Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Amesema barabara zilifungwa kitu ambacho sio kweli.Hakukuwa na barabra iliyofungwa.Hizo ndizo taarifa za kupikwa.
mkuu tutaaminije kuwa barabara haikufungwa? tupe uhakikisho sio maneno matupu......
 
Piga simu hiyo chini utajibiwa kama barabara ya Kyela-Tukuyu kupitia CCM makao Makuu ilifanywa nini kwa sababu ya mkutano huo!

Na kuhusu siku huwa nachanganya sana na TZ na huku nilipo Kabul!!

Mimi nilidhani umeshuhudia mwenyewe kwa macho yako, kumbe umesimuliwa!!! Jamani angalieni msiwe mnatulisha kasa kwa sababu zenu za kisiasa. Mwisho mtaanza kushusha hadhi ya JF.

Hivi hamjui kwamba JF ni chanzo kikubwa cha news nyeti za kitaifa? Ukiona mpaka magazeti makini kama Raia Mwema, ThisDay na Kulikoni wanakuja kuchota news hapa, hiyo ni indication kwamba JF iko makini na inaweza kutumika kama chanzo cha habari cha kuaminika.

Kwa hiyo mkituletea news hapa jamvini punguzeni ushabiki wenu wa kisiasa ili tupate habari sahihi. Sasa mtu uko mbali na eneo la tukio bado unakubali kwamba barabara zilifungwa, ukiombwa ushahidi huna.

Hizi siasa za Mwakyembe vs Mwakalinga naomba zisitushushie hadhi ya JF, after all kampeni za kura za maoni hazijaanza. Sasa huu ushabiki sioni hata kama una maana yoyote.
 
OMBI MAALUM KWA MODS

Mimi naomba kwa wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu uwawekee jukwaa maalum wale wote ambao wameshaingia katika kampeni za mapema za uchaguzi mkuu wa 2010.
Tafadhali kama fanya hima kushughulikia ombi langu kwani joto la kampeni limeanza kupanda sasa.
sio kampeni za 2010, alienda jimboni kwake kuongea na wapiga kura wake kwani tokea apate ajali walikuwa hawajamuona.
 
Siasa za Kyela ukitaka kuzifuatilia zinatia kinyaa na kichefu chefu huu si ushindani wa demokrasia.
 
Mimi nilidhani umeshuhudia mwenyewe kwa macho yako, kumbe umesimuliwa!!! Jamani angalieni msiwe mnatulisha kasa kwa sababu zenu za kisiasa. Mwisho mtaanza kushusha hadhi ya JF.

Hivi hamjui kwamba JF ni chanzo kikubwa cha news nyeti za kitaifa? Ukiona mpaka magazeti makini kama Raia Mwema, ThisDay na Kulikoni wanakuja kuchota news hapa, hiyo ni indication kwamba JF iko makini na inaweza kutumika kama chanzo cha habari cha kuaminika.

Kwa hiyo mkituletea news hapa jamvini punguzeni ushabiki wenu wa kisiasa ili tupate habari sahihi. Sasa mtu uko mbali na eneo la tukio bado unakubali kwamba barabara zilifungwa, ukiombwa ushahidi huna.

Hizi siasa za Mwakyembe vs Mwakalinga naomba zisitushushie hadhi ya JF, after all kampeni za kura za maoni hazijaanza. Sasa huu ushabiki sioni hata kama una maana yoyote.
.

Heshima yako Mkuu wangu Keil.
Watu wanajaribu kushusha heshima ya jf kutokana na habari za kupikwa.

Kama ulisimuliwa basi twambie ulisimuliwa.

Mwakyembe aliingia hapa kyela Asubuhi,sasa iweje barabara ya kutoka Tukuyu Ifungwe?

Wahusika tunaomba mufunge mjadala huu.
 
Mkuu Next Level.
Kweli kazi ipo.

Kama unashindwa kutambua ujumbe wangu na ule wa Malafyale,nafikiri mwalimu wako alikuwa na kazi ya ziada.

