La Liga vs EPL.

La Liga vs EPL.

sasa mbona husemei kuhusu barcelona kua wa kwanza LA LIGA lakini wamechapwa goli mbili na AC MILAN ambayo iko ya tatu na point 11 nyuma ya juventus? kwa hiyo unataka kusema SERIE A ni zaidi ya LA LIGA kwa kua ac milan wamewachapa barcelona???

unaongea pumba tu..ndio mijitu isiyokua na uzoefu wa soka nyie mnapayuka payuka
Mkuu Barca ki ukweli hatupo sawa hivi sasa, hata Mourinho hapa ataafiki, baada ya kocha wetu mkuu kuwa katika matibabu. Lakini ManU hakuna aliyekosekana (walikuwa full masinonda) kuanzia benchi la ufundi mpaka mashabiki wake.
 
Yeah nakubaliana na ww mkuu. Wabongo kawaida yao ni kubwabwaja bila kufanya tathmini ya vitu. Kwanza tangu lini ubora wa ligi au timu una determiniwa kwa ushindi wa siku moja au mbili? Ukiangalia ligi ya Spain timu zinazoshinda makombe( La liga na Copa del rey) mara nyingi kwa miaka zaidi ya kumi iliyopita ni Barca na Real Madrid. Hakuna timu zingine zinabeba makombe mengi zaidi ya hizo. La liga unaweza kuifananisha na Ligi ya Bongo (enzi zile) bingwa alikuwa Yanga au Simba. Hakuna timu nyingine zinazoweka upinzani mkubwa Spain, afadhali hata ligi ya kirushwa-rushwa ya Italia timu zinazogombania ubingwa ni zaidi ya mbili mwaka baada ya mwaka. Ukiondoa kelele za media na kubwabwaja kwa wapenda soka wa England, ligi yao ina ushindani. Timu ndogo zinatoa kamasi timu kubwa sio kama Spain.
Na wachezaji bora wa FIFA wengi wametokea La Liga.
 
so epl walipoingiza timu tatu nusu fainali na mbili fainali walibahatisha sio?unaweza weka takwimu hapa kuonyesha ni timu za ligi gani zimeingia nusu fainali zaidi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita?
Kwanza UK ni kisiwa na hakiko Ulaya hivo wanabebwa tuu ili wasionekane wapweke.
 
hawajui hata ligi bora ikoje wanabwabwaja tu.ligi barca anaenda kwa bilbao mnasubiri kusikia messi kafunga ngapi/barca wameshinda goli ngapi?just imagine,man city anaenda kwa stok cit hana uhakika na ushindi au man u anaenda reading hana uhakika wa kushinda!!!spain kuna timu bora sio ligi bora,jifunzeni kutofautisha mambo.
Hah hah hah hah! Timu bora? Blatter, rais wa FIFA kama sijasahau mwaka jana alitamka kuwa LIGI BORA ni La Liga mkuu. Kocha wa Real Madrid kasema juzi tu kuwa 'timu bora imeshindwa' akiwapaka kilemba cha ukoka!
LIGI BORA HUZALIWA NA TIMU BORA.
 
Ah, wazee wa La Liga! Ligi ya timu mbili.....!
Kama una DSTV jaribu kujifanya unapoteza muda kwa kuangalia La Liga siku za 'weekend' kwa timu zote (sio tu kuangalia mechi za Barca na Real Madrid) na utaamini soka zuri lipo hapo. Naamini hutapenda tena EPL.
HUU NI USHAURI WA BURE NAKUPA. SIUZI HATA SENTI MOJA.
 
Ofcoz unasababu ya kusema hivyo, even though kiwango cha La Liga kimedrop tofauti na msimu uliopita when Madrid, Barca, Atletico Madrid, Bilbao zilivyokuwa tishio kwa vilabu ulaya hasa vile vya England
Kwanza hongera mzee mwenzangu, nilikuwa nawe against hawa domo kaya. Mie bado nasema kuwa goli ulizomfunga ManU ni 3-0. Wanaobisha waseme mfungaji wa ManU ni nani!
 
Mkuu mtotowamjini unajua kuna watu wameanza kuangalia mpira wa Ulaya miaka mitatu minne iliyopita ukibishana nao utaonekana mjinga bora kunyamaza.

sasa mbona husemei kuhusu barcelona kua wa kwanza LA LIGA lakini wamechapwa goli mbili na AC MILAN ambayo iko ya tatu na point 11 nyuma ya juventus? kwa hiyo unataka kusema SERIE A ni zaidi ya LA LIGA kwa kua ac milan wamewachapa barcelona???

unaongea pumba tu..ndio mijitu isiyokua na uzoefu wa soka nyie mnapayuka payuka
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu! japo mimi kote kote nipo EPL na La Liga ila najua La Liga iko juu kisoka zaidi ya EPL hilo mimi silibishii!
 
Kweli kabisa. Mie kwa mshabiki wa Liverpool namheshimu kidogo kuliko hawa wa ManU, Arsenal au Chelsea.

Na wengi wameanza kuangalia mpira tangu enzi za Channel ten na mchambuzi alikuwa ni Dokta Rick, wengi ndo walianza kuzijua timu tokea hapo kwa msaada wa Dokta Rick!
 
