Laana ya Adam na Hawa

Laana ya Adam na Hawa

storyteller

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2014
Posts
1,511
Reaction score
1,844
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.

Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.

Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..

Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..

Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?

Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?

Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.

Nawatakia Jumapili njema.
 
Safi mkuu ngoja tuwasubiri wenye ufahamu zaidi wa hili
 
Mimi najiulizaga kama huyo mungu hajaumbwa katokeatokeaje maana kitu chenye akili nyingi kama yeye sidhani kama kinaweza kutokea tu kwa babati mbaya mkuu! Kama nikijitazama mimi najishangaa na kujiambia haiwezekani mimi mimi kutokea tu pasipo kiumbe/kiumba kilichosababisha kuwepo kwa sisi wote, je? Si zaidi kwa huyo mungu kushangaza zaidi katokeatokeaje? Tusubiri wajanja watie tim.
 
Yote yatapita(including me and you) ila Neno lake litadumu milele,na ndo ameshasema Hana mwanzo wala mwisho,Kama unadhani anao tafuta utueleze hapa
 
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.

Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.

Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..

Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..

Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?

Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?

Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.

Nawatakia Jumapili njema.

Good question.

Ngoja tusubiri waumini.
Eiyer, Mkuu wa chuo, Tz mbongo, @,,,CO
 
Last edited by a moderator:
Umewahi kujiuliza laana ni nini na kinyume cha laana ni baraka?? Unaweza barikiwa wewe na mambo yote au watu wote wanaokuhusu wakaingia ndani ya hiyo baraka, kimsingi hiyo laana ya adam na hawa iliathiri mpaka mambo yote ambayo lazima tu angekuwa na ushirika nayo, kuanzia ardhi na vyote vilivyotegemeka kwayo, mana yake chochote ambacho adam na hawa wangefikilia au kutengeneza tayali kilikuwa hakina ukamilifu tena.... jiulize kwa hii sayansi na tekn binadam ana uwezo wa kutengeneza kitu cha kudumu milele...
 
Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu
 
Short and clear unamanisha laana aliyotoa Mungu kwenda kwa Adam na Hawa baada ya kula tunda imetransfer (copy yake) moja kwa moja kuelekea kwa wanyama.

Jee ni kweli?
 
Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu

Adam na Hawa (binadamu) v. Viumbe wengine (living organisms) ni nani or kipi kiliumbwa mwanzo?
 
Ukitaka kujua jibu la hapo lazima kwanza utambue lengo la kuumbwa sisi wanadamu. Hapa kuna mkanganyiko juu ya vitabu vya dini tunavyovitegemea kama reference. Mkanganyiko ninaouzungumzia hapa ni mpishano juu ya lengo la kuumbwa na hasa kwa mujibu wa biblia na Qur-an.

Sitaki kuzama sana ndani ya vitabu hivyo na kuchambua kila kimoja kimeeleza nini kwani naweza kusababisha watu wakabadili mada na kuleta udini. Kwa uelewa wangu kutokana na kusoma historia ya "big bang" japokuwa haileti uhusianao wa moja kwa moja, biblia na quran ambavyo uhusiano upo.

Mola wetu aliiumba dunia kwa muda mrefu kabla hajaweka mimea, wanyama na binadamu. Dunia hii ilikuwa chini ya viumbe wengine ambao ni majini. Mungu akaamua kuipamba dunia kwa kuumba mimea na viumbe wengine kama ndege, wanyama wadudu n.k. Kisha akaona ni vema amuumbe binadamu atakaye vitawala na kuvitunza hivi vyote kwa utaratibu wa Mungu. Baada ya adam na hawa kumuasi Mungu laana walipewa wao lakini automatically laana ile.....(to be continue)
 
Iligusa mazingira yake yanayomzunguka. Kwanza aliambiwa adam "atakula kwa jasho lake" kauli hii ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa lazima iguse mazingira yake na katika kufanya hivyo lazima pia kuna viumbe vinadhurika hivyo kuathirika maisha yao. Kwa ufupi hiyo ndo sababu viumbe wengine wanakufa. Ukiangalia utagundua kuwa shughuli zetu wanadamu zinaathiri sana mazingira na hivyo uhai wa viumbe wengine pia kuathirika. Kwa adhabu hiyo aliyopewa adamu inatuonesha kuwa adamu hakuumbwa kufanya kazi zaidi kila kitu kilikuwa kinaandaliwa na Mungu mwenyewe. Kwa hiyo baada ya dhambi ilibidi atengeneze mazingira yake ya kupata mahitaji yake ya msingi kama chakula, mavazi na malazi.
 
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.

Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.

Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..

Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..

Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?

Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?

Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.

Nawatakia Jumapili njema.

Najaribu kufikiri kama watu wasingekuwa wanakufa toka kipindi cha Adam na Hawa. sijui kama kungekuwa hata na nafasi ya kugeuza shingo
 
Back
Top Bottom