Mitandaoni tumafundi kweli kweli wa kupiga debe...huyo Jide mwenyewe aliponzwa na maneno ya aina hii, ndio maana alipopelekwa mahakamani akabaki hoi.
Yawezekana kuna mengi yamefanyika nyuma ya pazia ambayo hakuna kati yao yupo tayari kuyaleta hadharani.
Kumbuka Jide ndiye kaamriwa kuomba msamaha na kulipa gharama za kesi hivyo Ruge angetaka kumkomoa Jide angempiga invoice ya mamilioni mpaka Bi dada mwenyewe achanganyikiwe....instead Ruge kasema yaishe na nyimbo ziendelee kuchezwa iwapo Jide ataridhia.
Sasa ni wangapi wanaweza kujua ni nini kiliendelea baada ya hukumu ile? Jide naye ni binaadamu usidhani angekaa kimya ili hali kuna adhabu ya mahakama inayoweza kumuumiza...kuna uwezekano jide alifanya kampeni za chini chini kuyamaliza bila kutaka yawe hadharani na walichofanya wao (Ruge na Jide) ni kuigiza tu kwenye media.
Mkumbuke jide na Ruge ni Waarabu wa Pemba 'nadhani mmeshanierewa'
Au la, tukumbuke Ruge ni mtoto wa mjini, na anajua jinsi ya kucheza hizi gemu..kwa kumrudisha Jide kundini bila kujali Jide ana impact gani kwa clouds, ni namna nzuri sana ya kuwapunguza nguvu wale wote walioanza/wanaoendeleza chokochoko za kuishutumu clouds kwa kutumia mgongo wa Jide...ofcoz ipo wazi kwamba kati ya wote waliojikuta wanatofautiana na clouds, ukimuacha Sugu ni Jide peke yake ndiye alikuwa na nguvu ya kujadiliwa....leo hii hata Ruby aongee anavyotaka hamuoni kuwa hana tena popote kwa kuegemea? au hata TID ni nani hata anampa uzito wowote.