Malafyale anasema Mheshimiwa alifanya mkutano tarehe 08/08 siku ya jumamosi kitu ambacho ni uzushi.Ukweli ni kwamba alifanya mkutano wake siku ya jumapili tarehe 09/08.
Amesema barabara zilifungwa kitu ambacho sio kweli.Hakukuwa na barabra iliyofungwa.Hizo ndizo taarifa za kupikwa.

Samwel kuhusu kujichanganya kwa siku ni issue ndogo sana hapa,issue kubwa hapa ni kuwaeleza wana jf kuwa Mwakyembe bado ana wafuasi wengi sana Kyela mjini na imedhihirika hivyo.

Cha ajabu Samwel hukanushi kama watu walikuwa wengi sana,na kama walikuwa wengi sana iweje barabara ile ya Kyela-Tky isifungwe ikiwa ina pita pale walipofanyia mkutano?

Iweje hukanushi agizo la wana Kyela mjini kuomba Mwakyembe asisumbuliwe na aachwe afanye kazi kwa ufanisi?iweje usikanushe kuhusu kupewa jina jipya la Obama?Mbona hukanushi hata habari za kugawa nyama?

Habari haiwi ya kupikwa kwa kutaja tu jumamosi badala ya jumapili,na hii imetokana na revolution ya sayari huko jioni huku asubuhi!

Tueleze unahisi kwa makadirio watu wangapi walihudhuria mkutano ule?na kwako wewe watu wengi sana huwa wangapi?
 
Hata Mrema alikuwa nao wafuasi wengi tu kwenye mikutano yake 1995. Barabara kufungwa ni jambo la kawaida tu hata mchiriku unaweza ukafunga barabara! Msitake kumbwetesha shujaa wenu Mwakyembe na visifa vya hovyohovyo kama hivi.
 
Ktk historia ya siasa za Kyela,haujapata kutokea umati wa watu wengi ukiambatana na kufungwa kwa baadhi ya barabara kwa masuala ya usalama;kama ulivyojitekeza jumamosi ya tarehe 8/8/2009 kumsikiliza hatimaye kumpa jina jipya mbunge wao Dr Mwakyembe.Umati huo kwa kauli moja hatimaye ukakubaliana kuwa Dr Mwakyembe akiwa kwenye jimbo lake la Kyela aitwe "Obama"

Mkutano huo uliofanyika ktk viwanja vya CCM-Kyela mjini ulipitisha kwa kauli moja kuwa mwana Kyela yeyote atakayejitokeza kumpinga Mwakyembe ktk uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM na ule wa ubunge aulizwe ataifanyia nini kipya Kyela ambacho Mwakyembe hajakifanya?!Walikumbusha kuwa chini ya miaka 4 tu ya ubunge wa Mwakyembe;kila kata ina sekondari yake,umeme Kyela ni wa uhakika,maji safi na salama yapo,miundo-mbinu hasa madaraja yamejengwa,na huduma za afya hasa vijijini zimeimarishwa!

Katika mkutano huu,vijana wa CCM wa Kyela mjini walimueleza Mbunge Mwakyembe kuwa wamekasirishwa sana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaolikodela macho jimbo hilo ukiambatana ushawishi wa utoaji wa na vitu kama vile nyama ya ng'ombe kama hadaa kwa wananchi.

Mwakyembe mwenyewe akihutubia huku kasimama kwenye meza iliyotandikwa bendera ya Taifa tena akilindwa na wazee maarufu wa mji wa Kyela akiwemo mzee Mboka,Mzee Hasab Baba,Mzee Mwakanyika na wengine wengi aliwashukuru sana wakazi wa Kyela kwa kumuunga mkono na akahaidi kuwatumikia kwa moyo mkunjufu zaidi!

Yaliyoelezwa kwenye mkutan huo ni mengi sana,na kama una taka kuyajua kwa ufanisi basi piga simu hii ili uelezwe zaidi 0784 370 227

Anastahili heshima tena zaidi ya hapo toka kwa watanzania wote wazalendo na si kwa Kyela tuuuuu. Mwakyembe, hongera baba!!!
 
