Zama hizi Ukimkuta mwanaume ana kila kitu, jiulize mara tatu tatu, sio rahisi akuoe, mtapoteza muda halafu atakuja kumuoa mwingine kabisaa...either atakaeolewa ana mchango wa namna fulani kwenye mafanikio ya huyo mwanaume
Ila wanawake inabidi wajifunze at some point, maisha ya kuanza pamoja from the scratch ni maisha mazuri na yana bond kubwa sana,hii bond inaletwa na your love history, ups and downs, better and worse, mvua na jua...na pia yanakua na value kwenu wote wawili yaani kila mmoja anaona thamani ya mwenzake, upendo wa kweli na uvumilivu.
Sasa wanawake wengine anabahatika kumpata mwenye kila kitu, akifika yeye kazi yake ni total destruction kwa huyo mwanaume, hana uchungu hata wa mali aliyoikuta, hawazi namna ya kuendeleza pale mwenzake alipoishia, hana mawazo chanya, zaidi anataka kuweka tamaa kwa sababu ya ubinafsi, ndio maana wanaume wanawaogopa sana wanawake, tena wanaume wengi ambao wamefanikiwa na hawajabahatika kuoa, huwa wanaogopa kuoa sijui kwa nini...labda kwa sababu ya hizi tabia
Wadada kama ukimkuta mwenza amejiandaa kimaisha na amekamilika, jaribu ku add value kwenye ulichokikuta, kithamini na uweke mchango wako, acha ubinafsi na tamaa, heshimu mali ulizozikuta at the end of the day Mwanaume nae atakuona una thamani na mchango kwa namna fulani kweye maisha yake