Kyela, Mbeya: Mwanachama wa CHADEMA afungwa Maisha kwa kuchoma moto nyumba ya Mwana-CCM

Safi sana!

Analeta mihemko ya kijinga anafikiri nchi ni ya Lisu hii?

Vijana acheni upumbavu! Acheni Utundu Lisu mtaishia jela wajinga nyie!
 
Kama alichoma kweli na hakuna kifo, hukumu yake huwa ni uharibifu wa Mali kifungo ni chini ya miaka miwili!! Huyu hakimu hana tofauti na ibilisi
Mtu umejipinda kujenga nyumba alafu mtu na ujinga wake wa kitundulisu unaenda na mihemko yako kuchoma moto?
 
Hii nchi inaendeshwa ki itikadi - ukiwa na itikadi tofauti ya CCM utapata misukosuko kibao wewe na familia yako. CCM inatamba kwamba ipo ndani ya kila taasisi nyeti, kwa hili nakubaliana nao asilimia mia.
 
[emoji871]Mleta uzi ungetulia na kuandika kitu kinachoeleweka.

[emoji871]Je ni kweli tukio la uchomaji nyumba lilitokea?

[emoji871]Je mtuhumiwa pamoja na kufikishwa mahakamani,kisheria ushahidi ulisemaje?

[emoji871]Kuwa mwana Chadema sio kinga ya kutopatikana na hatia pale jinai inapotendeka!

[emoji871]Tunaporipoti hizi habari za kisheria.
Vema tusijifiche kwenye mgongo wa vyama vya kisiasa.

[emoji871]Wewe mleta habari umeshindwa nini kumtaja huyo mwana CCM,aliyechomewa nyumba yake.

[emoji871]Hii ingetowa picha kamili ya tukio na pia maamuzi yaliyotolewa na Mahakama.

[emoji871]Na kibaya zaidi kuna nyumbu humu,wao wakiishasikia jambo linaihusu Chadema.
Basi wao huingia kazini kulaani ovyo,
Bila hata kujiridhisha na story balancing.

🤌Fundisho kwa wafia vyama!

[emoji871]Kuna funzo kubwa la kuchukua hapo.unapofanya siasa kwa kutumwa.
Ujuwe pia kuna gharama za kutumika.

[emoji871]Na pale zitakapokukuta ujuwe utazibeba wewe mwenyewe na kuiacha familia yako ikiteseka na siasa zikiendelea kama siku zote.
 
...Tunashukuru kwa taarifa...haya sasa mawakili wasomi wa Chama wajipange wakate rufaa...
 
Vijana mnapenda sana matusi. Arson ni kuchoma moto mali yeyote ya mtu, sio nyumba tu. Ukichoma moto nguo za mwenzako ni arson. Ukichoma moto baiskeli ya mwenzako, ni arson. Ukichoma moto pagala, ni arson. Ukichoma mazao ya mwenzio, ni arson.Unataka kutuambia kuwa adhabu ya makosa yote haya ni kifungo cha maisha?

Ninavyojua mimi kifungo cha maisha ni maximum sentence na sio mandatory. Kifungo hicho kinatolewa pale ambapo mtu amechoma moto nyumba akijua ndani kuna mtu au watu kwa lengo la kuwaua. Au mtu ana tabia ya kuchoma nyumba za wenzake. Au amechoma nyumba kama sehemu ya ugaidi. Vyote hivyo inaelekea havikuweko kwenye hii kesi, na adhabu imetolewa kumkomoa mtu ambae hata hakuhusika.

Kutetea kila kitendo cha uonezi kwa sababu ya ushabiki wa kisiasa ni upumbavu.

Amandla...
 
Wewe una hakika gani ni uongo? Wanachadema wao ni malaika hawafanyi makosa? Umefuatilia muenendo wa hiyo kesi na mkajiridhisha kaonewa? Mlimuwekea wakili kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki?
 
Kuna watu mlizaliwa akili haipo mama zenu walitoa uchafu tu leba ange! ange! Ndiyo nini?😎
hii mihemko nyie watu wa siasa ndio inawaponza,sasa kama hapa umemtukana mwenzako na kumtukania mamaye ukihukumiwa wewe na wenzako mtalalamika mnaonewa hamkutukana!
 
Eti kosa dogo hukumu kubwa mnajua alivuja jasho la kiasi gani kujenga nyumba yake?

Heko kwa Hakimu, funzo kwa wengine wenye mihemko ya kisiasa isiyo na tija.
Sheria iko wazi, ukichoma Nyumba adhabu yake ni kifungo cha maisha. Lazima tutafakari kabla ya kufanya maamuzi ya hovyo kisa siasa zinazopita na kuziachia maumivu familia zetu.
 
Vipi wale waliofungwa maisha kwa kuchoma kituo cha Polisi, akiwemo dogo wa shule aliyekuwa under 18?

Ukithibitika umechoma bila sababu yeyote adhabu yake ni kifungo cha maisha basi
 
Vipi wale waliofungwa maisha kwa kuchoma kituo cha Polisi, akiwemo dogo wa shule aliyekuwa under 18?

Ukithibitika umechoma bila sababu yeyote adhabu yake ni kifungo cha maisha basi
Ni adhabu nyingine ya kijinga na uonevu kama ile ya kuwafunga wakina Mbowe kwa sababu askari amemuua yule binti Akwilina.
Kifungo cha maisha ni maximum, Hakimu anaweza kutoa adhabu pungufu ya hapo kulingana na mazingira.

Amandla...
 
[emoji871]Je wewe umekwisha pata nakala ya hukumu na mwenendo wa kesi nzima na ukajiridhisha kwamba wakati nyumba hiyo ikichomwa moto kulikuwa hakuna watu ndani yake?

[emoji871]Tutaomba Martin Masesa aje kutupatia muhtasari wa hii kesi.
 
Nashangaa watu mnavyomtetea huyo mtuhumiwa utadhani mlikuwepo siku ya tukio...kuna sehemu nyingi chadema walileta vurugu 2020 kuna ofisi zilivunjwa sana ilo sio ata la kubishana.
 
[emoji871]Je wewe umekwisha pata nakala ya hukumu na mwenendo wa kesi nzima na ukajiridhisha kwamba wakati nyumba hiyo ikichomwa moto kulikuwa hakuna watu ndani yake?

[emoji871]Tutaomba Martin Masesa aje kutupatia muhtasari wa hii kesi.
Aliyeleta taarifa amesema hamna mahali paliposemwa kuwa kulikuwa na watu ndani.

Amandla...
 
Nashangaa watu mnavyomtetea huyo mtuhumiwa utadhani mlikuwepo siku ya tukio...kuna sehemu nyingi chadema walileta vurugu 2020 kuna ofisi zilivunjwa sana ilo sio ata la kubishana.
Na CCM wao hawakufanya fujo? Tulioyaona Hai na wale waliompopoa mawe mgombea urais wa Chadema walikuwa Chadema? Ofisi ngapi za Chadema zimevunjwa bila hatua yeyote kuchukuliwa? Hivi wale waliopigwa picha wakimpiga matofali mfuasi wa Chadema walihukumiwa miezi mingapi vile?

Kwenye hili ungetusaidia sana kama ungetueleza yaliyotokea kwa vile inaelekea ulikuwepo siku ya tukio.

Amandla...
 
Weka ushahidi , Chadema Tunduma walisingiziwa kuua mtu , wakawekwa ndani miezi mingi kama Mbowe , 54 chadema members , leo wote wako nje , wauaji wawezaje kuachiwa ?
Ushahidi ushawekwa na Jamhuri na haukuacha shaka yoyote ndio maana akatiwa hatiani.

Hao unaosema walisingiziwa kuua, ina maana Jamhuri ilishindwa kuthibitisha madai yao ndio maana wakaachiwa huru.

Mahakama imetenda haki.
 
Ushahidi ushawekwa na Jamhuri na haukuacha shaka yoyote ndio maana akatiwa hatiani.

Hao unaosema walisingiziwa kuua, ina maana Jamhuri ilishindwa kuthibitisha madai yao ndio maana wakaachiwa huru.

Mahakama imetenda haki.
dhambi ya unafiki itakutafuna milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…