Tatizo wanawake wengi wa hapa Bongo wako na tamaa kama hii ya Hamisa Mobeto, wanamfuata jamaa kisa ana hela ili awe anazitumia tu pesa na kujianika mitandaoni kuwa kapata. In reality hana any contribution katika maendeleo ya huyo mtu. Siku za nyuma nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke wa dizaini ya Hamisa na Wema, yule mwanamake alijuwa kuwa nina mke na alijitahidi sana kushindana na mke wangu na kutaka nimuache niwe naye yeye.
Najuwa nilifanya kosa kumcheat mke wangu ila haikuwa nia yangu, huyu mwanamke alikuwa kero kwangu, so kwa kifupi nilidhani ningeduu naye angeniacha alone kumbe sivyo. Mdada alikolea penzi na kunipigia simu hata nikimwambia niko na mke wangu anaanza kubwaka, yaani mimi unaniona sifai siyo?
Namwambia wewe na mimi ni marafiki tu huyu ni mke wangu, anakasirika na kuanza kumsaka mke wangu wajilinganishe. Nilikuja kumuacha aliponiambia nimjengee nyumba kama anayoishi mke wangu na nimnunulie gari kama la mke wangu, nikamtalia na kukata line.....Sasa anasema atanikomesha kwanini nimempotezea muda, yaani wanawake kwa kweli mnaboa sometimes.