Laana ya Umri inavyoitafuna China

Laana ya Umri inavyoitafuna China

Najua watu wengi mnasema hamjaelewa Kwa kuwa mnawaza mambo ya kustaafu. China kazi nyingi zipo kwenye mfumo wa Mkataba.

Lakini hoja siyo umri bali wenye kazi zao wanataka mtu anayeweza kufanya kazi kwa muda mrefu, kazi kubwa na kwa ustadi mkubwa.

Kwa ivo imeonekana shinikizo la kufanya kazi kwa masaa 12 mfululizo, watu wenye miaka 35 na kuendelea hawawezi.
Na huo ndio ukweli hata mbongo 35+ hawezi kufanya kazi masaa 12+ non stop lazima achoke na lazima aumwe
 
Walegeze sheria za uzazi ili kuijaza tena nchi.
Kuzaa zaa hovyo bila malezi bora kwa watoto ni upumbavu wa kiwango cha juu huu upumbavu ubaki kwa sisi wajinga watu weusi tunao endekeza ngono zembe
 
Sababu kubwa zipo tatu.

1 . Baada ya Japan nchi inayofuatia Kwa kufanya kazi kwa muda mrefu ni China. China Kwa Sasa kufanya kazi Kwa masaa mengi ni kitu kinachohitajika kwa mtu kubaki kwenye ajira.

China ni nchi inayosimamiwa na chama cha kikomunisti Lakini sehemu kubwa sana ya uchumi wake unaendeshwa na makampuni binafsi ya kibepari.

Hayo makampuni Yana ushindani mkubwa sana na Ili yakidhi nguvu ya kushindana ni lazima wafanyakazi wake wafanye kazi kwa bidii na Kwa muda mrefu sana.

Tatizo soko la ajira ni dogo kuliko idadi ya vijana wenye ujuzi na stadi ya kazi hizo na kutokana na udogo Wa soko la ajira, watu wanaotaka kufanya kazi kwa ujira wowote ule wanazidi kuongezeka.

Maana yake watu wenye umri wa miaka 35 na kuendelea wameonekana kuwa baada ya kufanya kazi kwa muda fulani huonekana kuchoka haraka na kushindwa kuhimili shinikizo la kufanyakazi nyingi na kwa muda mrefu.

2. Mahitaji ya bidhaa sokoni ni makubwa.

3. Viwango vya elimu viko Juu sana na vijana wengi Wana stadi za kazi wakati soko la ajirano dogo.
Waongezee na jingine... Watu wenye zaidi ya miaka 35 wengi wanakuwa wana familia hivyo wanakuwa na majukumu mengine ya nyumbani wakati vijana eg miaka 20 wengi hawajaoa na hawana majukumu.
 
Child labor ni kosa kisheria kampuni haziajiri watoto

Kwamba wanaanza kazi na miaka 12 ? Unavuta bangi ?
Sio hoja ya umri. China shahada ya kwanza watu wanapata wakiwa na umri wa miaka 22.

Kwa Ivo Kwa staili ya kufanyakazi Kwa masaa 12+ mfululizo Kwa miaka 10 siyo kitu kidogo.

Hili ni tatizo na ndiyo maana chama cha Kikomunisti China kimelijadili.
 
Waongezee na jingine... Watu wenye zaidi ya miaka 35 wengi wanakuwa wana familia hivyo wanakuwa na majukumu mengine ya nyumbani wakati vijana eg miaka 20 wengi hawajaoa na hawana majukumu.
That's true Ila kuna mwamba atakubishia
 
Najua watu wengi mnasema hamjaelewa Kwa kuwa mnawaza mambo ya kustaafu. China kazi nyingi zipo kwenye mfumo wa Mkataba.

Lakini hoja siyo umri bali wenye kazi zao wanataka mtu anayeweza kufanya kazi kwa muda mrefu, kazi kubwa na kwa ustadi mkubwa.

Kwa ivo imeonekana shinikizo la kufanya kazi kwa masaa 12 mfululizo, watu wenye miaka 35 na kuendelea hawawezi.
Bongo wengi hawatakuelewa kwa sababu hawajui nchi zilizoendelea watu wanavyofanya kazi. Kwa kifupi waambie ni kama mpira wa miguu. Kwa nini mchezeji mwenye mika 35 anakosa stamina na anaitwa mzee wakati miaka 20 ana soko zaidi?
 
Sio hoja ya umri. China shahada ya kwanza watu wanapata wakiwa na umri wa miaka 22.

Kwa Ivo Kwa staili ya kufanyakazi Kwa masaa 12+ mfululizo Kwa miaka 10 siyo kitu kidogo.

Hili ni tatizo na ndiyo maana chama cha Kikomunisti china kimelijadili.
Kwa hio unapingana na mleta mada au unaungana nae?
 
Back
Top Bottom