya Mwakipesile( hapa nina maana kujiunga na kambi hiyo kwa nia ya kumharibia mwakyembe)

Ni kweli elias alikuwa kwenye kambi ya Mwakyembe na alifanya kazi kubwa lakini sio kufika kusema kuwa asingekuwepo basi mwakyembe angeshindwa. Pia uwepo wa Elias kwenye kambi ya Mwakyembe ulikuwa ni risk kubwa sana hasa ukizingatia kuwa ni mtu anayeweza kuharibu muda wowote, hana msimamo na anapendwa kuabudiwa sana. Guess what kabla hata ya uchaguzi kufanyika alisha gombana na dada yake mwakyembe na ndiyo mojawapo ya kisa cha kuhamia kwenye kambi ya kumpinga mwakyembe sababu nyingine ilikuwa ni mategemeo yake kuwa mwakyembe atapata uwaziri hivyo angefaidi. Kumbuka kuwa lilikuwa ni tegemeo la kila mtu kuwa angepewa uwaziri. (kutokupewa ni moja ya vioja vikubwa sana kwa nchi hii kwa mtizamo wangu). Na sababu nyingine ya kuanza kumchukia eti ni kwamba mwakyembe anajitapa kuwa ni ukoo wa chief du! hii kali unapoanza kumlaum prince William kwa kuzaliwa kwenye familia ya kifalme sijui ulitaka afanye nini?

Nilipenda sana style ya mwakyembe aliyoitumia kudeal na issue ya Elias nayo ilikuwa ni kumignore completely na hapo ndipo Elias alipoanza kutapatapa sana. kumbuka kuwa nimekuambia mwanzo kuwa huyu jamaa anapendwa kuabudiwa na alichotegemea ilikuwa ni kwamba pindi mwakyembe atakapojua kuwa amejiunga na kambi ya kumharibu basi atapigiwa magoti na kuombwa kurudi kwa kuhisi kuwa yeye alifanya mchango mkubwa sana kwenye campaign ya mwakyembe. Yote hayo hayakutokea na ndipo alipoanza kuogopa kivuri chake kila kinachomtokea basi yeye anapelekea kuwa ni mkono wa mwakyembe.

Moja ya kioja alichotaka kukifanya ilikuwa ni kugombea ubunge yeye mwenyewe na akaanza kampeni na vijisenti vyake vimeliwa sana tu na wanjanja hapo kyela. kampeni yake ilifika mwisho pale baba yake mzee Mwanjala alipomwita na kumwambia " nimesikia kuwa unapita pita mitaani ukitangaza kuwa unataka kugombea ubunge nakwambia kuwa wewe pamoja na huyo rafiki yako (mwakalinga) mpeleke matumbo yenu huko huko msituletee ujinga wenu huku". Ukishaambiwa na baba yako maneno kama hayo basi kama uko fit kampeni inakuwa imeisha hapo hapo na ndipo Eliasi alipotokomeza kampeni yake. Big up mzee mwanjala kwa kuamua kusimamia ukweli na kuusema bila ya kuogopa, kumbuka kuwa huyu ndiye mtoto aliye na uwezo kuliko wote lakini akaambiwa ukweli na ukweli ukamweka huru.

sasa ninaposikia kuwa jamaa analalamika kuwa amehamishwa kwenye nyumba na kusema kuwa Mwakyembe kuwa ndiye muhusika watu msiomjua mnaweza kuanza kurusha mawe kwa mwakyembe kumbe hamna lolote, kapata nyumba kwa deal na ataondoka kwenye nyumba kwa deal.

Kitu kimoja amabchio ni kikubwa sana alichonacho Elias ni kwamba jamaa ni mtu wa msaada sana tofauti na watu wengi wanaotoka kyela pamoja na Mwakyembe mwenyewe asiye na msaada ( family affairs) kwa hilo Mungu lazima atamzidishia tu kwa sababu kanuni za mungu ziko pale pale
 

Kama huwezi kusaidia familia utawezaje kusaidia wananchi wasio ndugu zako?

Asante Shalom kwa vipande vyako na kuwaelezea kambi ya Dr hilo.

Charity inaanzia NYUMBANI
 

Shalom,

Nilikuwa nakuona kuwa wewe ni KASUKU wa Mwakyembe. Ila kama utakuwa unachangia maneno namna hii, basi mkulu Yesu atakuwa nawe. Mie mwenyewe nilishasema wazi kabisa kuwa "au ntamsifia Mwakalinga na kama kuna sehemu kaenda kombo, basi ntamwandikia yeye moja kwa moja na hapa nikifika nikute wanamsulubu, basi ntakula bati.

Mkuu nashukuru sana kufahamu ukweli wa Mwakyembe wa upande mwingine kuwa "Mwakyembe hana msaada kwa ndugu zake". Sasa sijui JIRANI zake na watu wa mbali inakuwaje?
 
 

Mbona hasira je ulikutana na Lowassa Arusha na uwe unauhakika kwani waijua vizuri JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…