Laana ya Adam na Hawa

Laana ya Adam na Hawa

"Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa WANA WA MUNGU.Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya UBATILI; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha katika TUMAINI; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa WATOTO WA MUNGU.Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa.Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia KUFANYWA WANA yaani, ukombozi wa mwili wetu."-Warumi 8:18-23.

Ukisoma biblia ya King James Version, hilo neno viumbe limetafsiriwa "CREATION".
Bila shaka uzito wa kimaana hapo unaongezeka zaidi.

"You're calling me over,
You're pulling me close
With love you surround me,
YOU GIVE ME HOPE
Yeah yeah yey!
You're taking me deeper
You're making me whole
with grace you redeem me, yeah
You restore my soul

Now I'm made new
Because of you..yeah!

You hold my head up
You remind me who I am
You hold my head up
I'm alive in you again
I'm made new (wowowooh)
I'm made new (wowowooh)

Sijui Lincoln Brewster alikuwa anatafakari hiyo mistari hapo juu wakati akitunga hizi lyrics?!

Hawa wakristo wana nyimbo zao na vimaneno vyao ambavyo kama hukisomi na kukielewa kitabu chao utabaki unawashangaa tu.
 
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.

Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.

Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..

Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..

Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?

Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?

Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.

Nawatakia Jumapili njema.

Kiongozi wa nchi anapoamua au kufanya madudu nchi yote inaingia vitani kwasababu KIONGOZI ndio kafanya madudu hayo na madhara ya vita hayataangalia nani kasababisha au hajasababisha.....

Adam alikuwa na mamlaka kwa kila kiumbe hapa duniani kama kiongozi,madudu aliyofanya madhara yake yanaingia kwa kila kimbe .....!!
 
Riwaya!
 
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele
 
Jee unaamini kabla ya kulaaniwa kwa wanadamu (Adam na Eva/Hawa) wanyama walikuwa hawafi?
 
Imani ya kikristo

Ikiwa ni hivyo. Na ikiwa wanyama walianza kufa kabla ya kufa wanadamu or kabla ya laana ya wanadamu, Hiyo laana inawahusu nini wanyama? or Nini kilibadilika kwa wanyama hao baada ya kulaaniwa kwa wanadamu?
 
Laana Ilitolewa Kwa Vitu vingi ikiwemo hadi Ardhi... Adam hakupewa Adhabu ya Kifo tu hata Ardhi ililaaniwa na Jasho la Adam ndo litakalompa Mazao mpk leo hii
 
Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

1 Mwanzo 1 :26

Mbona Umeenda Tofauti na Andiko
 
Mkuu....

Kwa context yako,Mungu ana sura kama yako?
 
Laana Ilitolewa Kwa Vitu vingi ikiwemo hadi Ardhi... Adam hakupewa Adhabu ya Kifo tu hata Ardhi ililaaniwa na Jasho la Adam ndo litakalompa Mazao mpk leo hii

Mkuu kifo sio adhabu ya Asam kukosea bali matokeo ya kula tunda,dhabu ni nyingine kabisa maana matokeo ya kula tunda yalikuwepo hata kabla hajakosea ....
 
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele

Mkuu kwenye Nyekundu hapo umetudanganya, Waliambiwa wazaliane waongeze dunia sasa wangezaliana vipi bila ya kufanya mapenzi??? embu acheni kuleta vistori vyenu vya vijiweni njoo na kitu tangible ili watu wajifunze na sio kuja na hivi vistori sawa boss!!
 
Haswaaaa .....!!

Aisee!

Kwaiyo Mkuu unaamini wale Carnibal animals mfano;
Samaki: Papa, Nzira, Nduaro Chewa etc Walikua wanakula nini?

Wanyama: Simba, chui, duma ect walikuwa wanakula nini?

Ndege wanaokula nyama tu, na wao walikua wakila nini?
 
Kwani ulaji wa nyama hata kwa binadamu ulikuwa tangu mwanzo?

Binadamu alipokosea alileta mabadiliko makubwa sana kwa viumbe vyote....!!
 
Back
Top Bottom