Jacobus,
Unaposema ligi fulani ni bora kuliko nyingine inabidi useme unatumia vigezo gani,watu wanabishana sana kishabiki lakini wanashindwa kuweka vigezo walivyotumia.Je vigezo vya timu bora ni vipi?
- Ligi ambayo timu zake zimefanikiwa kuchukua mengi makombe ya ulaya zaidi
- Idadi ya wachezaji maarufu/mastaa ambao wanachezea kwenye hiyo ligi
- Utajiri wa kiuchumi wa vilabu vilivyopo kwenye hiyo ligi kuu ya hiyo nchi
- Upinzani na tofauti iliyopo kati ya vilabu vya juu na vya chini kwenye hiyo league
- Staili ya uchezaji ya soka kwenye hizo ligi
- Matokeo kati ya timu kutoka kwenye hizo ligi zinapokutana
Ngoja tujue vigezo then tuanze kufanya assesment ligi gani ni bora