Blah blah tu
tu mara

George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!

Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!

Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".
 
Siasa za Kyela bana!
Si za kyela tu, hizo ndizo siasa tutakazoshuhudia wakati wa mapambano ya wanapinga na wanaunga mkono ufisadi. Si unamuona hata makondoro naye anatoa statement kila siku!!!
 
Samwel kuhusu kujichanganya kwa siku ni issue ndogo sana hapa,issue kubwa hapa ni kuwaeleza wana jf kuwa Mwakyembe bado ana wafuasi wengi sana Kyela mjini na imedhihirika hivyo.

Cha ajabu Samwel hukanushi kama watu walikuwa wengi sana,na kama walikuwa wengi sana iweje barabara ile ya Kyela-Tky isifungwe ikiwa ina pita pale walipofanyia mkutano?

Iweje hukanushi agizo la wana Kyela mjini kuomba Mwakyembe asisumbuliwe na aachwe afanye kazi kwa ufanisi?iweje usikanushe kuhusu kupewa jina jipya la Obama?Mbona hukanushi hata habari za kugawa nyama?

Habari haiwi ya kupikwa kwa kutaja tu jumamosi badala ya jumapili,na hii imetokana na revolution ya sayari huko jioni huku asubuhi!

Tueleze unahisi kwa makadirio watu wangapi walihudhuria mkutano ule?na kwako wewe watu wengi sana huwa wangapi?
.

Mkuu malafyale,

Sijajua upeo wako wa kufikiri unao kiasi gani.
Kwanza nikuulize maswali rahisi sana na ninaomba nikujibu mimi mwenyewe.
Neno Ubama linatamka sana na kundi gani hapa kyela?

Jibu ni watoto wa kijiweni ambao wengi wao sio kipimo cha kwamba mbunge anapendwa.Ni washabiki na hata hawapigi kura.Sidhani kama Baba yako kule kijijini Ngonga ambaye ni mpiga kura mzuri anaweza kumwita mtu ni Obama.

Siku mwakalinga atakapokuja hapa na kuruhusiwa kampeni,haohao watoto wakijiweni watamwita Musa,kumaanisha ni mkombozi wao.Hiyo ndiyo tabia ya mtoto wa kijiweni.

Hayo ni maneno ya vijiweni ambayo kwa mtu mwelewa hawezi ata kasema chochote.

Mwakyembe alihutubia kwa ustaraabu mkubwa sana na kumaliza hutuba yake kwa muda mfupi sana.Baadaye aliporuhusu maswali na ndipo hao hao watoto wa kijiweni walijitokeza na kumtolea sifa badala ya kuuliza maswali.

Kwamba kuna watu wanalitaka jimbo la kyela ndani ya ccm na sisi hatuwataki,Je hilo ni swali au ni statement?

Malafyale tumia ulewa wako vizuri badala ya kupotosha taarifa za watu.

Kumbuka kuwa wewe ndiye ulikuwa wa kwanza kuanzisha topic ya mwakalinga mapema kuwa yuko kyela na ameanza kampeni kitu ambacho ulikipika bila ushahidi wowote.Na wakati huo mwakalinga alikuwa ajafika hapa kyela.Kwa vile tu uliambiwa kuwa mwakalinga yuko Dar na anakuja kyela kwa ajili kuongea na wana kyela na kuonyesha nia ya kuwa mmoja wa wagombea ubunge 2010,bila utafiti wowote,ukazirusha hewani.Ni vizuri huyu mtu wako wa kijiweni akawa na uhakika sana na taarifa zake la sivyo unajishushia hadhi yako mzee

Watu kama wewe malayale ndiyo mnajaribu kuishusha hadhi ya jf.Punguza kuandika taarifa za kijweni ambazo muda mwingi zinakuwa ni uzushi.
 
Blah blah tu
tu mara

George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!

Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!

Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".

Ni Mwakipesile mkuu
 
Kweli kazi ipo.
Huko Kyela sio?

Kama unashindwa kutambua ujumbe wangu na ule wa Malafyale,nafikiri mwalimu wako alikuwa na kazi ya ziada.
Unataka ni utambue ujumbe wenu kivipi mkuu? Nyie mnaleta mipasho yenu ya huko Kyela, halafu unapobanwa useme wewe kilichojiri huko.....unaniletea hadithi za mwalimu wangu! Unajua katika maisha yangu nilishawahi fundishwa na Mwalimu?

Mkuu mimi si Mkyela but mkimwaga upupu wenu hapa tunaushughulikia ipasavyo. Na wewe nilichokuomba ni utuletea taarifa ambayo ni unbiased kutoka eneo la tukio...si ngonjera zenu sisizo na vichwa wala miguu!

Malafyale anasema Mheshimiwa alifanya mkutano tarehe 08/08 siku ya jumamosi kitu ambacho ni uzushi.Ukweli ni kwamba alifanya mkutano wake siku ya jumapili tarehe 09/08.
Amesema barabara zilifungwa kitu ambacho sio kweli.Hakukuwa na barabra iliyofungwa.Hizo ndizo taarifa za kupikwa
.

Kukosea kunukuu tarehe kwenye taarifa muhimu kweli kunapelekea habari yote kuitwa ya kizushi mkuu? Kama una nia njema na ni muungwana mbona hujerekebisha post yako baada ya mtoa mada kusahihisha hapo juu?

Pili, kufungwa barabara is it a big deal to you mkuu? or what is the implication ya kufungwa barabara kwako wewe?
 
kama upo TZ nunua tanzania daima au nipashe hii habari imetoka sio huzushi kweli huyu mtu ni OBAMA
.

Magreth.
Tangu mwanzo tulisema amekuja na wandishi wa watano.Ni wale wa magazeti ya Mengi,Tanzania Daima na Majira.Hata Mc wa siku hiyo alikuwa Richard Kilumbu ambaye ni mwandishi wa gazeti la tanzania daima.

Mwakyembe amekuwa akifadhiliwa sana na shemeji yake (mengi) na kila mara anaongozana na wandishi wa ippmedia.

Kumbuka kuwa mengi ni mmoja kati ya watu wanaochunguzwa na pccb kwa ajili ya ufisadi.

Detail kuhusu hili ziliwakiliswa na Rostam Aziz (MB)
 
Huko Kyela sio?

Unataka ni utambua ujumbe wenu kivipi mkuu? Nyie mnaleta mipasho yenu ya huko Kyela, halafu unapobanwa useme wewe kilichojiri huko.....unaniletea hadithi za mwalimu wangu! Unajua katika maisha yangu nilishawahi fundishwa na Mwalimu?

Mkuu mimi si Mkyela but mkimwaga upupu wenu hapa tunaushughulikia ipasavyo. Na wewe nilichokuomba ni utuletea taarifa ambayo ni unbiased kutoka eneo la tukio...si ngonjera zenu sisizo na vichwa wala miguu!

.

Kukosea kunukuu tarehe kwenye taarifa muhimu kweli kunapelekea habari yote kuitwa ya kizushi mkuu? Kama una nia njema na ni muungwana mbona hujerekebisha post yako baada ya mtoa mada kusahihisha hapo juu?

Pili, kufungwa barabara is it a big deal to you mkuu? or what is the implication ya kufungwa barabara kwako wewe?
.

msg sent
 
Ktk historia ya siasa za Kyela,haujapata kutokea umati wa watu wengi ukiambatana na kufungwa kwa baadhi ya barabara kwa masuala ya usalama;kama ulivyojitekeza jumamosi ya tarehe 8/8/2009 kumsikiliza hatimaye kumpa jina jipya mbunge wao Dr Mwakyembe.Umati huo kwa kauli moja hatimaye ukakubaliana kuwa Dr Mwakyembe akiwa kwenye jimbo lake la Kyela aitwe "Obama"

