Laana inavyovuruga watu bila kujua imetoka madhabahu gani!

Laana inavyovuruga watu bila kujua imetoka madhabahu gani!

Kuna maandiko yanasema: Basi njoo unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitaweza tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa na yeye umlaaniye hulaaniwa.

1.Laana ni sehemu ya kuua nguvu na laana hutoka kwenye kinywa cha mtu aliyeandaliwa na madhabahu, laana humfanya mtu apigwe, laana humfanya mtu afukuzwe, miungu ikitaka kumvuruga mtu inatumia laana kwanza.

2.Laana ni silaha ambayo inatumiwa na adui maeneo mengi bila watu kuwa makini.

Laana imekuwa silaha ya kuangamiza maono ya wengi bila wao kujua wanapigana na nini kumbe ni silaha ya laana toka vinywa vya watu kupitia miungu yao.

3.Hili jambo limekuwa likitumika na baadhi ya watu wanaoitwa watumishi wa Mungu pale wanapoona kuna mtu haendani nao au kukinzana nao ...wamekuwa wanatumia laana kama vitisho au silaha ya maangamizi kwa baadhi ya watu.

Hii ni dalili ya kwamba baadhi yao vinywa vya watumishi vinatumiwa na miungu kulaani!!. Maana neno linasema waombeeni wanaowaudhi. Pia samehe upishe ili upishe adhabu ya Mungu.

4.Ni mara nyingi utasikia watu baadhi tena ni watumishi wakisema fulani biashara yake imekufa ,ndoa yake imevurugika, mtoto wake amefeli, au amefukuzwa kazi au huduma imekufa au maisha yameenda mrama "sisi ndio tulimlaani au tuliomba"(utagundua huu ni uchawi toka kwa miungu) Ukichunguza watu hawa utagundua si wepesi kuonyesha shuhuda za mema waliyoomba.

Kwa miaka ya hivi karibuni nimekutana na baadhi ya watu wana matatizo na misongo ya mawazo na hawafanikiwi, ukishauriana nao unagundua wamelaaniwa na watumishi na kutishiwa vifo na kutokufanikiwa. Je ni Mungu yupi anayetaka tulaani badala ya kubariki!!? utagundua ni miungu inatumia vinywa vya baadhi ya watumishi bandia

Nafasi za utumishi tumepewa bure ni vyema tukazitumia kujenga na pia kujikomboa maeneo ambayo midomo yetu haijakombolewa

Mzazi anajilinda asimlaani mtoto wake halafu anashangaa haeleweki kumbe ameshalaaniwa na baadhi ya watumishi, hili ni jambo la kuomba rehema na kufuatilia pia ibada ambazo zinaweza kuleta madhara hata kwa vijana na mabinti na watu wengine.

Mungu aturehemu na afute kila laana na inayotamkwa ili kuua maono au nguvu. Ndoto na Nuru
Ndimi Mjoli wenu

Jr.View attachment 3129312
Hongera Mshana umetoka kwenye Uganga umehamia kwenye Injili
 
Kuna mtu aliwahi kufanya jamabo lisilo sahihi kwa wazazi wake, nikamwambia UTALAANIWA. Yeye alinijibu LAANA ni sehemu ya VISINGIZIO kwa walioshindwa maisha. Akimaanisha hakuna kitu kinaitwa laana. Lakini naona andiko la laana.
Nitaendelea kujifunza hapa.
Wasiojulikana tumewalaani sana na hakijawapata kitu chochote.

Laana haipo ni kutishana tu miongoni mwetu.
 
kutokutii mamlaka za dunia zilizowekwa na Mungu kupitia sauti ya wengi ni laana ambayo inawatafuna watu wengi bila kujua..😀😀😀
Sio kila mamlaka inatoka kwa MunguView attachment 3129333
Sasa haya masanamu ya Miti na Plastic yanaweza kumpa mtu Mamlaka wakati jayaongei, hayana mdomo, hayatembei mpaka yabebwe kutoka sehemu moja kwenda nyingine? Wala hayana uhai.
 
