Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Sikonge,
Utani hapa ndio penyewe, isipokuwa mimi watani zangu ni akina kalumanzila na akina omutwale a.k.a baba koku.
Kama unataka kuhamisha utani kutoka kwa wakwere kuja kwetu, au unataka kuongeza listi ya watani, karibu sana tarime.
Kwa kifupi tu ni kwamba nimekusikia sana mkuu, huyo dada yangu ndiye kasababisha nicheke. Maana najiuliza, pamoja na hiyo mimacho iliyomtoka, hivi Sikonge ulimpendea nini?au unafikiri hatujui kwamba umezaa nae?
kaazi kwelikweli.
Sawa mkuu. Umenichekesha kwamba eti huyo ni mke wangu.
Hebu fikiri unaota umefukuzwa na unapoamka, unagundua kumbe ilikuwa ndoto na ghafla unamwangalia mkeo anayekushangaa "kulikoni mume wangu?" na lahaula unapambana na macho. Hapohapo wapoteza fahamu.
Mkuu, nafahamu kuwa naingilia kazi ya akina "Mugambire muzungu SITOPU". Ila ndiyo raha ya mitandao. Ila kwa taarifa yako ni kuwa:
Wanyamwezi hatuna utani na Wakwere. Wakwere wanafahamu kuwa sisi ni BABA zao na hivyo huwa hawawezi kututania. Kimila ilitakiwa niende kumwambia Kikwete fanya hiki na kila na ingebidi atii. Ila leo hizo mila zimekufa, Mkwere anatesa.