Lady Jaydee: Naamka tena baada ya siku 30

Lady Jaydee: Naamka tena baada ya siku 30

Huwa namkubali sana ila huo wimbo usije kuwa unahusu taraka maana huwa hachelewi kutunga matukio yanayomtokea karibu tena jd.
 
Nilisikia fununu anamimba , kama kweli hongera zake , Mungu amlinde ajifungue salama
 
Aiseee kumbe! Alirudisha makazi bongo toka was it Germany or Netherlands! ??
 
Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena kwenye muziki baada ya ukimya wa muda kidogo kwenye muziki. Lady Jaydee ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki baada ya siku 30 kuanzia leo.

Wiki kadhaa zilizopita Lady Jaydee aliwahi kuwaomba wapenzi wa muziki wake kuwa wavumilivu na kuwataka wasubiri kwani kwa kipindi hicho alikiri wazi kuwa hana kitu cha kuimba wala hakuwa na mizuka ya kuimba, kutokana na mambo yake ya hapa na pale na kuwataka wapenzi wake kwenye muziki kudumisha amani.

“Karibu tu lakini sina lolote kwa sasa, sina kabisa na sitakuwa nalo kwa kipindi kirefu sana, yaani sina, sina, sina. wapenzi huvuta subira mashabiki huhama hama. Wapenzi vuteni subira na dumisheni amani” Aliandika Lady Jaydee.

Baada ya ukimya na mashabiki kuanza kuhoji juu ya ukimya wake kwenye muziki, mwanadada Lady Jaydee alikuja na kuweka wazi kuwa amekuwa kimya lakini hawezi kufanya lolote sababu hakuwa na jambo la kusema au kuimba kwa wakati huo na kuwataka tena mashabiki na wapenzi wa muziki wake kuwa wavumilivu.

“Ni kweli sijasema ,ni kweli nimekaa kimya lakini siwezi sema tu endapo sina cha kusema mnaweza kuvumilia? Kama ninavyo vumilia? Napumzika tu sina cha kufanya mvumilie nitarudi sema sina cha kusema na siko tayari kusema, nitasema nikiwa tayari kusema” Alimaliza Lady Jaydee.

Lady Jaydee sasa amepata cha kusema na amepata ya kuzungumza na ndio maana ametangaza rasmi ujio wake mpya kwenye muziki wa bongo fleva, Jide amesema kuwa baada ya siku 30 kuanzia leo atasimama tena.
Anasubiri stress za talaka zipoe.Pole sana Jaydee!
 
nyie mnaosema jide ajipange nafikiri wengi wenu ni kizazi cha diamond music time.ila kama mngekuwa mnjua muziki wa bongo.mgejua jide katoka wapi na akina nani.wenzake wote wamepotea ila yeye bado yupo.leo hii unasema ajipange..kwa lipi jide ana kipaji na muziki anaujua.sana..nyie ndo mnamlinganisha jide na watoto wadogo kwenye game.
 
Huyu aliacha mziki kama kiba.
Alidai anakwenda kuishi ujerumani mziki basi.
Kakurupuka huko atakuta watoto wamekaza ataanza kulia anahujumiwa
Alisema wapi anaenda kuishi ujerumani? mbona unakua mbea, shigongo ndie aliandika huo upuuz
 
Uzuri wa jay Dee watu wala huwa hawahitaji video ili wakubali kazi zake. . Trust me, hata asipotoa video atahit sana tu......Jay Dee ni mashine nyingine kwa Tz hakuna
Ni kweli kabisa, yule mwanamke ni moto wa kuotea mbali, huwa habahatishi
 
Hakuna anaeweza kushindana na Jide kwa kizazi hiki. Hao kina linah Vanessa mwasiti wameshakubali hilo ni vikwazo tu vya kimaisha ndio vinamsumbua Jide ila hakuna kabisa wa ligi yake.
Ni kweli jide ni level nyingine
 
nyie mnaosema jide ajipange nafikiri wengi wenu ni kizazi cha diamond music time.ila kama mngekuwa mnjua muziki wa bongo.mgejua jide katoka wapi na akina nani.wenzake wote wamepotea ila yeye bado yupo.leo hii unasema ajipange..kwa lipi jide ana kipaji na muziki anaujua.sana..nyie ndo mnamlinganisha jide na watoto wadogo kwenye game.
waambie hao hawajielewi, jide kaanza kuimba toka huyo domo wao hajazaliwa sasa sijui wanataka ajipange nn
 
Gadna sijui alimfanya nini huyu demu ???? maana toka waachane demu hasomeki, kachanganyikiwa kabisa kila kitu kwake kimekuwa hovyo, wakati Gadna yeye anaendelea na maisha yake kama kawaida.
images
 
Changamoto za mahusiano,kila mtu anakiwango cha namna ya kukabili....muda unatibu Mungu anaendelea kumpa nguvu atasimama tu.
 
JD si Msanii wa kubeza, video zake nyingi zimekwisha onyeshwa kwenye TV stations nyingi za nje na zikafanya vizuri.
Jide keshafanya Kolabo na Nguri wa muziki barani Afrika "Oliver Mtukuzi".
 
Back
Top Bottom