Najaribu kufikiri kama watu wasingekuwa wanakufa toka kipindi cha Adam na Hawa. sijui kama kungekuwa hata na nafasi ya kugeuza shingo
Nini kugeuza shingo!! Hata kupepesa macho hiyo nafasi isingalikupo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Najaribu kufikiri kama watu wasingekuwa wanakufa toka kipindi cha Adam na Hawa. sijui kama kungekuwa hata na nafasi ya kugeuza shingo
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.
Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.
Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..
Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..
Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?
Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?
Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.
Nawatakia Jumapili njema.
Jee viumbe vingine vilianza kufa kabla ya binadmu or baada?
Kiongozi wa nchi anapoamua au kufanya madudu nchi yote inaingia vitani kwasababu KIONGOZI ndio kafanya madudu hayo na madhara ya vita hayataangalia nani kasababisha au hajasababisha.....
Adam alikuwa na mamlaka kwa kila kiumbe hapa duniani kama kiongozi,madudu aliyofanya madhara yake yanaingia kwa kila kimbe .....!!
Mimea na viumbe vingine vilianza kufa kabla ya binadamu..
Kiongozi wa nchi anapoamua au kufanya madudu nchi yote inaingia vitani kwasababu KIONGOZI ndio kafanya madudu hayo na madhara ya vita hayataangalia nani kasababisha au hajasababisha.....
Adam alikuwa na mamlaka kwa kila kiumbe hapa duniani kama kiongozi,madudu aliyofanya madhara yake yanaingia kwa kila kimbe .....!!
Hayo ni kwa Mujibu wa mafundisho ya imani gani?
Imani ya kikristo
Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu
Riwaya!
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
1 Mwanzo 1 :26
Mbona Umeenda Tofauti na Andiko
Laana Ilitolewa Kwa Vitu vingi ikiwemo hadi Ardhi... Adam hakupewa Adhabu ya Kifo tu hata Ardhi ililaaniwa na Jasho la Adam ndo litakalompa Mazao mpk leo hii
Jee unaamini kabla ya kulaaniwa kwa wanadamu (Adam na Eva/Hawa) wanyama walikuwa hawafi?
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele
Haswaaaa .....!!
Aisee!
Kwaiyo Mkuu unaamini wale Carnibal animals mfano;
Samaki: Papa, Nzira, Nduaro Chewa etc Walikua wanakula nini?
Wanyama: Simba, chui, duma ect walikuwa wanakula nini?
Ndege wanaokula nyama tu, na wao walikua wakila nini?