Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

This is my honest opinion and I stand to be corrected. I look at politicians with 2 possible angles/spheres of influence. First - in his/her constituency and Second - nationally. Wanasiasa wa TZ wapo ambao wamelala, wengine active ktk mambo yao majimboni, na wengine mambo ya kitaifa, wengine mchanganyiko wa majimboni na mambo ya kitaifa.
Mwakyembe ametetea sana maslahi ya taifa hili, na anajitahidi hata jimboni, sasa anaetaka kumuondoa kweli atuthibitishie kuwa yeye ana nguvu zaidi ya Mwakyembe, na si vinginevyo. Sijui wenzangu mnaopenda kuingia ktk siasa nia yenu inakuwa nini hasa, je ni kupata ubunge tu au kutetea maslahi ya wananchi. Huo ndio uzalendo, sio kuweka historia kuwa ulishawahi kuwa mbunge.

Tueleze kwanza ,Mwakyembe kafanya nini Jimboni kwake?Ofisi iko Kunduchi yeye ni balozi wa jimbo?
 
Kaka Mwakipesile kamwambia agombee kupitia CCM, na anajua itakuwa rahisi kuunganishwa kwenye network ya RA na EL,siunajua tena mambo ya IT...

Kwani lazima agombee Kyela tu hakuna majimbo mengine Mbeya? Au huko hauziki?
 
Kwani lazima agombee Kyela tu hakuna majimbo mengine Mbeya? Au huko hauziki?

Mafisadi akina Lowassa, RA, Karamagi na timu yao yote ya mtandao wameshaweka mkakati wa kuhakikisha Mwakyembe harudi tena bungeni 2010 sijui nani wengine ambao watakuwa ni target ya hili kundi la mafisadi, lakini akina Kilango, Sendeki, Shibuda na Seleli lazima nao wataingizwa kwenye huu mkakati wa kuwaondoa bungeni wabaya wao. Ama kweli mafisadi wameshika utamu nchini.
 
Tueleze kwanza ,Mwakyembe kafanya nini Jimboni kwake?Ofisi iko Kunduchi yeye ni balozi wa jimbo?

Hembu niambie mbunge gani ana permanent ofisi jimboni mwake kwa maana ya kutokuwa na ofisi ndogo Dar au Dom...ukiacha wabunge wa Dar? Kwani kosa kuwa na ofisi Dar wakati shughuli zote muhimu za kisiasa, kuchumi, kijamii etc mipango yake hufanywa na huratibiwa huko Dar? pia ofisi za serikali kuu zote zipo Dar kwa maana ya Wizara zote nyeti zipo Dar....sasa Mbunge awe na permanent ofisi jimboni...ili iwaje? aonekane na yeye anashare kwa karibu matatizo ya wananchi wake au the best ni kutafuta sehemu nzuri strategically kwa ajili ya kufanikisha mipango ya maendeleo jimboni kwake?
 
Tueleze kwanza ,Mwakyembe kafanya nini Jimboni kwake?

Kafanya mengi, lakini moja kubwa ni kwamba kafanikisha ujenzi wa daraja katika jimbo lake mara baada ya mafuriko, kwa kusaidiwa na JWTZ.
Kwa sasa wananchi hawasombwi na maji tena katika mto Lufilyo. Kumbuka hapajawahi kuwa na daraja la kudumu katika eneo hilo tangu nchi hii ipate uhuru! Kwa habari zaidi juu ya daraja hilo soma hapa.
 
Mafisadi akina Lowassa, RA, Karamagi na timu yao yote ya mtandao wameshaweka mkakati wa kuhakikisha Mwakyembe harudi tena bungeni 2010

Unajua wakiingia kwa gia hii nina amini Mwakalinga hawezi kuupata ubunge kama kweli anatumiwa na hawa watu na vile vile kama yupo mgongoni mwa Mwakipesile yaani aandike maumivu tu bora atafute jimbo jingine.
 
Tueleze kwanza ,Mwakyembe kafanya nini Jimboni kwake?Ofisi iko Kunduchi yeye ni balozi wa jimbo?

Wakati ukisubiria jibu lako, je unaweza kueleza hapa Mwakalinga alifata nini monduli kwa Ma-mvi? hiyo michango ya mtoto wa Kikwete (fisadi wa IMMA) na wengine ina usalama kwa wana Kyela, support ya watu kama Kanda2 ambao wamejaa chuki za kidini dhidi ya wakristo ni mpango safi kwa wana kyela?

Na je, Mwakalinga anatisha (au anatambia) nani kuwa amekaa ulaya miaka 18?
 
Unajua wakiingia kwa gia hii nina amini Mwakalinga hawezi kuupata ubunge kama kweli anatumiwa na hawa watu na vile vile kama yupo mgongoni mwa Mwakipesile yaani aandike maumivu tu bora atafute jimbo jingine.

Makosa yaliaanza pale alipopitia kwa mzee wa richmonduli kupokea baraka. Akazidi kuongeza chumvi kwenye kidonda kwa kutaka kumtumia mtoto wa Kikwete (ambaye ni fisadi kubwa tu) kumpigia debe.

