Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 9,836
- 7,231
Kama ukifatilia program za superbrand station (kama wanavyojiita). Hawa clouds fm imeonekana dhahiri kabisa ni kikwazo cha maendeleo hapa Tz. Embu nitumie hoja hizi.
1. Kwenye muziki; Hawa clouds wamekuwa wakipiga mziki wa wasanii wao tu ama toka THT au wale ambao meneja wao ni Ruge, au kusaga. Wanatoa promo very selective. Hakuna fairness katika kupiga music na ndo maana hata wakati mmoja wakaingia kwenye ugomvi na mr ii.
2. Siasa; Pia clouds wameonekana kupendelea chama tawala cha CCM katika program zao alafu upande mwingine wana chuki ya dhahiri kwa CHADEMA. Watangazaji wao wawili bwn. Ephrahim Kibonde na Gerald Hando kwenye vipindi vyao moja kwa moja wameonekana wakileta chuki za waziwazi kwa CHADEMA. Ile video ya Lwakatare walijifanya kuikamia sana na kuitangaza huku wakitoa hukumu peke yao badala ya kuiachia mahakama.Ingekuwa kesi ni ya CCM ungemskia Kibonde akisema waziwazi 'suala lipo mahakamani tuwaachie' ila kwa kuwa ni chadema hali imekua tofauti. Clouds ndo mahakama, na hando & kibonde ndo judges. Kifupi hawazingatii ile hoja ya political neutrality au political fairness kama waandishi wanavyopaswa wawe.
3. Maafa yanapotokea..... Clouds wamekuwa wakijipatia pesa kupitia maafa ya watanzania. Nitoe mfano wa mtangazaji wao millard Ayo. Huyu dogo ana page zake kwa internet ambapo analipwa per visit. Kila member wakivisit page yake anaingiza mkwanja. Ok cyo mbaya ni biashara iyo.. Lakini juzi kwene tukio la ghorofa kudondoka ndo akachukulia sehem ya kujipatia ulaji. Kwene facebook anapost stori ya maiti waliopatikana lakini hamalizii anasema ivi 'idadi ya waliofariki hadi sasa iko hapa mtu wangu wa nguvu...' afu anaacha link uvisit. Uyu dogo hana ubinadamu kabisa! Suala la maafa ya kitaifa yeye anatumia kuipatia kipato?
4. Michezo...
Pole, kwani wewe mpaka leo hii unasikiliza Clouds FM, mbona redio ziko nyingi siku hizi?