Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

 

Ohhh my God. Mods mbona mnaruhusu matusi ya hali ya juu namna hii??
 

Thubutuuu!! kwenye umeme wa upepo mkatolewa nje akawaletea makaratasi yote sasa kimyaa!
 
Thubutuuu!! kwenye umeme wa upepo mkatolewa nje akawaletea makaratasi yote sasa kimyaa!

Thubutu nini? Wee subiri tu utaona. Haraka haraka haina baraka.

Umeme wa UPEPO, alipewa kibano na DR. Slaa akakaa kimya. Alisema nini kuhusu USHIRIKA wake na Rostam Azziz? Walipokosana ndiyo akataka kuanzisha yeye akina Shalom.

Dada/kaka Maggie, hebu soma maelezo hayo hapo juu ya MWITA. Wabunge wa CCM walivuta 5M za EPA. Unasikia mama/baba, walivuta 5M za EPA na ndiyo maana hawasemi kitu chochote kuhusu EPA. Kama huamini si usubiri tu siku wakikosana na Rostam Azziz na yeye aamue kuwambua Watu wote waliopokea salamu kutoka kwa MJOMBA zikiwa kwenye packet. Na RA alivyo mshenzi, akawasainisha kabisaa kama alivyomfanya mchungaji Mtikila.

Wee mtu anakuja anakupa 5M na wala huulizi hizi pesa, mjomba kazitoa wapi?
 
Last edited:
Safi sana Mh Mwakyembe sisi wanaKyela daima tutakuunga mkono.....mpiganaji.....wale wa uzao wa ufisadi wakaogombee Zimbabwe! Umenisikia Mwakalinga?

Masanilo,
Kinepi_nepi amekujibu hapa chini.

Mkuu Kinepi_nepi ni maneno mazito sana haya. Aliye na macho haambiwi ona. Maneno yenyewe ya ki-utu uzima hasaa. Keep it up!!!

 
 
Msanilo.
Kumbe wewe ni secretary.
Ndiyo maana una muda mwingi wa kuandika pumba na ujinga mwingi sana hapa.

Mwanzo nilipoletewa CV yako nilibisha na sasa nimeamini.

Hongera sana sana .Nsesi amekwenda wapi?

Mwakalinga okoa kampeni yako kwa kutimua hawa wapambe wanaojikomba, mimi naona wanakuharibia hawa
 

Uwiii uwiiiiiiiii, Masanilo njooo huku uokoe jahazi.

Kumbe Mwakyembe ndiyo mzee wa VISASI? Aliponyimwa mlo kwenye Richmond akaja juu na kumkalia kooni Lowassa hadi akamtoa cheo cha Waziri mkuu wa Tanzania kwa mara ya kwanza.
Walipokosana na Rostam Azziz kwenye UMEME WA UPEPO, akaja na kuanza kuitisha vikao vya kusema "RA anaoga kwenye maji taka".
Huyu jamaa anaonekana kuwa mtu wa VISASI sana na hasira za kufa mtu. Loooohhhh, kwa kweli.
Haya wapambe wa Mwakyembe na mjibu sasa shutuma kutoka kwa Dr.Slaa kuwa Mwakyembe na Rostam Azziz walishirikiana kuanzisha kampuni la KIFISADI la umeme, huku akifahamu wazi kabisa kuwa RA si msafi.

Mwisho, kama kweli Rostam Azziz ana sahihi za watu wote (kumbuka alikuwa mweka hazina wa CCM) za watu wakipokea pesa za EPA, basi ingelikuwa heri yake AKIMBIE NCHI.
Mzee Mwanakijiji naanza kuamini sasa maneno yako kuwa ungelikuwa wewe ndiyo RA, basi ungelikimbia Tanzania. Yaani huyu jamaa ana siri nyingi za nchi yetu kuzidi hata Balali. Nafikiri kuna watu wengi wangelipenda kuwa na uhakika kwamba MILELE hatakuja kuropoka.
 
Uwiii uwiiiiiiiii, Masanilo njooo huku uokoe jahazi.

Kumbe Mwakyembe ndiyo mzee wa VISASI? Aliponyimwa mlo kwenye Richmond akaja juu na kumkalia kooni Lowassa hadi akamtoa cheo cha Waziri mkuu wa Tanzania kwa mara ya kwanza.

Suala la EPA linahusisha usalama wa taifa, tusije shikwa uhaini na vilaputopu vyetu vya kupewa...EPA iko complicated sana maana hata Mkulu wa Nchi imechangia kumweka pale magogoni. Hii imepelekea baadhi ya ring leaders wawe hawashikiki.

