Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna maandiko yanasema: Basi njoo unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitaweza tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa na yeye umlaaniye hulaaniwa.
1.Laana ni sehemu ya kuua nguvu na laana hutoka kwenye kinywa cha mtu aliyeandaliwa na madhabahu, laana humfanya mtu apigwe, laana humfanya mtu afukuzwe, miungu ikitaka kumvuruga mtu inatumia laana kwanza.
2.Laana ni silaha ambayo inatumiwa na adui maeneo mengi bila watu kuwa makini.
Laana imekuwa silaha ya kuangamiza maono ya wengi bila wao kujua wanapigana na nini kumbe ni silaha ya laana toka vinywa vya watu kupitia miungu yao.
3.Hili jambo limekuwa likitumika na baadhi ya watu wanaoitwa watumishi wa Mungu pale wanapoona kuna mtu haendani nao au kukinzana nao ...wamekuwa wanatumia laana kama vitisho au silaha ya maangamizi kwa baadhi ya watu.
Hii ni dalili ya kwamba baadhi yao vinywa vya watumishi vinatumiwa na miungu kulaani!!. Maana neno linasema waombeeni wanaowaudhi. Pia samehe upishe ili upishe adhabu ya Mungu.
4.Ni mara nyingi utasikia watu baadhi tena ni watumishi wakisema fulani biashara yake imekufa ,ndoa yake imevurugika, mtoto wake amefeli, au amefukuzwa kazi au huduma imekufa au maisha yameenda mrama "sisi ndio tulimlaani au tuliomba"(utagundua huu ni uchawi toka kwa miungu) Ukichunguza watu hawa utagundua si wepesi kuonyesha shuhuda za mema waliyoomba.
Kwa miaka ya hivi karibuni nimekutana na baadhi ya watu wana matatizo na misongo ya mawazo na hawafanikiwi, ukishauriana nao unagundua wamelaaniwa na watumishi na kutishiwa vifo na kutokufanikiwa. Je ni Mungu yupi anayetaka tulaani badala ya kubariki!!? utagundua ni miungu inatumia vinywa vya baadhi ya watumishi bandia
Nafasi za utumishi tumepewa bure ni vyema tukazitumia kujenga na pia kujikomboa maeneo ambayo midomo yetu haijakombolewa
Mzazi anajilinda asimlaani mtoto wake halafu anashangaa haeleweki kumbe ameshalaaniwa na baadhi ya watumishi, hili ni jambo la kuomba rehema na kufuatilia pia ibada ambazo zinaweza kuleta madhara hata kwa vijana na mabinti na watu wengine.
Mungu aturehemu na afute kila laana na inayotamkwa ili kuua maono au nguvu. Ndoto na Nuru
Ndimi Mjoli wenu
Jr.