Mkutano huo uliofanyika ktk viwanja vya CCM-Kyela mjini ulipitisha kwa kauli moja kuwa mwana Kyela yeyote atakayejitokeza kumpinga Mwakyembe ktk uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM na ule wa ubunge aulizwe ataifanyia nini kipya Kyela ambacho Mwakyembe hajakifanya?!Walikumbusha kuwa chini ya miaka 4 tu ya ubunge wa Mwakyembe;kila kata ina sekondari yake,umeme Kyela ni wa uhakika,maji safi na salama yapo,miundo-mbinu hasa madaraja yamejengwa,na huduma za afya hasa vijijini zimeimarishwa!

Katika mkutano huu,vijana wa CCM wa Kyela mjini walimueleza Mbunge Mwakyembe kuwa wamekasirishwa sana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaolikodela macho jimbo hilo ukiambatana ushawishi wa utoaji wa na vitu kama vile nyama ya ng'ombe kama hadaa kwa wananchi.

Mwakyembe mwenyewe akihutubia huku kasimama kwenye meza iliyotandikwa bendera ya Taifa tena akilindwa na wazee maarufu wa mji wa Kyela akiwemo mzee Mboka,Mzee Hasab Baba,Mzee Mwakanyika na wengine wengi aliwashukuru sana wakazi wa Kyela kwa kumuunga mkono na akahaidi kuwatumikia kwa moyo mkunjufu zaidi!

Yaliyoelezwa kwenye mkutan huo ni mengi sana,na kama una taka kuyajua kwa ufanisi basi piga simu hii ili uelezwe zaidi 0784 370 227

Nafikiri sasa mtamwelewa Malafyale ni nani. Alipozua mambo ya Mwakalinga kuna watu walifikiri ni kweli pamoja na Mwakalinga kukanusha kwamba hata Kyela hajafika.

Mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa CCM na wala sio uwanja. Ukumbi huo hauwezi hata kuingiza watu 1000. Kulikuwa na watu around 1000 wengine wakiwa nje ya ukumbi.

Kungelikuwa na kitu anachokisema Malafyale mungeliona hata kwenye TV.

Hakukuwa na kufungwa barabara wala hakukuwa na maandamano. Kwanza maandamano na mikutano ya nje imepigwa marafuku Kyela tokea zile vurugu za vijana. Ni mikutano ya ndani tu ndio inaruhusiwa na ndio maana hata huo mkutano wa Dr. ulifanyika kwenye ukumbi.

Huyu Malafyale yuko USA na ni yule mzee aliyetokea hata kwenye report ya Richmond na pia ana ubia kwenye kampuni ya kufua umeme. Ni mtu mzima na mwenye elimu yake kubwa, inashangaza anajiingiza kwenye hizi siasa za kupika.

Hata Wapambe hawakuwa kama inavyokuwa kwenye mikutano ya Dr. Ni yule Mwandishi Richard tu ndiye aliongea sana na kusema Dr. ni Obama ni pia ni mbunge wa Muyaya kama alivyokuwa anaitwa rais Banda kule Malawi. Dr. mwenyewe alikuwa amepoa sana na aliongelea ajali yake na kuwashukuru watu kwa maombi na pole baada ya ajali.

Kweli Malafyale ni mtu wa ajabu hasa na unatia aibu kweli kweli kwa kuzua mambo ambayo hayapo.
 
.

Mwakyembe amekuwa akifadhiliwa sana na shemeji yake (mengi) na kila mara anaongozana na wandishi wa ippmedia.

Mkuu una ushahidi wowote kuhusu haya madai yako?

Kumbuka kuwa mengi ni mmoja kati ya watu wanaochunguzwa na pccb kwa ajili ya ufisadi.
So what? unataka kujustify nini hapa?

Detail kuhusu hili ziliwakiliswa na Rostam Aziz (MB)

Kweli mapenzi ni kizunguzungu!
 
Back
Top Bottom