Richmond, najua unakumbuka ilikuwa kamati ya Bunge Mh Spika yule wa Urambo kuamua kuunda tume ichunguze, ndipo hapo Mfadhili wa Mwakalinga akaumbuka, na kuja na madai ya cheke chea kuwa hakutendewa haki ya kujitetea. Akajiuzulu kwa hasira.

All the best Harrison Mwakyembe, PhD
 

Na hapo Mwakyembe juzijuzi akajisifu kuwa "baadhi ya mambo waliyaficha".

Hata MEREMETA ilikuwa usalama wa Taifa, ila Mzee Mwanakiji akaiweka yote hapa ndani ya JF. Swala la EPA kabaki Dr. Slaa peke yake na sidhani kama JF watakuja kulifuatilia sana maana unaweza kukuta mtu unamfunua mama mkwe wako......
Masanilo, wasalimie huko Kanda2 na Mwafrika.
 
Last edited:
Wewe badala ya kupost kitu kizima unataka kupigiwa simu. Tunafaidi nini mpaka tupige simu na kwa gharama za nanai? Acha hizo.
 
Juu Mwakyembe Juu zaidi.Ila jamani anayeharibu siasa za Mbeya ni Mkuu wa Mkoa John Mwakipesile sijui kwa nini haamishwi au amewekwa kwa kazi ya kuvuruka Siasa hapo nini?
 
Jana mheshimiwa Mwakyembe alihutubia Ipinda na kuanza kuweka vijembe vyake. Aliwaambia wananchi kwamba Mwakalinga kaletwa Kyela na DC Mashimba na ndio maana rais aliamua kumfukuza kazi huyo DC.

Pia kwenye mkutano wa ndani na wapambe wake aliwaambia Mwakalinga amekamatwa na yuko mahabusu Uingereza na kwamba serikali inafanya mpango wa kumrejesha nchini.

Hizo ndio siasa za Kyela, vipi Mwakalinga uko salama huko? Sikujua na wewe una matatizo kama yule jamaa wa Ze Utamu.

Huyo rais JK yuko sehemu ngapi? Mara anamuunga mkono Mwakalinga mpaka kumtuma mtoto wake kumpigia kampeni, mara kamwondoa DC kwasababu DC anamwunga mkono Mwakalinga. Mara sasa kawaagiza Interpol wamrudishe Mwakalinga TZ.

Kuna mtu anatapatapa kweli kweli!
 

Kuna uwezekano wa kupata maneno (tape) ya maneno ya Mwakyembe akisema kuwa Mwakalinga yuko jela UK? Itabidi haya yatumike sana wakati wa kampeni. Fanya juu chini upate tape ya maneno hayo.
 


Mkuu Sikonge,

Najua unachekelea kwakuwa uko kwenye kampeni ya kumnadi Mwakalinga, kwahiyo popote unapompatia upenyo Mwakyembe huchelewi kukandamizia, siwezi kukulaumu kwa hilo kwa kuwa una uhuru na haki ya kumuunga mkono mtu yeyote unayemuona anafaa kuwa mwakilishi wako mjengoni (ingawa mbunge wako toka sikonge ni Saidi Nkumba ambaye vilevile uko against naye).

Lakini pamoja na hayo yote ni ukweli ulio dhahiri kwamba Mwakyembe amefanya kile ambacho wengi hawawezi kuthubutu kukifanya. Tume ngapi za bunge zimewahi kuundwa na zikaishia kuilamba miguu serikali?

Wabunge wangapi wamepewa zawadi ya uwaziri kwa kazi yao nzuri ya kuisafisha serikali?unakumbuka Abdala Kigoda na Wilson Masilingi walivyopata uwaziri enzi za mkapa?

Kwahiyo ukweli ni kwamba angalau Mwakyembe amethubutu kufanya kile wengi walichoshindwa, na wala hiyo haiwezi kuwa visasi.After all hakuwa peke yake, unajua kamati ile ilikuwa na wajumbe wangapi na kama findings za kamati zilikuwa uongo bunge lisingeyapitisha maazimio ya kamati yake tena yaliongezwa na bunge hadi kufikia 23.
 
huyu mwakyembe akisindwa ubunge 2010 nadhani anaweza akafa kwa BP.....huu ni uoga tu ,apokewe kama mfalme kwa lipi alilolifanya kyela..
 
Maneno yako Malafyale yanaonesha hukuwepo kwenye tukio ila umesimuliwa
 
Si tu Dr hajafanya la maana Kyela hata Taifa hajalifanyia la maana.

Richmond ilikuwa ni agizo sio yeye aliyelipua bomu kama Dr Slaa na EPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…