Lady Jay Dee lazima ukubali, huu ni wakati wa Zuchu

East Africa jide hafanani na kikaragosi chochote cha jinsia yake jide ni comando na msanii mzuri kweli kweli
Kwani Jide ana nini haswa cha tofauti kwenye muziki.. Au kutangulia kuimba?
 
Zuchu ana kitu ndio maana watu wanaweweseka.

Wanasema kwa kuwa yupo Wasafi ndio maana anazungumzwa lakini tukumbuke hata Queen Darlin yupo Wasafi toka inaaanza.

Kama una jicho la ziada lazima ukubali kuna kitu kwa huyu mtoto tena kikubwa.

Huo ung'aavu ndio unawafanya mpaka waliotangulia kuweweseka.
 
Wakati ukuta, sauti moja imezoeleka sana kwa watu.
 
Kwa nini asifananishwe labda? Hao uliowataja wamefanya nini ambacho Zuchu awezi kukifanya?

Ishu si wameimba tu tena wote hao wote hawana uwezo wa kuandika nyimbo zao wenyewe. Zuchu ni mwandishi wa nyimbo zake anaandika yeye mwenyewe.

Tatizo tumekalili kila aliyetangulia ni mkali kuliko atayekuja kesho.

Kutangulia sio kuwa mkali kuliko wote, kina Lady Jaydee tuwape heshima ya kutangulia kwenye game na kufungua milango ya kuimba kwa kina dada ila haimaanishi wao ndio wakali kuliko kila mmoja.
 
Mkuu sio mimi niliomringanisha ni watanzania ndio wanasema uwezo wa Zuchu ni mkubwa kuliko hao waliomtangulia.
Na unaposema hawezi kupafom yeye kama yeye ni lini umemuona kasimama jukwaani akashindwa kupafom? Tuwasikilize watanzania sio wajinga.
Watanzania gani?

Ama tunao comment hapa ni wa'kenya?

Too much promotions erode brand
 
Power of Promotion, assume Zuchu asingekua chini ya WCB au wasingemfanyia hiyo promo kubwa walioyoifanya yaani angekua wa kawaida sana kuliko hata Queen Darlin ambaye hajawahi kufanyiwa any kind of big promo na kaka yake/Management,
 
Power of Promotion, assume Zuchu asingekua chini ya WCB au wasingemfanyia hiyo promo kubwa walioyoifanya yaani angekua wa kawaida sana kuliko hata Queen Darlin ambaye hajawahi kufanyiwa any kind of big promo na kaka yake/Management,
Kwani hao wasanii wakubwa kina Nandy hawafanyiwi promotion?

Mind you, Zuchu ametoa extended playlist akiwa anasikika katika platforms chache kushinda kina Nandy na wengineo

Ni mapema mno na sio heshima kabisa kuanza kumlinganisha Zuchu na Legends kama Jide ambao wametengeneza framework kwa wasanii wengine wote wakike kwa waume lakini ni mapema mno kuanza kubeza kipaji cha zuchu kisa tuu yupo WCB

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania gani?

Ama tunao comment hapa ni wa'kenya?

Too much promotions erode brand
Wewe unawakilisha haters, nenda youtube, tiktok na instagram ndio utawajua watanzania naowazungumzia.
 
Mimi ni shabiki wa WCB, lakini lazima tukubaliane Kipaji cha Zuchu ni cha kawaida mno, yuko highly overatted, (Zuchu - WCB = Zero)Siwezi kumfananisha hata na Gigy Money wa Nampa Papa au Queen Darlin
Yani kumtaja tu Gigy Money kwenye uimbaji nishaelewa uwezo wako wa kufahamu muziki, haustaili kuwepo kwenye hii thread.
 
Media zote kubwa za burudani hazijawai piga nyimbo za Zuchu lakini watu bado wanalalamika anabebwa na promo, ila anaepigwa na kila media hapa nchini wanasema anabebwa na uwezo.

Ngoja muda utasema na tutaelewana.
 
ningekuw karibu hapo ningekupiga bonge la kofi kwann unakuwa mbishi unapoelekezwa na wanao elewa mziki?
zuchu bado saaan kumfananisha na hao watu mbali na jayde
Wananchi ndio walaji wa muziki ndio kipimo nani anaejua muziki. Ndio maana wote wanaosifiwaga hapa ni mafundi wa muziki uwezi kukuta wamepenya uswahilini.

Mnaowaita janjajanja au waimba taarab ndio utakuta gumzo mtaani wanawakosha watu balaa.
 
Wewe unawakilisha haters, nenda youtube, tiktok na instagram ndio utawajua watanzania naowazungumzia.
Ok, naenda huko uliposema.

Ila kabla sjaenda nikukumbushe tu, 'too much promotions erode brand'

Ni muhimu promotion iendane na quality ya brand.
 
Media zote kubwa za burudani hazijawai piga nyimbo za Zuchu lakini watu bado wanalalamika anabebwa na promo, ila anaepigwa na kila media hapa nchini wanasema anabebwa na uwezo.

Ngoja muda utasema na tutaelewana.
ndio kinachoshangaza hapo, Kuna watu kazi zao zinapigwa E FM , Clouds FM , EA Radio, wanapewa interviews kibao kwenye TV zote ila bado kazi zao haziendi ila mtoto wa watu nyimbo zake zinapigwa Wasafi tuu ambayo mkoani haisikiki na bado anawakimbiza halafu wanatuambia promo !!!!

What if angekuwa anapewa airtime clouds, Eastafrica na kwingineko... si wangesema uchawi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…