3.Hili jambo limekuwa likitumika na baadhi ya watu wanaoitwa watumishi wa Mungu pale wanapoona kuna mtu haendani nao au kukinzana nao ...wamekuwa wanatumia laana kama vitisho au silaha ya maangamizi kwa baadhi ya watu.
Yule RC naye pia alilaaniwa na mtumishi mmoja hivi
 
Kwa mfano serikali yetu imewekwa madarakani na wananchi gani ili ipate sifa ya kuwa ipo kwa ridhaa ya Mungu kupitia sauti ya wengi? na vipi wale wanaodhulumu sauti ya wengi laana haiwahusu? vipi hizo serikali zikisha kuwa kwenye madaraka kipaombele chao cha mwisho ndio wananchi laana haiwahusu?
ndio maana unakuta watu wanalalamika tu bila kua na maono ya mbadala wa malalamiko yao..

ndiyo maana wana mihemko, makasiriko na ghadhabu kupindukia ambazo hazina maana, umuhimu wala msaada wowote kwao..

ndio maana roho ya chuki, ukaidi na kiburi vimewajaa na kila wanalopanga linabuma tu, na linalofanikiwa halina matokeo. Laana za kujitakia mbaya sana aise...

laana inamfanya muungwana ajione ni bora zaid ya wote, ajipe umuhimu wa kipekee zaid ya malaika, kwamba asemacho yeye au atakacho yeye ndio cha muhimu na cha maana kuliko wengine..Laana bana dah

Laana inamfanya muungwana awe ni mtu wa kuzira, kugoma na kususa tu 🤣
inafanya mtu aone dosari na makosa ya wenzie tu 🤣

Ni muhimu kutii mamlaka za dunia zilizowekwa na Mungu la sivyo mtapata tabu sana kwa laaana za kujitakia bila kujua 🐒
 
ndio maana unakuta watu wanalalamika tu bila kua na maono ya mbadala wa malalamiko yao..

ndiyo maana wana mihemko, makasiriko na ghadhabu kupindukia ambazo hazina maana, umuhimu wala msaada wowote kwao..

ndio maana roho ya chuki, ukaidi na kiburi vimewajaa na kila wanalopanga linabuma tu, na linalofanikiwa halina matokeo. Laana za kujitakia mbaya sana aise...

laana unamfanya muungwana ajipe umuhimu wa kipekee zaid ya malaika, kwamba asemacho yeye au atakacho yeye ndio cha muhimu kuliko wengine..Laana bana dah

Laana unamfanya muungwana awe ni mtu wa kuzira, kugoma na kususa tu 🤣
inafanya mtu aone dosari na makosa ya wenzie tu 🤣

Ni muhimu kutii mamlaka za dunia zilizowekwa na Mungu la sivyo mtapata tabu sana kwa laaana za kujitakia bila kujua 🐒
Na nyie watu wa kundi lile ndio mmejaa sana humu.
 
IMG_20241011_104647_843.jpg
 
Mkuu umeongea kwa hisia sana japo naona umenukuu kifungu kutoka kwenye biblia na kukitafsiri vibaya alafu kwa muujibu wa hizi picha zako ni wazi unachanganya uchawi na laana, au kurogwa na laana, kiufupi sijui upo upande gani yani umeeleza vitu tofauti ambavyo hauna uwelewa navyo vizuri hebu tafuta kwanza elimu zaidi uelewe vitu hivyo naona hauko sawa
Labda nadhani hujafuatilia mjadala vema. Huyo mdau alisema mamlaka za dunia ziheshimiwe kwakuwa zinatoka kwa Mungu
Mimi nikampinga kwa kusema si kila mamlaka ya dunia ina baraka za kimungu na nikaambatanisha na picha
 
Ndivyo mtazamo wa wasio tii mamlaka za dunia zilizowekwa na Mungu ulivyo maeneo mengi ulimwenguni..

Tujitahidi kuwasikiliza na kuwatii wazazi na walezi wetu, manung'uniko na laumu zao dhidi yetu kwamba tunawapuuza na kutokuwajali, ni chanzo cha kuchuma laana bila kujua.. unaona tu mambo yako hayaendi na muda unakutupa mkono...

Na mbona unaniwekea madhabahu za kishetani gentleman?🐒
Kuna mamlaka za giza duniani na zina nguvu sana.. Take this note
 
Ndivyo mtazamo wa wasio tii mamlaka za dunia zilizowekwa na Mungu ulivyo maeneo mengi ulimwenguni..

Tujitahidi kuwasikiliza na kuwatii wazazi na walezi wetu, manung'uniko na laumu zao dhidi yetu kwamba tunawapuuza na kutokuwajali, ni chanzo cha kuchuma laana bila kujua.. unaona tu mambo yako hayaendi na muda unakutupa mkono...

Na mbona unaniwekea madhabahu za kishetani gentleman?🐒
Za watu kutekwa na kuuwawa nazo mamlaka hizo zinatoka kwa Mungu!?
 
Picha inatisha hivyo vidubwasha kwenye picha viko chumbani mwa mtu na analala usingiz mzuri kbsa.
Huyo tayari ameshauza roho yake na kusaini mikataba na kutiwa mihuri hivyo hana shida hapo yuko salama kabisa.. BTW hiyo ni madhabahu hapo kwenye chumba chake
 
Back
Top Bottom