Kama kweli huyu Mwakalinga ni mwanzilishi wa JF, basi hii JF ilianzia mguu tofauti.
 
Kitendo cha Mwakalinga kuitumia JF kwenye kampeni zake kinafaa kupigwa vita na wote wanaoitakia mema JF,hakina future nzuri!!!

Huyo aliyemtaja mwakalinga kuwa ndiye mtanzania mbona yeye anapiga kampeni hapa kujimilikisha hilo jimbo la kelya.?
Kwanini hapewi onyo na ma mods?
 
Huyo aliyemtaja mwakalinga kuwa ndiye mtanzania mbona yeye anapiga kampeni hapa kujimilikisha hilo jimbo la kelya.?
Kwanini hapewi onyo na ma mods?

ha ha ha ha ... vilio mpaka asubuhi.
 
Kwani lazima agombee Kyela tu hakuna majimbo mengine Mbeya? Au huko hauziki?

Ndo shindwa kushangaa sasa hapo mkuu! But ukiangalia post ya BAK hapo chini u can connect the dots poti!

Mafisadi akina Lowassa, RA, Karamagi na timu yao yote ya mtandao wameshaweka mkakati wa kuhakikisha Mwakyembe harudi tena bungeni 2010 sijui nani wengine ambao watakuwa ni target ya hili kundi la mafisadi, lakini akina Kilango, Sendeki, Shibuda na Seleli lazima nao wataingizwa kwenye huu mkakati wa kuwaondoa bungeni wabaya wao. Ama kweli mafisadi wameshika utamu nchini.

Mwenye macho haambiwi tazama mkuu! Si umesikia na Six analalamika watu wanagawa pikipiki na misaada kibao jimboni kwake mkuu? So wacha tusubiri 2010!
 
Kafanya mengi, lakini moja kubwa ni kwamba kafanikisha ujenzi wa daraja katika jimbo lake mara baada ya mafuriko, kwa kusaidiwa na JWTZhttp://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=141

Hili daraja Mwakipesile alishindwa kabisa kulijenga na alileta chuki za ajabu wkt JWTZ wanajenga daraja hilo na wananchi wanajua hilo sasa kama Mwakalinga anapigiwa chapuo na mtu ambae ni Mwakipesile aandike maumivu wananchi wanajua kabisa kidonda walichopata toka kwa Mwakipesile sasa kama Mwakalinga atoneshe kidonda hicho aende kwa mgongo wa Mwakipesile.
Kama anania ya kuendeleza Demokrasia aachane na misaada ya akina mzee mvi-nyeupe hata Mwakipesile watamuharibia.
 
Mafisadi akina Lowassa, RA, Karamagi na timu yao yote ya mtandao wameshaweka mkakati wa kuhakikisha Mwakyembe harudi tena bungeni 2010 sijui nani wengine ambao watakuwa ni target ya hili kundi la mafisadi, lakini akina Kilango, Sendeki, Shibuda na Seleli lazima nao wataingizwa kwenye huu mkakati wa kuwaondoa bungeni wabaya wao. Ama kweli mafisadi wameshika utamu nchini.

Hizo ni fikra mufu.
 
Ndo shindwa kushangaa sasa hapo mkuu! But ukiangalia post ya BAK hapo chini u can connect the dots poti!

Mwenye macho haambiwi tazama mkuu! Si umesikia na Six analalamika watu wanagawa pikipiki na misaada kibao jimboni kwake mkuu? So wacha tusubiri 2010!

Kuanzia leo, George Mwakalinga ni fisadi papa kama mafisadi wengine. Na tena akane taarifa zinazoandikwa na wapambe zake kule majira kuwa yeye ndiye muanzilishi na mwanachama mahiri wa JF.

Hii JF haiendeshwi na mafisadi (ingawa hawakomi kujiletaleta hapa).
 
Huyo aliyemtaja mwakalinga kuwa ndiye mtanzania mbona yeye anapiga kampeni hapa kujimilikisha hilo jimbo la kelya.?
Kwanini hapewi onyo na ma mods?

Mkuu nyamaza mods wanakazi ngapi hapa?
Wanakazi nyingi sana.
Nyamaza kulia lia mkuu.
 
Mbona mimi nikitaja Nsesi ndiye Mwakyembe inafutwa kwa kasi???

ha hahaha ... kwa sababu Nsesi sio fisadi kama alivyo Lowasa, Rostam na Mwakipesile ambao ndio wanamfadhili George Mwakalinga.
 
Hizo ni fikra mufu.

Zipi ni Fikira hai? ......kuishi ulaya for 18yrs? kutangaza sera za kujipendekeza kutoa laptop kama hongo.... wakati suala la kuboresha miundo mbinu ni la serikali badala ya kutangaza ni namna gani au ana mbinu gani ya kuibana serikali kuweka miundo mbinu hiyo.......!
 
Mbona mimi nikitaja Nsesi ndiye Mwakyembe inafutwa kwa kasi???

Una uhakika lakini mkuu?
Maana lawama zingine mnawatwisha mods hazina miguu jaribuni kuwa wastraabu.
 
Back
Top Bottom