Na wengi wameanza kuangalia mpira tangu enzi za Channel ten na mchambuzi alikuwa ni Dokta Rick, wengi ndo walianza kuzijua timu tokea hapo kwa msaada wa Dokta Rick!
Mkuu upo sahihi mno mbona! DSTV ilipoingia na channel zake tatu ndo iliwamaliza kabisa.
 
Jacobus,

Unaposema ligi fulani ni bora kuliko nyingine inabidi useme unatumia vigezo gani,watu wanabishana sana kishabiki lakini wanashindwa kuweka vigezo walivyotumia.Je vigezo vya timu bora ni vipi?

  • Ligi ambayo timu zake zimefanikiwa kuchukua mengi makombe ya ulaya zaidi
  • Idadi ya wachezaji maarufu/mastaa ambao wanachezea kwenye hiyo ligi
  • Utajiri wa kiuchumi wa vilabu vilivyopo kwenye hiyo ligi kuu ya hiyo nchi
  • Upinzani na tofauti iliyopo kati ya vilabu vya juu na vya chini kwenye hiyo league
  • Staili ya uchezaji ya soka kwenye hizo ligi
  • Matokeo kati ya timu kutoka kwenye hizo ligi zinapokutana

Ngoja tujue vigezo then tuanze kufanya assesment ligi gani ni bora
 
Last edited by a moderator:
Jamani mchezo wa soka si sawa na karata......Mbona Norwich alimfunga Man Utd, Liverpool alimfunga Norwich, wakati huo huo liverpool ilichpwa na Man Utd
 
Jacobus,

Unaposema ligi fulani ni bora kuliko nyingine inabidi useme unatumia vigezo gani,watu wanabishana sana kishabiki lakini wanashindwa kuweka vigezo walivyotumia.Je vigezo vya timu bora ni vipi?

  • Ligi ambayo timu zake zimefanikiwa kuchukua mengi makombe ya ulaya zaidi
  • Idadi ya wachezaji maarufu/mastaa ambao wanachezea kwenye hiyo ligi
  • Utajiri wa kiuchumi wa vilabu vilivyopo kwenye hiyo ligi kuu ya hiyo nchi
  • Upinzani na tofauti iliyopo kati ya vilabu vya juu na vya chini kwenye hiyo league
  • Staili ya uchezaji ya soka kwenye hizo ligi
  • Matokeo kati ya timu kutoka kwenye hizo ligi zinapokutana

Ngoja tujue vigezo then tuanze kufanya assesment ligi gani ni bora
Swali lako ni zuri (limekaa ki-EPL zaidi). Nimeisha sema humuhumu kuwa hata rais wa FIFA (Blatter) alitamka jambo hili sio kutuambia sisi Watanzania ila akiwaeleza walimwengu kuhusu UBORA wa La Liga.
 
Laliga ipo juu. Tatizo ndugu zetu wa england vyombo vyao vya habari wanajipaisha sana, kuanzia ligi yao mpaka timu lao la taifa. Hawana tofauti na sisi maneno mengi mpira hakuna. Mimi naona bora wangewachukua Rage na Julio

Hapo unakosea wanaongea sana na mpira wanacheza..kamwe huwezi linganisha ligi/timu za bongo na EPL bana!!! utakuwa unakosea...

IN OTHER NEWS: mnapoiponda Chelsea mi nachukiaaaa....:nono:
 
Jacobus ,kumbe na wewe ndio wale wale mnaongea kishabiki,toa vigezo vyako hata Blatter akiulizwa hili swali atatoa sababu/vigezo vya tamko lake
 
Last edited by a moderator:
Na wachezaji bora wa FIFA wengi wametokea La Liga.

Ni kweli wengi wanatokea La liga lakini ukumbuke jinsi hao wachezaji bora wanavyopatikana. Wapiga kura wengi wanatokea South America ambao wanafuatilia ligi kuu mbili Serie A na La Liga badala ya EPL, Ligue 1, Bundesliga,Eredivisie nk. Jiulize kuna wachezaji bora wangapi waliotoka nje ya Serie A, na La Liga? Pia ukifuatilia tamaduni za South Americans hasa hasa Brasil na Argentina zinafanana na kitaliano na kispanish ndo maana wanavutiwa na hizo ligi.
 
Jacobus,

Unaposema ligi fulani ni bora kuliko nyingine inabidi useme unatumia vigezo gani,watu wanabishana sana kishabiki lakini wanashindwa kuweka vigezo walivyotumia.Je vigezo vya timu bora ni vipi?

  • Ligi ambayo timu zake zimefanikiwa kuchukua mengi makombe ya ulaya zaidi
  • Idadi ya wachezaji maarufu/mastaa ambao wanachezea kwenye hiyo ligi
  • Utajiri wa kiuchumi wa vilabu vilivyopo kwenye hiyo ligi kuu ya hiyo nchi
  • Upinzani na tofauti iliyopo kati ya vilabu vya juu na vya chini kwenye hiyo league
  • Staili ya uchezaji ya soka kwenye hizo ligi
  • Matokeo kati ya timu kutoka kwenye hizo ligi zinapokutana

Ngoja tujue vigezo then tuanze kufanya assesment ligi gani ni bora

Swali zuri, kwangu mimi natumia hicho kigezo cha mwisho ktk hivyo ulivyoviorodhesha, ngoja mtoa mada naye aseme ni vigezo vp vya kuzingatia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom