Kyela, Mbeya: Mwanachama wa CHADEMA afungwa Maisha kwa kuchoma moto nyumba ya Mwana-CCM

Kyela, Mbeya: Mwanachama wa CHADEMA afungwa Maisha kwa kuchoma moto nyumba ya Mwana-CCM

Vijana mnapenda sana matusi. Arson ni kuchoma moto mali yeyote ya mtu, sio nyumba tu. Ukichoma moto nguo za mwenzako ni arson. Ukichoma moto baiskeli ya mwenzako, ni arson. Ukichoma moto pagala, ni arson. Ukichoma mazao ya mwenzio, ni arson.Unataka kutuambia kuwa adhabu ya makosa yote haya ni kifungo cha maisha?

Ninavyojua mimi kifungo cha maisha ni maximum sentence na sio mandatory. Kifungo hicho kinatolewa pale ambapo mtu amechoma moto nyumba akijua ndani kuna mtu au watu kwa lengo la kuwaua. Au mtu ana tabia ya kuchoma nyumba za wenzake. Au amechoma nyumba kama sehemu ya ugaidi. Vyote hivyo inaelekea havikuweko kwenye hii kesi, na adhabu imetolewa kumkomoa mtu ambae hata hakuhusika.

Kutetea kila kitendo cha uonezi kwa sababu ya ushabiki wa kisiasa ni upumbavu.

Amandla...

Mimi nilijibu kuhusu ukubwa wa adhabu, kama alichoma nyumba ama hakuchoma mimi sijui.
Ninachojua nikwamba ukichoma nyumba ya mtu adhabu yake ni ngumu.

Sasa kamaunasema hajahusika mimi sijui ni juuya walio shuhudia kutohusikakwake kukata rufaa na kudhibitisha ionezi,na kama kunauonezi bila shaka adhabu itatengiwa.
 
Mimi nilijibu kuhusu ukubwa wa adhabu, kama alichoma nyumba ama hakuchoma mimi sijui.
Ninachojua nikwamba ukichoma nyumba ya mtu adhabu yake ni ngumu.

Sasa kamaunasema hajahusika mimi sijui ni juuya walio shuhudia kutohusikakwake kukata rufaa na kudhibitisha ionezi,na kama kunauonezi bila shaka adhabu itatengiwa.
Ndio maana ukaanza na matusi? Hata hiyo adhabu ngumu unayozungumzia ina muongozo wake. Sio kila anaechoma moto nyumba anatakiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha. Kifungo cha maisha ni adhabu ya mwisho.

Hizi adhabu zinatolewa ili kumkomoa mtu kwa sababu wanajua mpaka uamuzi wa rufaa utakapotoka jamaa atakuwa ameisha umia sana jela.

Nadhani wanazitoa wakijua kabisa kuwa zitatenguliwa kwenye rufaa. Nia ni kumkomoa mtu na sio kutenda haki. Tumeiona kwa Sugu. Tumeiona kwa wakina Mbowe. Na tunaendelea kuiona.

Amandla...

Amandla...
 
Kwa wanaosema kosa la arson hukumu yake ni kifungo cha maisha, warudie kesi ya mwanachama wa Chadema Kishabi na wenzake wanne waliohukumiwa kifungo cha miaka MINNE kwa kosa la kuchoma moto kituo cha polisi Shimiyu. Hukumu hiyo ilitenguliwa na Mahakama Kuu baada ya kukata rufaa.

Wanaowafunga maisha wenzao kwa kosa la arson wana roho mbaya tu.

Amandla...
 
Nashangaa watu mnavyomtetea huyo mtuhumiwa utadhani mlikuwepo siku ya tukio...kuna sehemu nyingi chadema walileta vurugu 2020 kuna ofisi zilivunjwa sana ilo sio ata la kubishana.
Hii kesi ni ya 2019 wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Taarifa kwa Umma: Leo Tarehe 15/2/2022 Mahakama ya Wilaya ya Kyela imemhukumu kifungo cha maisha Gerald Mwakitalu kwa kesi ya uongo ya kuchoma moto nyumba ya Mwana-CCM kwenye uchaguzi wa 2020, huu ni ule ule mwendelezo wa hujuma dhidi ya CHADEMA ulioasisiwa na utawala wa awamu ya 5 kwa hisani ya Jiwe.

View attachment 2120559View attachment 2120558

Hata hivyo Chadema - Kyela imeahidi kukata rufaa ili kupambana na hukumu hiyo ya mchongo .

Nakala: PETER KIBATALA
Ni uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
 
dhambi ya unafiki itakutafuna milele
Wewe ndio mnafiki ambaye unataka kila maamuzi ya Mahakama yawe mazuri kwa upande unaotaka wewe. Asingefungwa ungesema mahakama imetenda haki, sasa katiwa korokoroni unasema mahakama haijatenda haki.

Hata hivyo rufaa ipo wazi.
 
Waliomsababishia hukumu ya uongo kijana huyu hakika WATALIPWA KWA UBAYA WAO .
 
Kwenye kichwa cha Habari niliandika kwamba hii kesi ilikuwa ya uongo , sasa Moderator uliye edit heading ile unajisikiaje unaposikia kwamba Mtuhumiwa huyu ameachiwa huru kwa sababu kesi ile ilikuwa ya Uongo ?

Mungu akusamehe sana
 
Eti kosa dogo hukumu kubwa mnajua alivuja jasho la kiasi gani kujenga nyumba yake?

Heko kwa Hakimu, funzo kwa wengine wenye mihemko ya kisiasa isiyo na tija.
Unajisikiaje kwa roho yako mbaya utofauti wa vyama usitufanye kukosa ubinadam
 
Back
Top Bottom