Hawa wasanii wa bongo mi nawaita wajinga kwa sababu wao ndio wanafiki na wataendelea kuburuzwa na hao clouds mpaka mwisho wa dunia, unafiki wa kwanza ni kutoziamini/kudharau redio nyingine na kuona kuwa nyimbo zao haziwezi ku hit mpaka zipigwe na clouds. Na unafiki wa wao kwa wao wasanii ambao wanatukuzwa na kupambwa kijinga na clouds kwa nia ya kuibiwa wanawatenga wasanii wengine wanajiona wao ndio wao lakini wakibwagwa ndio wanalalamika na kutaka msaada(ndio yaliyomkuta jay dee) ushauri wangu kwa wasanii jikazeni lenu liwe 1 unganeni kiukweli sio kinafiki, mtakuwa matajiri wa kubwa na hamtolalamika ovyo. Maana kwa unafiki wao ndio unawasumbua
LADY JAY DEE: CLOUDS FM NI WANAFIKI, WANATAKA WAHONGWE ILI WAPIGE NYIMBO ZA WASANII
Mwanamziki nguli wa Bongofleva, Lady Jay Dee ameamua kuwapa madongo Clouds FM kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay Dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu.
>> Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo pichani
Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".
Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa hasa Mr II aka Sugu
Ni lazima utakuwa miongoni mwa wale wanaotafutwa na dr Manyau nyau!Unatema nyongo as if wewe ndo clouds!Sasa zile kwaya anazoimba nani anataka kusikia...???? Watu wamejipanga wamemkalia juu anahaha kutafuta mlango wa kutokea heheheheeeee.... jitahidi kuomba mungu akupe mtoto walau mmoja ulee mama.. huu muziki unaung'ang'ania ila wenyewe haukutaki... nilikukubali way back not now adayz hata ningekuwa mimi dj au presenter nisingecheza ngoma zako.. hauvutii kusikilizwa Mama.
Walewale wapenzi wa nataka kulewa. Jaydee ni Mwanamuziki halisi kwa sababu anatumbuiza na Live band na siyo hao masharobaro wenu wanaoweka CD na kuimba playback. (Computer artist ).Jay dee amefulia alikuwa zamani nyimbo yake haina ubora hata chembe inapigwa sababu ya ukongwe wake tu
Hawapigi tena track redioni, na hata kwenye TV hamnioni, na jina haliendi chini.
Najua mnashangaa hata mi Sijui kwa nini?