NYEPESI NYEPESI.
Wana ukumbi, leo nilipata kuongea na jamaa yake Mwakyembe, ndg Elias Mwanjala ambaye alikuwa mpiga kampeni mkubwa sana 2005 na alitumia pesa zake nyingi kumsaidia Mwakyembe kupata kiti hicho.
Elias anasema kuwa Mwakyembe amemfanyia mambo mabaya sana na baado anaendelea kumnyanyasa.
Anasema alipata nyumba ya National Housing Mikocheni na ndiko anakoishi, basi Mwakyembe alikwenda kumwambia Sitta ili wamnyang'anye ile nyumba.
Anasema naye Sitta akakubali azimio hilo na jamaa ameletewa notice ya kuondoka ile nyumba haraka kwa sababu hasizozijua, na alipofuatilia sana akapata habari kuwa hiyo nyumba anatakiwa kuhamia Sitta.
Anasema Mwakyembe amemwambia kuwa amesikia tetesi kuwa anamuunga mkono Mwakalinga na atamuonyesha lasivyo awaambie wapambe wake wampe kura yeye.
Elias amekimbilia Mahakamani kupinga hiyo notice ambayo haina sababu yoyote ya msingi zaidi ni uonevu tu.
Haya huyo ndiye mpinga ufisadi, haya ni zaidi ya ufisadi.
Kgwamaka